_Asema waandae mapendekezo kuhusu utitiri wa taasisi za udhibiti na kodi_ _Ataka yawasilishwe kwa Waziri wa Fedha, yaingizwe katika Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka huu_ WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka Wakuu wa Mikoa na watendaji wao katika mikoa yote nchini wajipange kutoa taarifa kuhusu uwekezaji na ukuzaji wa biashara kwenye mikoa yao kila wanapotoa taarifa kwa viongozi wa kitaifa. “Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri mbebe jukumu la kuwa mabalozi wa kwanza wa uwekezaji katika maeneo yenu kwa kutambua na kutangaza fursa mbalimbali zilizopo katika maeneo yenu.” “Tubebe hili jukumu, kila Mkuu wa Mkoa anapotoa taarifa atapaswa aseme ameongeza uwekezaji kwa kiasi gani, amekuza biashara kwa kiasi gani na katika kuongeza biashara mpya Ametoa wito huo leo jioni (Jumatano, Machi 11, 2026) wakati akifunga Mkutano wa Kuhakiki Rasimu ya Pili ya Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (Mkumbi II) uliofanyika katika ukumbi wa Kam...
Marato tv - Sauti ya Jamii