Skip to main content

Posts

Showing posts from August 8, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tamasha la Zanzibar Reggae Festival Kufanyika Mambo Club

  Na Andrew Chale-Zanzibar TAMASHA kubwa la muziki wa Rege (Reggae) Zanzibar msimu wa Sita linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia usiku wa Ijumaa Agosti 9-10, 2024, Mambo Club ndani ya Ngome Kongwe, Unguja, Zanzibar. Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Said Omary Hamad 'Side Rasta'  Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa kutambulisha wasanii na utayari wa Tamasha hilo, ameishukuru Serikali kwa ushirikiano ambapo ameomba wadau kujitokeza kudhamini kwani ni Moja ya matamasha yanayoongeza fursa za kiuchumi Visiwani humo. Side Rasta amesema Zanzibar Reggae Festival ni moja ya matamasha makubwa Afrika Mashariki kwa sasa hivyo ni wakati wa Makampuni ya binafsi na taasisi za Kiserikali kujitokeza kuweka udhamini wao. "Muziki wa Rege unahamasisha amani na umoja na upendo. Ni muziki wenye ustaarabu na kuponya pia hivyo hii ni fursa ya kipekee kwa Wadau kujitokeza kudhamini ilikuongeza tija kwa vijana na maendeleo katika Nchi. Side Rasta amesema Kenya wameweza kuipa nguvu mziki...

Sultan Saleh Seif Ampongeza Rais Samia

Na Mwandishi wetu-Rukwa MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mkoa wa Rukwa   MNEC Sultan Saleh Seif amempongeza Rais DK Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi  kutekeleza zoezi la mradi wa mipango ya matumizi ya ardhi ngazi ya vijiji wilaya hadi Mkoa ikilenga kupunguza migogoro ya ardhi ya mwingiliano wa matumizi ya ardhi kati ya wawekezaji, wakulima na wafugaji mkoani humo. MNEC Sultan Saleh Seif ameyasema hayo baada ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi ikiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi Uzingatiaji Matumizi ya ARDHI B Rehema Kishoa kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bi Rehema Kishoa kuutambulisha mpango huo kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani humo. "Mkoa wa Rukwa kumekuwa na migogoro mingi vijijini  kila unapopita utasikia wafugaji hawana maeneo na wakulima wanaingiliwa na wafugaji,mpango huu utatatua changamoto kwa kiasi kikubwa katika mkoa wa Rukwa. Wito wangu Tume ifanye  ja...

Rais Samia Azindua Mradi wa Ujenzi wa Maabara ya Taifa ya Kilimo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 08 Agosti, 2024 ameweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Ujenzi wa Maabara ya Taifa ya Kilimo ikiwa ni sehemu ya mradi unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika ambapo ujenzi wake upo katika hatua za mwisho. Jengo hili lenye  maabara 14 ndio litakuwa Maabara ya Rufaa ya Vituo vyote vya Tafiti za Kilimo nchini vilevile ndipo patakuwa Makao Makuu ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI ili kuacha kutumia vituo ambavyo vipo Mikoani. Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa Mradi huo, Mhe. Hussein Bashe (Mb), Waziri wa Kilimo amesema pamoja na kuwa na hizo maabara 14 kila maabara itakuwa na ofisi yake vilevile kutakuwa na ofisi 14 za utawala ili kurahisisha utendaji wa kazi katika maabara hizo. "Baada ya kuwa tumeanza kujenga hili Jengo tutaongea na wenzetu wanaohusika na mji wa Serikali hapa pembeni kuna viwanja viwili vina square meter kama 60000 ambavyo tumekwisha viomba ili kuweza kuongeza ukubwa wa eneo hi...

Kikwete Ashiriki Uzinduzi wa Kiwanda Cha Sukari

Aeleza kiwanda kilivyotengeneza ajira zaidi ya Elfu 11 kwa Vijana na Jinsi Rais Samia alivyoidhinisha Bilioni 344 kujenga kiwanda hicho. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete aliambatana bega kwa bega na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ziara yake mkoani Morogoro ambapo Jana Jumatano Agosti 07, 2024 alishiriki kwenye Uzinduzi wa Kiwanda kikubwa cha Mkulazi- Mbigiri  cha kuzalisha sukari takribani Tani Elfu 50 kwa mpigo kilichopo Kata ya Mkulazi Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro. Waziri Kikwete amesema ujenzi wa kiwanda hicho ni utashi binafsi wa Rais Samia kuirudisha Morogoro ya viwanda na dhamira yake ya kuongeza ajira kwa vijana ambapo baada ya kuapishwa kuwa Rais mara moja aliridhia ujenzi wa kiwanda hicho kwa kuidhinisha takribani Bilioni 344 ya ujenzi wake. "Kiwanda hiki ni kielelezo cha ushahidi wa dhati kwamba Wewe (Rais Samia) ni Rais wa dhati unaposema au kuahidi unatimiza. Baada ya kuapishwa kuwa Rais mwezi wa 3, m...