Skip to main content

Posts

Showing posts from August 16, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Watu 357 Wakamatwa Katika Oparesheni ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara

Na Shomari Binda-Musoma JESHI la Polisi mkoani Mara linawashikilia watuhumiwa 357 waliokamatwa kwa tuhuma za makosa mbalimbali wakiwemo wanaojishughulisha na uvuvi haramu. Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Mara Salim Morcase, amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika oparesheni iliyofanyika kipindi cha mwezi julai. Amesema katika oparesheni hiyo watuhumiwa 28 waliokamatwa walifikishwa Mahakamani ambapo kesi 8 zilipata mafanikio kwa watuhumiwa kuadhibiwa kwa makosa mbalimbali. Kamanda Morcase amesema katika oparesheni hiyo vilikamatwa pia vifaa vya uvuvi haramu zikiwemo nyavu aina ya makokoro pisi 30,kupatikana kwa pombe moshi ya gongo na watumiaji na wasafirishaji wa dawa za kulevya. Kwa upande wa mifugo kamanda Morcase amesema wamefanikiwa kuokoa mifugo iliyoibwa sehemu mbalimbali zikiwemo ng'ombe 23,mbuzi 5,kondoo 2 na watuhumiwa 17 wamekamatwa. Kamanda huyo wa jeshi la polisi mkoani Mara amesema katika oparesheni hiyo wamefanikiwa kukamata...

Kikwete Akutana na Kufanya Mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo mafupi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) Bi. Ndomba Doran aliyeongozana  na Meneja wa Kanda ya Kati wa ATE, Bw. Leonard Mapha alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma, leo mchana, kwa ajili ya kujitambulisha rasmi kwake na kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuhudumu katika Wizara hiyo.

Rais Samia Ashiriki Mkutano wa SADC- Zimbabwe

Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ Troika Summit), Harare nchini Zimbabwe, leo tarehe 16 Agosti, 2024.

Klabu ya Namungo Yatangaza Jezi Mpya Zitakazo Tumika Msimu wa 2924/2025

  Timu ya soka ya Namungo kuelekea Kuanza Kwa Msimu wa ligi Kuu Tanzania bara 2024/2025 imetangaza Jezi mpya, Zitakazo tumika Kwa ajili ya Msimu huu Uzi huo mpya ambao umeonakana kuwa na mvuto na rangi za kuvutiwa utatumiwa na timu hiyo Katika mashindano ya Ndani na nje.

Askari Kata ya Kisangura Amshukuru Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya ya Serengeti

Na Shomari Binda-Serengeti ASKARI Polisi Kata wa Kata ya Kisangura iliyopo   wilayani Serengeti mkoani Mara, Genuine Kimario amemshukuru Mganga Mfawidhi wa Hospital ya wilaya hiyo Joseph Muhere kuguswa na kusaidia jamii. Shukrani hizo zimepelekwa pia kwa mganga mkuu wa wilaya ya Serengeti Dk.Adam Lusubilo kwa pamoja kufanikisha kupatikana kwa baiskeli mbili za magurudumu matatu kusaidia wenye ulemavu. Akizungumza na George Marato Tv leo agosti 16,2024 askari Kata huyo amesema moja ya majukumu yake ni kuifikia jamii na kujua changamoto na kuweza kusaidia. Amesema askari hana kazi ya kukamata pekee bali jamii inazo changamoto nyingine ambazo hata askari wa jeshi la polisi analo jukumu la kushirikiana kupata ufumbuzi. Askari huyo mwenye cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi akiwa askari Kata wa Kata ya Kisangura amesema katika majukumu yake ya kazi alizitembelea jamii zenye watu wanaoishi na ulemavu wanaohitaji msaada na kufanya jitihada za kuwasaidia. Amesema jamii za fam...

Waziri Jenista Mhagama Akabidhiwa Ofisi na Mhe. Ummy Mwalimu

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama leo Agosti 16, 2024 amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu. Shughuli ya makabidhiano ya ofisi imefanyika Leo tarehe 16 Agosti, 2024 katika Ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali, Mtumba, Dodoma.  Mhe. Jenista amempongeza Mhe. Ummy Mwalimu kwa uongozi wake ndani ya Wizara ya afya kwa kipindi chote alichofanya kazi ndani ya Sekta ya Afya kwa miaka 14.  “Nakupongeza Mhe. Ummy Mwalimu hakika maendeleo haya ya Sekta ya Afya una mchango mkubwa katika kuifikisha Sekta ya Afya hapa ilipo, tutaendelea kushirkiana na kupeana ushauri zaidi katika kazi” amesema Waziri Mhagama. Akikabidhi Ofisi Mhe. Ummy Mwalimu amempongeza Mheshimiwa Jenista Mhagama kwa kuaminiwa na kuchaguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Afya. “Umekuwa Kiongozi mwenye uzofu wa kutosha ndani ya Serikali naamini kwa uwezo wako ulionao pamoja na timu hii ya Wizara unaweza kuendelea zaidi katika kub...

Waziri Mkuu Atembelea Kiwanda na Kituo Cha Utafiti Cha Labiofam-CUBA

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amembelea kiwanda na kituo cha utafiti kinachotengeneza Viatilifu na Viuadudu cha Labiofam kilichopo Boyeros nchini Cuba, Agosti 13, 2024. Kulia kwake ni rais wa kiwanda na kituo hicho  Rod Manuel Valdes. Waziri Mkuu alikuwa katika ziara maalum ya kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Cuba. Tazama habari picha za  matukio mbalimbali Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rodi Manuel Valdes ambaye ni rais wa Kiwanda na Kituo cha Utafiti kinachotengeneza Viatilifu na Viuadudu cha Labiofam kilichopo Boyeros nchini Cuba alipokitembelea, Agosti 13, 2024. Mheshimiwa waziri Mkuu alikuwa katika ziara maalum ya kuboresha mahusiano kati ya Cuba na Tanzania.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kiwanda na Kituo cha Utafiti kinachotengeneza Viatilifua na Viuadudu cha Labiofam kilichopo Boyeros nchini Cuba alipokitembelea, Agosti 13, 2024.  Wa tatu kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Po...

Rais Mwinyi: Serikali Kudumisha Uhuru wa Kuabudu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali zote mbili zitaendelea kudumisha uhuru wa kuabudu kwani ni njia muhimu ya kuimarisha umoja miongoni mwa Watanzania. Rais Dk. Mwinyi ameyesema hayo leo, tarehe 15 Agosti 2024, katika Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) uliofanyika katika Chuo cha Biblia cha Miyuji, Dodoma. Ameeleza kuwa Serikali inathamini kazi zinazofanywa na taasisi za kidini nchini kwani zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi katika maeneo mbalimbali. Wakati huo huo, Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG, Barnabas Mtokambali, amemkabidhi Rais Dk. Mwinyi Tuzo Maalum ya Uongozi Uliotukuka na kuthamini juhudi zake za kuimarisha uchumi wa Zanzibar. Tuzo hiyo ni ya pili kutolewa na kanisa hilo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1939. Askofu Mkuu, Barnabas Mtokambali amempongeza Dk. Mwinyi kwa maendeleo makubwa yanayofikiwa na Zanzibar kwani yanaonesha dhamira ya dhati aliyonayo ya kuwatumikia wananchi. V...