📌 Watu zaidi ya 20,000 washiriki Kili Marathon 📌 Awaasa kuzingatia ulaji na kufanya mazoezi 📌 Serikali kuboresha miundombinu ya viwanja vya michezo *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kushirikiana na Kampuni ya Kili International Marathon ambao ni waandaji wa mbio za Kili marathon kuhakikisha mbio hizo zinatumika kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko nchini. Dkt. Biteko ametoa agizo hilo leo Februari 23, 2025 mkoani Kilimanjaro wakati aliposhiriki mbio za Kili Marathon za kilomita 5. “ Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo iangalie namna bora ya kushirikiana na Kili Marathon ili mbio hizi ziwe nyenzo ya kutangaza utalii wetu na kuwa fursa kwa wageni kutembelea vivutio vyetu vya utalii,” amesema Dkt. Biteko. Amesema mbio hizo zimeendelea kuwavutia watu wengi zaidi ndani na nje ya nchi ambapo mwaka huu zaidi ya watu 20,000 wameshirik...