Skip to main content

Posts

Showing posts from January 29, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tanzania na Comoro Kushirikiana Sekta ya Nishati

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko amekutana na Waziri wa Nishati wa Umoja wa Visiwa vya Comoros, Dkt Aboubacar Anli na kukubaliana maeneo kadhaa ya ushirikiano katika Sekta ya Nishati. Awali, Waziri wa Nishati wa Comoros alieleza umuhimu wa ushirikiano kwenye sekta hiyo baina ya Comoro na Tanzania hususan kuanza mazungumzo kwa ngazi ya wataalam ili kufanya upembuzi wa  maeneo muhimu ya kuanzia hususan katika uzalishaji na usambazaji umeme kwenye visiwa hivyo akieleza pia azma ya Serikali yao kuzalisha umeme kwa vyanzo vya nishati ya mvuke (Geo Thermal) inayopatikana kwa wingi visiswani humo. Aidha, aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa maandalizi mazuri na  mkutano wa mafanikio wa Wakuu wa Nchi kuhusu Nishaki uliomalizika hivi karibuni. Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu Dkt.Biteko alieleza utayari wa Tanzania katika kushirikiana na Comoro kwenye maeneo tajwa na kuelekeza taratibu rasmi ili kuweza kufikiwa makubaliano rasmi kwenye Sekta...

Bunge Lapitisha Miswada Miwili ya Marekebisho ya Sheria

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Miswada Miwili ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya 2024, leo tarehe 29, 2025 katika kikao cha pili cha Mkutano wa kumi nane  wa Bunge hilo. Miswada iliyopitishwa leo ni pamoja na  Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mbalimbali (Na.3) wa Mwaka 2024 (The written Laws (Miscellaneous Amendments (No. 3) Bill 2024, na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mbalimbali (Na. 4) wa Mwaka 2024 (The written Laws (Miscellaneous Amendments (No. 4) Bill 2024No. 3) Bill 2024. Akizungumza wakati wa kuwasilisha Miswada hiyo,  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari amesema kuwa  Miswada hiyo inakusudia kufanya marekebisho katika jumla ya Sheria kumi na mbili. "Malengo ya marekebisho haya ni kuboresha utekelezaji wa masharti ya sheria husika na kuzifanya sheria hizi ziendane na wakati na kuleta tija kwa wananchi". Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Aidha, Mwanasheria Mkuu amezitaja Sheria zilizo...

Wasira: Uzee siyo hoja, bado nina uwezo

Na Mwandishi Wetu  CHAMA Cha Mapinduzi kimesema hakitayumbishwa na hoja dhaifu za upinzani kuhusu maendeleo huku ikiutaka upinzani kujipanga vema kuhimili kishindo chake. Aidha, Makamu Mwenyekiti wa CCM - Bara, Stephen Wasira ametoa angalizo kwa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanaotaka kutumia hoja ya umri wake kama mtaji wa kisiasa na kuwataka wajipange vyema. Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Kakubilo wilayani Geita Mkoa wa Geita, leo, Wasira alisema CCM imejipanga kwa kila namna kuwaletea maendeleo wananchi na haitayumbishwa na hoja dhaifu. "Wako watu wanahoji na kusema tumekaa miaka mingi madarakani, hii ni hoja dhaifu kwani tulipokuwa tunapigannia uhuru tuliingia mkataba wa kukaa madarakani kwa muda gani. "Nataka tuwaambie kuwa bado tutakaa sana madarakani, hatuna mpango wa kutoka kwa kuwa tunaongoza kwa ridhaa ya wananchi," alisema. HOJA YA UMRI Alisema viongozi wa CHADEMA akiwemo mwenyekiti wake Tundu Lissu n...

Rc Mtambi ashiriki Dua ya Kumuombra Rais Samia na Taifa

  Na Shomari Binda-Musoma  MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi ameshiriki dua ya kumuombea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na Taifa kuendelea kutekeleza majukumu yake. Dua hiyo imefanyika kwenye Msikiti mkuu wa Ijumaa mjini Musoma ikiongozwa na Sheikh wa mkoa wa Mara Msabaha Kasim. Akizungumza kabla ya kusomwa kwa dua hiyo Sheikh Msabaha amesema hayo ni maelekezo ya Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuber bin Ally kumuombea Rais kutokana na mazuri anayoyafanya. Amesema dini inatambua utawala wa dunia na kwa taifa la Tanzania Rais Dkt. Samia anawafanyia mema watanzania katika kuwaletea maendeleo. Msabaha amesema kwa mkoa wa Mara yapo mengi mazuri ambayo yamefanywa na Rais Dkt.Ssmia na wanamuombea dua ili Mola aendelee kumsimamia. " Tunamuomba Mwenyezi Mungu aendelee kumlinda Rais Dkt.Samia kwa kumpa afya njema na kuendelea kuwahudumia watanzania. "Rakini tunakuombea pia mkuu wetu wa mkoa Kanali Mtambi kwa kuwa tangu umefika mkoa wa Mara umekuwa ukitupa ushirikiano kila tunapo...

Tanzania Yaahidi Kuendeleza Ushiriano Na Burundi Sekta Ya Nishati

📌Burundi yaipongeza Tanzania kwa mafanikio ya nishati 📌Wampongeza Rais Samia kudumisha amani nchini Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Serikali imeahidi kuendelea kushirikiana na nchi ya Burundi katika nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo sekta ya nishati.  Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko katika mazungumzo yake na Waziri wa Nishati na Madini wa Burundi, Mhe Ibrahim Uwizeye aliyemtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.  "Rais Samia ni kinara katika kujenga mahusiano na ndani ya nchi na kimataifa, kama ilivyo kwa uhusiano kati yetu na Burundi ambayo  imewezesha kutekeleza miradi kadhaa ukiwemo mradi wa umeme wa RUSUMO unaoendeshwa kwa ubia wa nchi Tatu za Rwanda, Burundi na Tanzania" Amesema Dkt. Biteko.  Ameongeza kuwa, Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano na Burundi na kuwataka kuimarisha mahusiano kwa wafanyabiashara ili kuondoa migogoro inayoweza kujitokeza na kusababisha usumbufu kw...

Rais Samia akutana na Rais wa Somalia

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud leo kwenye makazi yake Ikulu, Jijini Dar es salaam leo tarehe 29, Januari 2025.

Watu Wawili Wafariki Dunia Mkoani Kagera

 Na Angela Sebastian; Biharamulo. Watu  wawili wa familia moja wamefariki dunia huku Wahisiwa  44 wakiendelea kuwekwa chini ya ungalizi wa wataalam wa Afya wakiwa majumbani kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa marburg uliotokeaWilayani Biharamulo mkoani Kagera.  Watu 281 walihisiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya marburg ambapo 145 kati ya hao waliwekwa chini ya uangalizi katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma baada ya kusambaa kwa ugonjwa huo. Kutokana na taarifa ya Wizara ya Afya watu hao 145 waliokuwa chini ya uangalizi kwasasa wameruhusiwa kuungana na familia zao baada ya wataalam wa afya kujiridhisha kuwa hawana maambikizi ya virusi hivyo. Naibu waziri wizara ya Afya Dk.Godwini Mollel amefanya ziara ya kutembelea Kambi za wahisiwa wa virusi vya Marburg katika Wilaya ya Biharamulo na kupata taarifa juu ya mwenendo wa ugonjwa huo kwasasa kutoka kwa Mkurugenzi wa  huduma za kinga  wizara ya Afya  Ntuli  Kapologwe.  Amesema  wahisiwa ...