Na Shomari Binda-Musoma Viongozi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Wilaya Musoma mjini wamekuwa miongoni mwa wananchi waliojitokeza kushiriki mazoezi ya" jogging" yaliyoandaliwa na mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka. Mazoezi hayo yamefanyika leo septemba 28 yaliyoanzia na kumalizikia kwenye uwanja wa posta ambapo licha ya viongozi hao makundi mbalimbali yameshiriki. Akizungumza mara baada ya mazoezi hayo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma Benedict Magiri amemshukuru na kumpongeza mkuu huyo wa Wilaya kwa kuanzisha utaratibu huo muhimu kwa afya. Amesema mazoezi yana umuhimu mkubwa katika kufanya mwili kuwa na afya njema na kuweza kutekeleza vyema shughuli za kiuchumi. Magiri amesema ilani ya uchaguzi ya CCM inazungumzi pia ushiriki wa michezo na wao kama viongozi wanamuunga mkono kwa kuhamasisha wanachama na wananchi kushiriki mazoezi na michezo. Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka kwa upamde wake amesema anataka Musoma iliyochangamka kwa matukio ya mara kwa mara yakiwemo ya kim...
Marato tv - Sauti ya Jamii