Na Shomari Binda-Musoma WANANCHI wa jimbo LA Musoma vijini wamepokea zawadi ya sikukuu ya Krismass na mwaka mpya kutoka kwa Raid Dkt.Samia Suluhu Hassan. Zawadi iliyotolewa ni gari la kubeba wagonjwa( Ambulance) lililokabidhiwa na mbunge wa jimbo hilo Profesa Sospeter Muhongo. Gari hilo limekabidhiwa jana disemba 24 kwenye kituo cha afya cha Kata ya Bugwema na kupokelewa kwa shangwe na wananchi walioshuhudia tukio hilo. Wanavijiji kutoka Kata hiyo yenye vijiji vinne vya (Bugwema, Kinyang'erere, Masinono na Muhoji) wamemshukuru sana Rais Dkt.Samia kwa kuwapatia gari jipya la wagonjwa ambalo litawasaidia kwa huduma za afya. Wanavijiji hao wameahidi kumpatia Rais Samia kura zote za Kata hiyo kwenye uchaguzi mkuu wa mwakani (2025). " Tunamshukuru sana Rais Dkt.Samia kwa zawadi hii nzuri kwetu na tuna muombea maisha marefu ili aendelee kutuhudumia watanzania"anasema Musa Jumapili. Akikabidhi gari hilo mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema Rais ...
Marato tv - Sauti ya Jamii