Skip to main content

Posts

Showing posts from June 29, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Museveni Kuwania Tena Urais Nchini Uganda

 Akiwa na umri wa miaka 80, Rais Yoweri Museveni amepuuza wito wa kustaafu, huku wakosoaji wake wakimshutumu kwa kuanza njia ya kimabavu bila upinzani wowote, hata ndani ya chama chake tawala cha National Resistance Movement (NRM). Museveni alichukua madaraka kwa mara ya kwanza kama Kiongozi wa kikosi cha waasi mwaka 1986.  Tangu wakati huo amechaguliwa mara sita, ingawa chaguzi za hivi karibuni zilikumbwa na ghasia na madai ya udanganyifu katika uchaguzi na Ukandamizaji wa Upinzani.  Mpinzani wake mkuu katika uchaguzi uliopita alikuwa msanii maarufu anayejulikana kwa jina la Bobi Wine, ambaye pia alitangaza kugombea katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Januari 2026.  Wine, ambaye jina lake halisi ni Kyagulanyi Ssentamu, ameona washirika wake wengi wakifungwa au kulazimishwa kujificha wakati vikosi vya usalama vilipopambana na wafuasi wa upinzani.  Rais wa Uganda Yoweri Museveni, 80, amethibitisha nia yake ya kugombea katika uchaguzi wa Rais Januari mwakani lich...

Serikali itaendelea kuratibu ajira kwa vijana na mataifa ya nje-Kikwete

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imesema itaendelea kuratibu na kusimamia masuala ya ajira nchi ili kutoa fursa kwa vijana kwa kuzingatia sera na maono ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,  Ajira na Watu wenye Ulemavu, Ridhiwan Kikwete alisema hayo wakati akiongoza na kuzindua Maonesho ya nne ya ajira kati ya Tanzania na China. "Nawahakikishia Watanzania kuwa serikali kupitia wizara itaendelea kuratibu kwa tija masuala ya ajira nchini na kusimamia maslahi ya kisheria, sera na miongozo ya ajira na kazi na maono ya Rais," alisema Kikwete. Maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam yalikuwa na lengo la kutangaza na kuwaunganisha vijana wahitimu na wenye ujuzi na kuwaunganisha na makampuni ya Kichina. Kikwete aliwakumbusha washiriki wa maonesho hayo umuhimu wa kuenzi ushirikiano ulioasisiwa na waasisi wa nchi mbili hizo lakini hatua mbalimbali zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Ra...

Dkt. Biteko Awasili Rwanda Kushiriki Mkutano wa Nyuklia Afrika

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt Doto Biteko Juni 29, 2025 amewasili Kigali nchini Rwanda kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano unaohusu masuala ya nyuklia Afrika. Katika Mkutano huo unaotarajiwa kuanza Juni 30 hadi Julai 1, 2025  nchini humo unajumuisha wadau wa nishati kutoka ndani na nje ya Afrika wenye lengo la  kuharakisha  matumizi ya nyuklia kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuleta mabadiliko ya nishati Afrika. Pamoja na ushiriki wake katika Mkutano huo Dkt. Biteko anatarajiwa kufungua mjadala wenye mada kuhusu nishati Afrika na utashi wa kisiasa. Aidha, katika Mkutano huo Dkt. Biteko ameambatana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba na Mkurugenzi wa Tume ya Mionzi ya Atomiki, Prof. Najat Mohamed.

Umasikini wa Tarime Vijijini na Ajira kwa vijana wamliza Chichake

TARIME KADA wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Nicholas Mgaya Chichake amechukua fomu kuwania ubunge wa jimbo la Tarime Vijijini. Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua fumu hiyo kwenye ofisi za chama hicho amesema kutokana na fursa zilizopo kwenye jimbo hilo wananchi hawapaswi kuwa na hali hizo za kiuchumi Amesema serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan mambo mengi ya maendeleo yamefanyika lakini bado wananchi hali zao za kimaisha hazijalisha. Tunazo fursa za mgodi wa Barrick,Hifadhi ya Serengeti na ardhi ya kutosha lakini wananchi wetu hawako sawa mfukoni " Ndugu zangu leo nimejitokeza kuchukua fumu jimbo la Tarime Vijijini ili nipiganie keki hii tuweze Ä·uila pamamoja. " Ninao uwezo mzuri wa kuwapigania wananchi wa jimbo la Tarime Vijijini muda wa kula ukifika naomba wanichague kwa kula za kishindo",amesema Amesema.

Mmiliki Mwanamke Aongoza Mageuzi ya Uchimbaji wa Shaba Mpwapwa

Mpwapwa,Dodoma Mmiliki wa mgodi wa Ikombo Hill uliopo katika Kijiji cha Matonya, Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Bi. Doreen Kissia, ameibuka kuwa mfano wa kuigwa katika sekta ya uchimbaji wa madini ya shaba, akiwa mwanamke pekee anayeongoza mgodi unaotoa ajira kwa zaidi ya asilimia 98 ya wakazi wa vijiji vya Matonya na Kinusi. Bi. Doreen ameonesha uongozi bora na ubunifu kwa kufanikisha ujenzi wa barabara ya kilomita moja inayounganisha mgodi huo na barabara kuu, jambo lililorahisisha usafirishaji wa madini. Kwa sasa, mgodi huo unazalisha wastani wa tani 30 za madini ya shaba kwa mwezi. Akizungumza katika mahojiano maalum, Bi. Doreen ameiomba Serikali kusaidia kupeleka umeme katika mgodi wake ili kupunguza gharama kubwa za uendeshaji zinazotokana na matumizi ya jenereta. Kwa upande wake, Mhandisi Chacha Megewa wa Tume ya Madini, ametoa elimu kwa Bi. Doreen na wachimbaji wengine kuhusu umuhimu wa matumizi ya teknolojia ya uchenjuaji. Amebainisha kuwa changamoto kubwa kwa wachimbaji wa ...

Tutaendelea Kuilinda na Kuidumisha Amani Nchini-Majaliwa

_▪️Asema falsafa ya 4R ya Rais Dkt. Samia imekuwa msingi imara wa kulinda amani._   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka mkazo katika kulinda na kudumisha amani nchini ili kuhamasisha maendeleo na kuziba mianya ya kuibuka kwa migogoro miongoni mwa wanajamii. Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili Juni 29, 2025) wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufunga kongamano la Afrika Mashariki la Amani lililoandaliwa na The Islamic Foundation, katika viwanja vya shule ya msingi Mirongo jijini Mwanza “Nataka niwaambie bila amani hatuwezi kupata mafanikio yoyote, kupitia kongamano hili mmepata nafasi ya kujadili kuhusu tunu hii ya amani, ambayo wakati wote tumeshuhudia viongozi wa dini mkiwa kwenye majukwaa yenu mkihimiza amani miongoni mwa wanajamii, tuishike tunu hii”. Kadhalika, amewataka Watanzania kuangalia kwa upana wake suala la mmomonyoko wa maadili katika jamii hasa kwa vijana. “Ni muhimu sana suala hili mkaliweka kama agenda katika mikutano n...