Skip to main content

Posts

Showing posts from October 5, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

KENYA YATHIBITISHA KISA CHA KWANZA CHA EBOLA, MGONJWA AFARIKI

  Wizara ya Afya imethibitisha kisa cha kwanza cha ugonjwa wa Ebola nchini Kenya, huku mgonjwa aliyekuwa akiugua akifariki Jumatatu usiku mjini Nairobi. Waziri wa Afya Aden Duale alisema Jumanne, Oktoba 6, kuwa mgonjwa huyo alikuwa ametoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kupitia Uganda, kabla ya kuwasili Nairobi. Duale alisema mgonjwa huyo alikuwa akiishi na kufanya kazi DRC kwa miaka saba na alianza kuugua takriban mwezi mmoja uliopita. Alitibiwa katika hospitali kadhaa nchini humo kabla ya kusafiri kwa barabara kupitia Uganda kurejea Kenya. “Wizara ya Afya inawafahamisha wananchi kwamba imethibitisha kisa cha kwanza kilichoingizwa nchini cha ugonjwa wa Ebola  aina ya Bundibugyo,” alisema Duale. Mgonjwa huyo baadaye alipanda ndege ya Jambojet iliyokuwa na abiria 23 na wahudumu wanne, na kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) Jumamosi, Oktoba 3, saa  saba mchana. Alifanyiwa ukaguzi wa kawaida wa afya JKIA kabla ya kupita katika kituo ...

UFANISI NA MAFANIKIO MAKUBWA YA DKT SAMIA YACHOCHEA MWAMKO WA UONGOZI KWA WANAWAKE.

Mjumbe wa Baraza kuu la UWT Taifa ngazi ya viti vitano Tanzania bara Mariam Sagini amesema kuwa ufanisi na mafanikio yanayofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yamechochea mwamko wa uongozi kwa wanawake. Ameyasema hayo Oktoba 4,2026 wakati wa kilele cha wiki ya Jumuiya ya wanawake Tanzania ( UWT) ya chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mara katika viwanja vya chama hicho Kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma. Mjumbe huyo amesema kuwa juhudi anazofanya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa ambae ndie Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimeendelea kuwa kichocheo kwa wanawake kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi. " Mimi kama mwanamke kiongozi ngazi ya viti vitano Tanzania bara naendelea kuona namna ambavyo wanawake wenzangu wamekuwa na mwamko mkubwa ndani ya chama wakikipambania chama chao kuanzia ngazi za Matawi,vijiji, Kata,wilaya mpaka Taifa", amesema Mariam. Ameendelea kusema hakika hamasa hiyo kubwa imetokana na Rais wa awamu ya sita kuonyesha ufanisi mkubw...

TASAC, NBS KUANZA SENSA MAALUMU YA VYOMBO VYA MAJINI TANZANIA BARA

 Na Mashaka Mhando, Tanga SERIKALI kupitia Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), imeanza maandalizi ya kufanya sensa maalumu ya vyombo vyote vya majini Tanzania Bara ili kuwezesha mipango sahihi ya maendeleo, usalama, na huduma za uokozi. Sensa hiyo ya kimkakati itahusisha vyombo vyote vya majini bila kujali ukubwa au eneo vinapofanyia shughuli; ikiwemo meli, boti, mashua, mitumbwi, pamoja na karakana zinazojihusisha na ujenzi wa vyombo hivyo. Akizungumza na kituo hiki, Ofisa Mfawidhi wa TASAC Mkoa wa Tanga, David Chilagi, amesema zoezi hilo linalenga kuibua idadi halisi, maeneo vilipo, pamoja na aina ya vyombo vinavyotumika katika shughuli za usafirishaji na uvuvi. "Tunapotambua idadi halisi ya vyombo na maeneo vilipo, tunakuwa na uwezo wa kujua wapi tunapaswa kuongeza elimu ya usalama, wapi tunahitaji kuimarisha huduma za utafutaji na uokozi, na wapi wananchi wanahitaji kupewa kipaumbele katika mipango ya maendeleo,...

DKT. MWIGULU AFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU MWENYEKITI WA BUNGE LA VIETNAM

 Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo, Oktoba 5, 2026, amefanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Vietnam, Mhe. Nguyen Hong Dien, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), kando ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU). Viongozi hao wamejadili namna ya kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Vietnam na kupanua ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili.

RAIS SAMIA AHIMIZA HATUA ZA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA ΝΑ ΜΤΟΤO BARANI AFRIKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kutoa kipaumbele kwa ajenda ya Afya ya Mama na Mtoto katika utekelezaji wa mipango yao ya kitaifa. Rais Dkt. Samia amesema hayo leo tarehe 05 Oktoba, 2026, alipokutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, Ikulu jijini Dar es Salaam, Dkt. Tedros yupo nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi, pamoja na kushiriki Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), unaofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 05 hadi 09 Oktoba, 2026. Akiwa Kinara wa Umoja wa Afrika wa Afya ya Mama na Mtoto, Rais Dkt. Samia amesema ataendelea kushirikiana na viongozi wa nchi za Afrika kuimarisha afya ya uzazi, kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na ujauzito na kujifungua, pamoja na vifo vya watoto. Amesisitiza kuwa Mpango Elekezi wa Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto, Mtoto Mchanga na Afya kwa Vijana unapaswa kutekelezwa kwa vitendo katika k...

UWAJIBIKAJI KATIKA CHAMA WAMPA TUZO YA HESHIMA AGNES MARWA MBUNGE WA VITI MAALUM (CCM)

 Na Mwandishi wetu Jovina Massano. Jumuiya ya Umoja wa wanawake Tanzania(UWT) wa chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara wamtunuku tuzo ya heshima Mbunge wa viti maalum Agnes Marwa kwa kuendelea kukijenga chama. Tuzo hiyo imekabidhiwa na Godfrey Kavenga Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mara kwa niaba ya Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Mara Nansi Msafiri katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya umoja huo kimkoa yaliyofanyika katika eneo la chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma. Nansi amesema UWT imeona na kutambua jitihada zinazofanywa na mbunge huyo za kuhakikisha chama kinaendelea kuimarika kuanzia ngazi ya shina hadi mkoa. Kilele hicho kimefanyika Oktoba 4,2026 ambapo shughuli mbalimbali zimefanyika ikiwemo uwekaji wa jiwe la msingi kwenye jengo ya UWT Rorya na jengo la UWT lililopo Kata ya Mwisenge . Mara baada ya kupokea tuzo hiyo Mbunge Agnes amewashukuru viongozi wote wa chama na wa Jumuiya ya wanawake kwa zawadi hiyo. Mbali na shukrani hizo hakusita ...

REGINA NDEGE AWAFIKIA KINAMAMA WALIOJIFUNGUA, ATOA MABLANKETI 30 DAREDA

 NAIBU Waziri wa Utumishi na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara, Mhe. Regina Ndege, amewafikia kinamama waliojifungua katika Kituo cha Afya Dareda Kati, Wilaya ya Babati Vijijini, kwa kutoa msaada mbalimbali wa kiutu pamoja na mablanketi 30 kwa ajili ya kituo hicho. Regina ametoa msaada huo Oktoba 3, 2026 alipokuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe za Wiki ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Babati Vijijini, chini ya Mwenyekiti wa UWT Wilaya hiyo, Ndg. Agata. Akiwa katika Kituo cha Afya Dareda Kati, Regina ametembelea kinamama waliokuwa wamejifungua na kuwapatia msaada mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya kuwafariji na kuunga mkono katika kipindi hicho muhimu cha maisha yao. Aidha, alikabidhi mablanketi 30 kwa ajili ya matumizi ya kituo hicho, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi. Baada ya kutembelea kituo hicho, Regina alifika katika Shule ya Msingi Dareda Kati, ambako alikutana na wanafunzi wenye mahitaji ma...