Skip to main content

Posts

Showing posts from December 19, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wawekezaji Wakaribishwa Kagera

  *📌 Dkt. Biteko asisitiza teknolojia itumike uchakataji zao la ndizi* *📌Dkt. Biteko ahimiza uwekezaji viwanda vya kuongeza thamani mazao ya uvuvi na ufugaji* *📌 Kagera yaongoza kwa uzalishaji zao la ndizi nchini kwa asilimia 60* *📌 Mradi wa Mashamba Makubwa ya Kahawa Kagera kunufaisha watu 10,000* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi wamekaribishwa kuwekeza mkoani Kagera kufuatia hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi ambazo mkoa wa huo umefikia ikiwa ni pamoja na mipango ya maendeleo na fursa nyingi za uwekezaji zilizopo.  Mkoa wa Kagera ni wa pili kwa uzalishaji wa samaki na fursa ya uvuvi nchini ukitanguliwa na Mkoa wa Mwanza fursa ambayo inawanufaisha wakazi wake kwa kuwapatia ajira, lishe bora, kipato na maendeleo ya kiuchumi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa makazi bora kutokana na shughuli za uvuvi. Akizungumza Desemba 19, 2024 katika Uwanja wa Kaitaba wilayani Bukoba mkoani Kagera wakati aliposhiriki katika Tama...

Wakala wa Nishati Vijijini ( Rea ) kugawa Mitungi ya Gesi 9765 katika Mkoa wa Katavi

  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unaendelea kutekeleza Mradi wa usambazaji wa mitungi ya gesi ya kilo 6 kwa bei ya ruzuku, ambapo inatarajia kugawa mitungi 9,765 katika mkoa wa Katavi. Mkuu wa mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko leo tarehe 19 Desemba, 2024 ameupokea rasmi Mradi huo wa kusambaza mitungi ya gesi kwa Wananchi wa mkoa wa Katavi. REA, imeingia mkataba na mtoa huduma; kampuni ya Taifa Gas, kampuni ambayo, itahudumia wilaya 3 za Mkoa wa Katavi kwa kuuza mitungi hiyo ya gesi ya kilo 6 kwa bei ya ruzuku ya shilingi 19,500 pamoja na vifaa vyake, katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji. Mhe. Mwanamvua Mrindoko, amewaomba REA kuhakikisha kuwa teknolojia za nishati safi ya kupikia, zinapatikana kwa wakati na kuwafikia Wananchi muda wote ili kuhakikisha matumizi ya nishati safi yanakuwa endelevu. Mhe. Mrindoko ameongeza kuwa mkoa unaendelea kutoa elimu kwa Wananchi kuhusu matumizi ya nishati safi na amewapongeza Wadau mbalimbali (Wakiwemo REA) wanaosaidia kampeni h...

Dkt. Biteko awataka Wana Kagera Kuungana Kuinua Uchumi wa Mkoa huo.

Na Agela Sebastian ;Bukoba Naibu Waziri mkuu na waziri wa nishati Dk Dotto Biteko amewataka wanakagera walioko ndani na nje kuendelea kuwaunga mkono wawekezaji waliowekeza na wanaotaka kuwekeza ili kuendelea kuinua uchumi wa mkoa huo wenye fursa nyingi za uwekezaji.  Amesema hayo wakati wa jukwaa la uwekezaji mkoani Kagera ampo ni mwendelezo wa wiki ya tamasha la IJUKA OMUKA ambalo linawahimiza wazawa wa Mkoa wa Kagera kurudi nyumbani na kuwekeza ili kuchochea uchumi wa mkoa huo pamoja na kuongeza ajiran kwa wananchi wake husa vijana. "Najua Kuna wawekezaji wengi wanataka kuja lakini maneno ya kukatisha tamaa huwa hayaishi ,na vikwazo ,kama tutaondoa vikwazo na kuwaunga mkono mkoa wa Kagera utabadilika kwani Fursa nilizozisikiliza hapa zikitajwa na mkuu wa mkoa na viongozi wake ni nyingi sana"ameeleza Biteko   Amesema mkoa huo unafursa nyingi kutokana na kuzungukwa na nchi za Afrika Mashariki. Kwa upande wake Waziri wa mambo ya ndani Inocent Bashungwa amesema wata...

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka iwe ni Ofisi ya Mfano katika Kusimamia Haki-DPP

Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu amesema  Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ina  dhamira ya dhati ya kuona kuwa inakuwa mfano katika kusimamia haki kwa kujenga imani kwa wananchi na jamii nzima kwa ujumla. “Tujenge imani kwa jamii na kwa wananchi, jambo la mwananchi likiwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka haitaji kutoa chochote bali aamini kwamba haki itatendeka, jambo hili litafanikiwa kama ninyi mnaoamua kushtaki ama kutokushtaki mtatenda kwa haki na kutokukubali kutumika iwe kwa maslahi binafsi ama ya watu wengine”. Mkurugenzi wa Mashtaka amebainisha hayo wakati akifungua Kikao kazi na Mafunzo ya Nadharia na Vitendo kwa Wakuu wa Mashtaka wa Wilaya na Waendesha Mashtaka Viongozi yanayofanyika tarehe 17 hadi 21 Desemba, 2024 Mkoani Pwani. Amesema, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imepewa jukumu kubwa na nyeti linalogusa haki za watu kwa kuwa wao  wanahusika na kutoa maamuzi ya kushtaki na wakati mwingine maamuzi ya kutokushtaki na hayo yote yanagusa haki za ...

Dkt Biteko apongeza Tamasha la Ijuka Omuka

*📌 Waomba Kujengewa Uwanja Mpya wa Ndege Bukoba* *📌 Apongeza Wawekezaji Kagera* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa kwa maandalizi mazuri ya Kongamano la Uwekezaji mkoani humo litakaloibua fursa za uwekezaji na kukuza uchumi wa mkoa. Dkt. Biteko ametoa pongezi hizo leo Desemba 19, 2024 mkoani Kagera wakati akizungumza katika Tamasha la Pili la Uwekezaji la mkoa huo ikiwa sehemu ya Wiki ya Ijuka Omuka (Kumbuka Nyumbani). “ Nawapongeza waandaaji wa Kongamano hili na kama kuna watu wamekuja kuwekeza hapa napenda kuwapongeza wale mlioitikia wito tangu kwenye kongamano la kwanza na kuja kuwekeza hapa,” amesema Dkt. Biteko. Amesisitiza “ Maombi yangu baada ya mkutano huu waje wengine kuwekeza na tutumie fursa hii ya uwepo wa mkoa huu kijiografia na kutumia fursa zilizopo,” Aidha, amewaasa wananchi wa Mkoa wa Kagera kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa n...

Balozi Dkt Nchimbi awasili Tabora kwa ziara ya siku mbili

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewasili mkoani Tabora kwa ajili ya ziara ya siku mbili. Baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Tabora, na kupokelewa na wenyeji wake, waliiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Ndugu Said Juma Nkumba, Balozi Nchimbi alipata nafasi ya kupokea taarifa ya utendaji wa kazi wa Chama kutoka kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora, Ndugu Wilson Nkhambaku na taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 - 2025, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paulo Matiko Chacha, leo tarehe 19 Disemba 2024.