Skip to main content

Posts

Showing posts from October 6, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

BEI MPYA ZA MAFUTA ZATANGAZWA, PETROLI YAFIKA SH4,348 KWA LITA

  MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo mpya za petroli, dizeli na mafuta ya taa zitakazoanza kutumika kuanzia Jumatano, Oktoba 7, 2026, saa 6:01 usiku. EWURA imesema ongezeko hilo limechangiwa na kupanda kwa bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia kutokana na kuibuka upya kwa mgogoro wa kisiasa katika Mashariki ya Kati. Kwa bei za rejareja katika bandari, Dar es Salaam petroli itauzwa hadi Sh4,057 kwa lita, dizeli Sh4,086 na mafuta ya taa Sh4,067. Tanga, petroli itauzwa hadi Sh4,123, dizeli Sh4,152 na mafuta ya taa Sh4,133 kwa lita, huku Mtwara petroli ikiwa Sh4,170, dizeli Sh4,199 na mafuta ya taa Sh4,180 kwa lita. Kwa baadhi ya maeneo ya ndani, bei ya juu zaidi ya petroli iliyotajwa katika jedwali la EWURA ni Sh4,370 kwa lita Kyerwa (Ruberwa), Kagera, huku dizeli ikiwa Sh4,399 na mafuta ya taa Sh4,380. EWURA imewataka wafanyabiashara kuzingatia bei kikomo zilizotangazwa na imeonya kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wa...

MAGEREZA YAHITIMISHA MASHINDANO YA BAMATA KWA KISHINDO YATINGA TATU BORA KATI YA KANDA SABA

 Na Ssgt Mawazo Mtondo - DODOMA. Kanda ya Magereza imeonesha uwezo mkubwa katika Mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) 2026, baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kati ya Kanda saba zilizoshiriki mashindano hayo yaliyofanyika jijini Mwanza kuanzia Septemba 21 hadi Oktoba 3, 2026. Kwa mujibu wa matokeo ya jumla yaliyotolewa leo, Oktoba 6, 2026, Kanda ya Magereza imefanya vizuri katika Mashindano ya BAMMATA 2026, baada ya kutwaa vikombe viwili vya mshindi wa kwanza kupitia michezo ya wavu kwa wanaume na wanawake, pamoja na vikombe vinne vya mshindi wa pili, vikiwemo mpira wa pete na kurusha vishale. Aidha, Katika riadha, Kanda ya Magereza ilipata kikombe cha mshindi wa pili kupitia Inspekta Catherine Lange, aliyeshika nafasi ya pili katika mbio za Half Marathon. Mafanikio hayo yanaonesha ushindani wa Kanda ya Magereza katika mashindano yaliyowakutanisha wanamichezo kutoka vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama nchini, kwa lengo la kuimarisha umoja, mshikama...

TARURA NJOMBE YAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA.

 #Wananchi sasa kuzifikia huduma za kijamii kirahisi Njombe Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Wilaya ya Njombe imeendelea na kazi ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara ili kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji kwa wananchi. Hayo yamebainishwa na Meneja wa TARURA katika wilaya hiyo Mhandisi Costantine Ibengwe ambaye ameitaja miradi inayotekelezwa kwa sasa kuwa ni pamoja na ujenzi wa Barabara ya NBC- Kibena kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 2.84, mradi wa ujenzi wa daraja la mawe lenye urefu wa mita 31 linalounganisha Kata za Mji Mwema na Ramadhani ambapo ujenzi huo umefikia asilimia 70. Kwa mujibu wa Mhandisi Ibengwe mradi mwingine unaotekelezwa katika Wilaya hiyo ni pamoja na ujenzi wa Barabara ya Mama White Kilomita 1.5 kwa kiwango cha changarawe ambapo barabara hiyo tayari imekamilika na inatumika. " TARURA katika Wilaya ya Njombe tunatekeleza miradi hii ili kuwawezesha wananchi kusafiri kwa urahisi na kufanya shughuli zao za kila siku...

ASIYESIKIA LA MKUU HUVUNJIKA GU

 📍 Tujiadhari na mvua za Elni-nino Na Mwajuma Selemani (Madam Nice) 0713689868 Ilikuwa mwaka 1993, nikiwa bado mtoto, katika Kijiji cha Jitengeni, Kata ya Mombo, Wilaya ya Korogwe Vijijini. Kulikuwa na mvua za rasharasha zilizokuwa zikiendelea kunyesha kwa wiki hiyo. Kwa kweli, hazikuwa mvua kubwa sana za kutisha. Ilikuwa asubuhi, mpiga mbiu alipoanza kutangaza: “Tangazo! Tangazo! Tangazo! Tunawatangazia watu wote katika Kijiji hiki cha Jitengeni kwamba kuna hatari ya kutokea mafuriko. Hivyo, tunaombwa tuondoke sisi pamoja na familia zetu. Narudia tena: Asiyesikia la mkuu huvunjika guu, na mchelea mwana kulia hulia yeye.Serikali inawaomba sana wote mlioko mabondeni mhame mpaka hali itakapokuwa salama.” Mpiga mbiu aliendelea kurudia tangazo hilo mara kadhaa. Hata alipokutana na mtu mmoja mmoja, alimsihi wahame. Kwetu sisi, ilikuwa ni kama kupigia mbuzi gitaa, maana hakuna aliyemjali. Kila mtu alimpuuza. Walioenda shambani kulinda mpunga waliendelea na shughuli zao. Wengine waliende...

DR. MNYEPE OPENS 7TH TANZANIA-MOZAMBIQUE DEFENCE AND SECURITY MEETING IN DAR

By Prosper Makene  The Permanent Secretary of the Ministry of Defence and National Service, Dr. Faraji Kasidi Mnyepe, has officially opened the 7th Session of the Joint Permanent Commission for Cooperation (JPCC) on Defence and Security between Tanzania and Mozambique. The meeting was opened on 5 October 2026 at the Aga Khan Diamond Jubilee Hall in Dar es Salaam. Dr. Mnyepe said the cooperation between the two countries in defence and security diplomacy has a long history, built on good neighbourliness, friendship and shared interests of their peoples. "This meeting is an important opportunity for both sides to jointly assess defence and security issues, exchange experience and expertise, and discuss areas to further strengthen cooperation," he said. The session is attended by Permanent Secretaries, representatives of Heads of Defence and Security Organs, and experts from Tanzania and Mozambique. Dr. Mnyepe urged delegates to deliberate in depth and with a common perspective ...