Skip to main content

Posts

Showing posts from March 18, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

📍19 Machi 2025 🗒️  Dar es salaam ➖19 Mach 2021 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ilipata Raisi wa Kwanza mwanamke Shupavu na jasiri Muongoza njia. Ametimiza miaka minne Tanzania ikiwa na mafanikio makubwa. ➖Mungu kambariki Uwezo na ameweza kuivusha nchi. Amekuja na falsafa ya 4Rs na ametekeleza kwa vitendo. ➖Tanzania imefunguka kimataifa kaleta diplomasia ya Uchumi na kuvutia wawekezaji wa nje.  ➖Ameleta demokrasia katika siasa na kufungulia mariadhiano baina ya vyama vya kisiasa na mikutano ya hadhara. Amefanya maboresho sheria za vyama vya kisiasa na ameunda tume huru ya.uchaguzi   ➖Amefikia hatua za mwisho kukamilisha miradi mikubwa  ya kimkakati SGR, Bwawa la Mwl Nyerere na daraja la Mwanza Kigongo- Busisi.  ➖Ameboresha huduma za  Jamii Afya Elimu, na Maji. Na ndio Champion wa Nishati safi kaleta hamasa kubwa katika utunzaji wa mazingira.  ➖Katika afya amepunguza vifo vya wajawazito na watoto chini ya miaka mitano. ➖Elimu ameboresha miundo mbi...

Mbunge Mathayo Aelezea Mafanikio ya Miaka 4 ya Rais Dkt.Samia Jimbo la Musoma Mjini

  Na Shomari Binda-Musoma  MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amezungumzia miaka 4 ya uongozi wa Rais Dkt.Ssmia Suluhu Hassan na maendeleo yaliyofikiwa. Akizungumza kwa njia ya simu na GMTV leo machi  19,2025 ikiwa ni miaka 4 kamili ya uongozi huo amesema yapo ya kujivunia na yanayoonekana ikiwemo miradi ya maendeleo. Mathayo ameanza kwa kuzungumzia miradi ya elimu kwa kuelezea namna shule mpya za msingi na sekondari zilivyojengwa ndani ya jimbo kwa maendeleo ya elimu. Amesema kwenye Kata za Bweri,Buhare,Makoko na Kigera zimejengwa shule mpya na za kisasa na maeneo mengine kuongezwa madarasa ambayo imekuwa chachu ya elimu. Mbunge huyo amesema kumsaidia mtoto wa kitanzania na wa jimbo la Musoma mjini ni kumpa elimu na hilo limefanyika kupitia serikali ya awamu ya 6 chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan  " Tunapozungumzia miaka 4 ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan tunazungumzia mafanikio yaliyopatikana kwa taifa zima na jimbo letu la Musoma mjini. " Kwenye upande...

Kila Mwananchi Butiama Kufikiwa na Huduma ya Maji Safi na Salama-Sagini

  Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini Leo Machi 18, 2025 amefanya Ziara ya Kusikiliza na Kutatua kero za Wananchi wa Kata ya Kyanyari na kueleza kuwa Utekelezaji wa huduma ya mtandao wa mabomba ya maji safi na salama umefikia asilimia 70 na kazi inaendelea. Mhe. Sagini amesema Vijiji vyote vya Kata ya Kyanyari tayari vimefikiwa na huduma hiyo huku lengo madhumuni ikiwa ni kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma ya maji safi na salama kama alivyotoa ahadi kwenye majukwaa na mikutano mbalimbali na wananchi. "Tumekubaliana sote kuwa tutazidi kuboresha na kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wote kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo," amesema Mhe. Sagini. Naye Diwani wa Kata ya Kyanyari Mgingi Mhochi amesema kuwa Mbunge Sagini aliahidi kuwa Vijiji vya Nyakiswa, Mwibagi na Nyamikoma vya Kata ya Kyanyari vyote vitafikiwa na huduma ya mtandao wa maji safi na salama ambapo tanki la maji lita 150...

Waziri Mkuu Amesema Rais Samia Ametimiza Ahadi Zake Kwa Watanzania

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani ameweza kutekekeza miradi yote ya kimkakati iliyoasisiwa na watangulizi wake  ikiwemo  ya Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli. Amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia  ametimiza ahadi aliyoitoa kwa Watanzania mara alipoingia madarakani ya kuwa hakuna mradi utakaosimama chini ya uongozi wake na kwamba ataendeleza kila kilichoanzishwa na watangulizi wake. Amesema hayo leo Jumanne (Machi 18, 2025) alipozungumza katika Kongamano la kumpongeza Mheshimiwa Rais DKt. Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio ya miaka minne ya uongozi wake  lililoandaliwa na Waandishi wa Habari Mahiri wa Mkoa wa Mwanza kwenye ukumbi wa Tunza jijini Mwanza. Mheshimiwa Majaliwa amesema Rais  Dkt. Samia alipotoa hotuba yake ya kwanza bungeni  aliahidi kuwa miradi yote itaendelezwa na mingine mipya  itaanzishwa. Mheshimiwa Majaliwa amesema Rais Dkt. Samia amefani...

Mh Waziri Mkuu Majaliwa Ashangiliwa Ukumbi Mzima Baada ya Kugusia Tena "Degree" Kwenda Veta

  George Michael Uledi. Waziri Mkuu wa JMT Mh Kassim Majaliwa Majaliwa ni kama amekoleza tena mjadala wa "wasomi" kwenda kujiunga VETA kwa ajili ya kozi za Muda mfupi lakini zenye soko kubwa la ajira kwa sasa! Mh Waziri Mkuu Majaliwa alishangaliwa mara kwa mara na washiriki wa Mkutano huo wa maadhimisho ya miaka 30  tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo Nchini!(VETA). "..tutumie vizuri maadhimisho haya ambayo yamekuja wakati huu kuna mjadala muhimu wa umuhimu wa mafunzo ya VETA kwa "Wasomi " Nchini..." Waziri Mkuu alisisitiza! Tangu Waziri Mkuu kuja na MAONO hayo ya jinsi VETA inavyoweza kupunguza tatizo la ajira kwa "wasomi" wenye Shahada na kuendelea Nchini, kumejitokeza Vijana mbalimbali wenye Elimu ya Shahada na kuendelea ambao wamekuwa wakitoa ushuhuda wa jinsi walivyoweza kujiunga na mafunzo ya VETA na sasa wanafanya shughuli zao mbalimbali ambazo zinawapa kipato kikubwa kuliko ajira za kawaida(ajira za Degree). VETA SASA KUTEMBEA NA MAONO YA M...

Chadema Yasisitiza No Reform No Election

Chama cha Demokrasia na Maendeleo leo, Jumanne Machi 18.2025  kimemueleza Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusiana na msimamo wake wa 'No Reform, No Election' unaolenga kushinikiza mageuzi makubwa ya mifumo ya uchaguzi nchini, na kwamba endapo mageuzi hayo hayatafanyika basi chama hicho kupitia 'nguvu ya umma' kimejipanga kuzuia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu Akizungumza na wanahabari nje ya viunga vya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa muda mfupi baada ya kutoka kwenye ofisi hizo, Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika amesema viongozi wa chama hicho wamelazimika kufika kwenye ofisi hizo kufuatia wito walioupokea hivi karibuni ambao pamoja na mambo mengine uliwataka kufika hapo ili kueleza wanamaanisha nini wanaposema 'No Reform, No Election' Kupitia kikao hicho kilichochukua zaidi ya saa nne, Mnyika amesema viongozi wa CHADEMA wameieleza Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuwa kauli hiyo hawajaitoa kwa bahati mbaya kwani kwa muda mrefu...

Waziri Mkuu Awasili Mkoani Kagera

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Machi 18, 2025 amewasili, kwenye uwanja wa Ndege wa Bukoba ambapo alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatuma Mwasa na viongozi wengine.  Kesho Mheshimiwa Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Jubilei  ya Askofu Msaidizi Methodius Kilaini itakayofanyika kwenye Kanisa Kuu Jimbo la Bukoba.

Wasira Achukizwa na Kampuni Ya Gdm Kuwakopa Wakulima Wa Kahawa Rungwe

   Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Steven Wasira, ameiagiza Kampuni ya GDM kuhakikisha inalipa madeni ya wakulima wa KAHAWA wa Wilaya ya Rungwe ndani ya siku 14, baada ya malalamiko ya wakulima hao kuwasilishwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Machi 18, 2025, katika Stendi ya Mji Mdogo wa Tukuyu.   Wakulima hao wanadai malipo ya zaid ya Shilingi milioni 600 kutoka kwa kampuni hiyo, wakisema ucheleweshaji wa malipo umewaathiri kwa kiasi kikubwa, huku wengi wakikosa fedha za kugharamia mahitaji yao na kuendeleza uzalishaji wa chai.   Akizungumza katika mkutano huo, Wasira amesisitiza kuwa serikali haitavumilia ucheleweshwaji wa malipo ya wakulima, akitoa onyo kali kwa kampuni hiyo kuhakikisha inatekeleza agizo hilo ndani ya muda uliowekwa.   "Natoa siku 14 kwa mnunuzi wa chai wa GDM kuhakikisha wakulima wote wanalipwa haki yao bila visingizio. Wakulima hawa wamefanya kazi yao na wanapaswa kuheshimiwa kwa kulipwa kwa wakati,"...

Familia ya Marehemu King Majuto, yatoa futari kwa Yatima, Wamtaja Rais Dkt Samia

Na Mashaka Mhando, Tanga  FAMILIA ya marehemu Amri Athumani Majuto 'King Majuto', imetoa msaada wa futari kwa watoto yatima wa kituo cha Goodwill Children Home kilichopo kata ya Tangasisi Jijini Tanga. Akizungumza mara baada ya kukabidhi futari hiyo Leo Machi 18 2025, mmoja ya mke wa marehemu King Majuto,  Aisha Mbwana Yusuph alisema wamekabidhi sadaka ya chakula kwa ajili ya watoto yatima hao. Alisema wamesukumwa kutoa chakula hicho kutokana na uwepo wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani lakini pia fedha walizopewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kiasi cha shilingi milioni 30. "Tupo kwenye mfungo wa Ramadhani mara nyingi heri nyingi zinapatikana katika kipindi hiki, hivyo tumeshirikiana na familia kutoa sadaka hii," alisema Aisha. Mtoto mkubwa wa marehemu King Majuto, Othman Amri alisema kuwa lengo lao la kutoa futari hiyo ni kumshukuru pia Rais baada ya kuwapatia fedha hizo ambazo, wameweza nao kutoa sadaka hiyo ili kumuombea mzazi wao huyo. Alisema fedha hizo wam...