Skip to main content

Posts

Showing posts from August 29, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Balozi Dkt Nchimbi Apokewa na Maefu ya Wananchi Kisesa na Nyanguge

  Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi akiwasalimia wananchi wa Kisesa na Nyanguge wilayani Magu leo Jumamosi Agosti 30,2025 wakati akielekea mkoani Mara kuendelea na kampeni zake eneo la kanda ya Ziwa ikiwa ni baada ya kumaliza mkoa wa Mwanza. Pamoja na mambo mengine Dkt Nchimbi akiwa ni mgombea mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amemnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Magu, Kiswaga Destery  Boniventura pamoja na Wagombea Udiwani. 

Makamu wa Rais wa Zimbabwe Awasili Nchini Kwa Ziara ya Kikazi

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mheshimiwa Kanali Mstaafu Kembo Campbell Mohadi amewasili nchini Agosti 30. 2025 kwa ziara ya kazi ya siku mbili hadi Agosti 31 2025 kwa mwaliko wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango. Alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Makamu wa Rais Mohadi alipokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi na viongozi wengine waandamizi wa Serikali. Akiwa nchini, Mheshimiwa Makamu Rais Mohadi atakuwa na mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango Ikulu jijini Dar es Salaam na baadaye kuzungumza na waandishi wa habari. Aidha, Mheshimiwa Mohadi atatembelea Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha, Chuo cha Kilimo na Mifugo kilichopo Kaole, Bagamoyo na Kituo cha Urithi wa Ukombozi barani Afrika cha jijini Dar es Salaam.

Majaliwa Azindua Matumizi Ya Nishati Safi Kwenye Magereza

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Agosti 30, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika Magereza 129 nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika gereza la Karanga lililopo Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa niaba ya magereza yote nchini. Mpaka sasa vyanzo vya nishati mbadala vinayotumika katika magereza ni Gesi Vunde (BIOGAS), Mkaa Mbadala (Briquettes), Kuni Poa na Gesi Asilia (NATURAL GAS) na umeme. Mheshimiwa Majaliwa amesema hatua hiyo ni ya kupongeza kwa kuwa inaunga mkono maono ya Rais Dkt. Samia ya kuhakikisha jamii yote inatumia nishati hiyo na hivyo kwa kiasi kikubwa kuondoa madhara yatokanayo na matumizi ya nishati isiyo safi.  Akizungumza wakati akitoa taarifa ya mradi huo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu, Msimamizi wa Kitengo cha Kilimo, Mifugo na Utunzaji wa Mazingira kutoka Jeshi la Magereza SACP Daimu Mmolosha amesema lengo la jeshi hilo ni kuhakikisha kunakuwa na chanzo zaidi ya  kimoja cha nishati ili kuepukana ...

NACTVET yatoa ithibati kwa program tano za CBE

Na Mwandishi Wetu BARAZA la Taifa la Elimu na Ufundi Stadi (NACTVET), limezipatia Ithibati Program mpya tano  za Chuo cha Elimu ya Biashara CBE kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya chuo hicho, Profesa Zacharia Mganilwa wakati akizungumza na waandishi wa habari. Alisema kuanzishwa kwa program hizo ni sehemu ya jitihada za Chuo hicho katika kuhakikisha wanatoa elimu bora, ya kisasa na inayoendana na mahitaji ya soko la ajira ndani na nje ya nchi. Alisema wameanzisha Shahada ya Usimamizi wa Biashara (Double Degree) ikiwa ni utekelezaji wa maagizo yaRais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa Agosti mwaka jana wakati wa katika kikao chake pamoja na Hazina na Viongozi wa Taasisi za Serikali na Mashirika ya Uma ya kuwekeza nje ya Nchi. “ Chuo chetu kimeanzisha program hii inayolenga kuwaandaa wanafunzi kuwa mameneja na viongozi bora katika taasisi za umma na binafsi. Programu hii itawawezesha wahitimu kupata ujuzi wa kupanga, kuongoz...