Skip to main content

Posts

Showing posts from April 17, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa,amtaja Rais Samia katika mafunzo ya Jkt

  Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa  kuendeleza mafunzo ya vijana wa JKT. Meja Jenerali Mabele, ameyasema hayo Aprili 17 mwaka 2025 alipokuwa anahitimisha mafunzo ya Awali ya kijeshi kwa vijana wa Operesheni miaka 60 ya Muungano katika kikosi Cha Ruvu JKT kilichopo mlandizi mkoani Pwani. Meja Jenerali Mabele, amewaasa vijana hao kuzingatia Afya zao kwani afya ndio msingi na mtaji mkubwa kwa kijana wa Jeshi la Kujenga Taifa. Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda, Brigedia Jenerali Abubakar Charo, amewataka kwenda kuzingatia Mafunzo ya Stadi za Kazi na Stadi za Maisha kwani ndiyo yatakayowasaidia kujitegemea baafa ya kumaliza mkataba wa Jeshi la Kujenga Taifa.  Kamanda Kikosi Ruvu JKT Kanali Peter Mnyani  akitoa taarifa fupi ya mafunzo amesema mafunzo hayo yalianza...

Dkt. Biteko Ashiriki Mkutano wa Eapp Nchini Uganda

📌 *Tanzania yapongezwa kwa  kuandaa Mkutano wa M300* 📌 *WB, AFDB kuunga mkono EAPP* 📌*Mawaziri wa Nishati Mashariki Mwa Afrika wakutana Uganda* *Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Aprili 17, 2025 jijini Kampala nchini Uganda ameshiriki katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Nishati wa nchi Wanachama wa Umoja wa Soko la Pamoja la Kuuziana Umeme katika Ukanda wa Mashariki mwa Afrika (EAPP) na Mkutano wa Wakuu wa Mashirika au Taasisi za Umeme za nchi wanachama. Kando ya mkutano huo, mawaziri hao walijadiliana kuhusu biashara ya kuuziana umeme miongoni mwa nchi wanachama. Awali akifungua mkutano huo, Waziri wa Nchi wa Nishati  wa Uganda, Mhe. Sidronius Opolot Akaasai amesema kuwa lengo la EAPP iliyoanzishwa Aprili 24, 2005 ni kuwa na uwiano sawa wa raslimali ya nishati katika ukanda huo. Amesema hadi sasa EAPP ina nchi wanachama 13 na idadi inatarajiwa kuongezeka, ambapo nchi hizo zina nishati inay...

Wasira Apokelewa Sikonge, Awasilisha ujumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Ccm

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira amewasili wilayani Sikonge Mkoa wa Tabora na kushiriki mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM ya wilaya hiyo. Wasira amewasili wilayani humo leo Aprili 17, 2025 akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 akiambata na viongozi mbalimbali wakiwemo baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora,  Said Nkumba. Akizungumza na wana CCM katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama Wilaya ya Sikonge, Wasira amesema pamoja na mambo mengine amefika kuwaeleza wanachama kuhusu uamuzi wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama kumchagua Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais wa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka na mgombea mwenza wake ni Dk. Emmanuel Nchimbi. Kwa upande wa urais wa Zanzibar, Wasira amewaambia wana CCM hao kuwa mkutano mkuu uliridhia na kumpitisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi kuwa mgombea wa ...

Serikali yasimamisha huduma za upachikaji figo katika hospitali za Mediheal

Waziri wa Afya Nchini Kenya Aden Duale, amesimamisha huduma zote za  upachikaji figo katika hospitali za Mediheal kufuatia madai ya ukiukaji sheria. Akizungumza leo Alhamisi katika jumba la Afya Jijini Nairobi, Duale amesema kuwa agizo hilo limesababishwa na malalamishi kuhusu taratibu za upachikaji figo katika hospitali ya Mediheal tawi la Eldoret. Duale alisisitiza kujitolea kwa wizara ya afya kulinda usalama wa wagonjwa  na kurejesha imani ya umma katika huduma za matibabu nchini Kenya. Wakati huo huo,waziri Duale ameunda kamati huru ya wataalam itakayofanya uchunguzi kamili kuhusu huduma za upachikaji figo katika hospitali zote za  Mediheal zilizotolewa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na kuwasilisha ripoti yake katika muda wa siku 90 zijazo. Kamati hiyo ina Jukumu la kuchunguza mifumo ya usimamizi ya hospitali hizo, utendakazi wa kliniki, kubainisha iwapo zimetimiza mahitaji ya kimaadili na taratibu za kiusalama za wagonjwa. Waziri huyo amemsimamis...

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Awasilisha Ujumbe wa Rais Samia kwa Rais wa Burkina Faso Ibrahim Traore

Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amehitimisha ziara yake kwa kukutana na Rais wa Burkina Faso, Mhe. Captain Ibrahim Traoré. Mkutano huo ulifanyika jijini Ouagadougou Aprili 17, 2025 na kuhudhuriwa na maafisa waandamizi kutoka Serikali zote mbili. Katika mkutano huo, Mhe. Kikwete alielezea shukrani zake kwa kupata fursa ya kukutana na Captain Traoré na kumkabidhi ujumbe maalum wa Rais Samia. "Rais wangu amenituma nije kuwasilisha Ujumbe Maalum kwako na nimefurahi umenipa fursa hiyo na leo umeupokea rasmi", Alisema Dkt. Kikwete.  Dkt. Kikwete aliwasilisha pia salamu za Rais Samia kuhusu umuhimu wa kuimarisha ushirikiano baina ya nchi za Afrika, hususan kubadilishana uzoefu ili kwa pamoja Afrika iweze kuendeleza rasilimali zake kwa faida ya watu wa bara lao.

Raia wa Haiti wakerwa na magenge, waandamana tena

  PORT-au-PRINCE, HAITI RAIA wa Haiti kwa mara nyingine waliandamana Jumatano wakitaka wahakikishiwe usalama dhidi ya majahili ambao wanaendelea kudhibiti taifa hilo wakipigania uongozi wa nchi. Mvua kubwa ambayo ilikuwa ikinyesha haikuwazuia maelfu kujitokeza barabarani huku wakiteketeza magurudumu ya magari, wakiweka vizuizi barabarani na kupiga kemi kulalamikia kudorora kwa usalama. Polisi wenye silaha walitazama tu raia hao wa Haiti wakiandamana. Hii ni kinyume na majuma mawili yaliyopita ambapo polisi walilazimika kutumia vitoza machozi kutibua maandamano ya maelfu ya raia. Wakati huo, waliokuwa wakiandamana walikuwa wakitembea wakielekea afisi ya Alix Didier Fils-Aime ambaye Baraza la Uongozi wa Mpito Haiti, lilimchagua kuwa waziri mkuu Novemba mwaka uliopita. Ghadhabu za raia wengi wa Haiti zimekuwa zikipanda kutokana na magenge kuendelea kudhibiti asilimia 85 ya jiji la Port-au-Prince ambalo zamani lilikuwa kisiwa cha amani. Serikali ya Haiti mnamo Jumatatu ilitangaza kuwa ...

Makao ya watoto 1,000 kutiwa kufuli, serikali ikiibuka na mpango mpya ‘bora zaidi’

TAKRIBAN makao 1,000 ya watoto nchini Kenya yatafungwa kufuatia mpango wa serikali wa kuanzisha njia mbadala za kuwatunza watoto hawa wenye mahitaji maalum. Serikali, kupitia Baraza la Kitaifa la Huduma za Watoto, imeanzisha mageuzi katika mfumo wa utunzaji wa watoto unaolenga kuanzisha utunzaji wa watoto katika jamii wala sio katika makao ya watoto. Kwa miaka mingi, watoto mayatima na wengine waliotelekezwa na wazazi wao wamekuwa wakitunzwa katika makao ya watoto yaliyoko maeneo mbalimbali nchini. Lakini sasa Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza la Kitaifa la Huduma za Watoto Adanoor Mohamed, kupitia taarifa, anatoa wito kwa wadau katika sekta hiyo kukumbatia mfumo huo mpya wa kutunza watoto.  Mohamed alisema hatua hiyo itawasaidia kulainisha shughuli zao na kuelekeza rasilimali kwa utunzaji watoto katika mazingira ya familia na jamii. “Utafiti umeonyesha kuwa utunzaji watoto katika makazi ya makao rasmi una madhara ya muda mrefu kwa watoto ilhali utunzaji wa kifamilia na kijamii unaleta...

Waziri aomba radhi baada ya kusema wanawake huuawa kwa kufuata hela za wanaume

WAZIRI mpya wa Jinsia, Sanaa, Urithi na Utamadani Nchini Kenya, Hannah Cheptumo, amewaomba msamaha Wakenya kwa matamshi yake yenye utata kuhusu visa vya mauaji ya wanawake alipokuwa akipigwa msasa na wabunge baada ya kuteuliwa kwa wadhifa huo. Akihojiwa mbele ya Kamati ya Bunge la Kitaifa, Bi Cheptumo aliashiria kuwa wasichana wa vyuo vikuu wanaouawa kwenye vyumba vya kukodisha, aghalabu huwa kwenye harakati za kusaka hela. Matamshi hayo yalivutia hisia kali miongoni mwa Wakenya kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi wakitilia shaka uwezo wa waziri mteule katika utekelezaji wa majukumu ya kukabiliana na kero ya mauaji ya wasichana na wanawake ambayo yamekithiri kote nchini Kenya.  Punde baada ya Bunge la Kitaifa kupitisha uteuzi wake Jumatano kama waziri mpya wa Jinsia, Sanaa, Urithi na Utamaduni, Bi Cheptumo aliwaomba radhi Wakenya kupitia mtandao wa kijamii wa X. “Nilipokuwa nikihojiwa, nilitoa matamshi nikijibu swali kuhusu mauaji ya wanawake katika AirBnB. Ningependa kuchukua f...

Madiwani Kibondo waridhia utekelezaji mradi wa Umwagiliaji Lumpungu

Na NIRC ;Kigoma Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya Kibondo Mkoani Kigoma limepitisha utiaji saini mkataba wa utekelezaji ujenzi, uendeshaji na usimamizi wa mradi wa Umwagiliaji Lumpungu.  Mradi huo utakaogharimu zaidi ya sh. Bilioni 150 unalenga kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao, uhakika na usalama wa chakula nchini. Mradi wa umwagiliaji Lumpungu unatarajiwa kutekelezwa kwa ushirikiano kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) katika vijiji vya Kibuye, Kigina, Kisana,Nyarugusu, Kumshawabure, Kukinama,Magarama, na Nyaruhanga. Akizungumza katika kikao maalumu cha baraza la madiwani na wadau wa maendeleo, Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Kibondo, Habili Maseke, amesema kutokana na umuhimu wa mradi huo na mahitaji yaliyopo madiwani hao wamepitisha kwa kauli moja na wana kiu ya kuona mradi huo unatekelezwa kwa wakati.  Aidha lengo la mradi ni kukidhi mahitaji ya ndani pamoja na utoshelevu wa chakula, mahitaji ya malighafi kwa...