Skip to main content

Posts

Showing posts from March 27, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Watumishi wa Ncaa Wapanda Miti 1,000 na Mingine 10,000 Wagaiwa Wananchi

  Na Mwandishi wetu, Karatu -Arusha Watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) leo tarehe 28 machi, 2025 wameunga mkono kampeni ya upandaji miti iliyozinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda tarehe 15 machi, 2025 kwa lengo la kutunza mazingira na kuboresha mandhari ya mkoa wa Arusha ambao ni  kitovu cha utalii hapa nchini.  Akizungumza wakati wa zoezi la upandaji miti lilofanyika ofisi za NCAA Karatu, Afisa Uhifadhi Mkuu anayesimamia sehemu ya Usimamizi wa wanyamapori na utafiti Lohi Zakaria amesema lengo  la zoezi la upandaji miti kwa watumishi ni kuunga mkono jitihada za serikali za kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kutunza mazingira. “NCAA leo tumetekeleza maagizo yaliyotolewa na mkuu wa Mkoa wa Arusha kupanda miti, siku ya leo pekee tumepanda miche ya miti 1,000, tunaungana na serikali kuhakikisha kuwa tunakabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi hasa swala la hewa ukaa ambalo dunia nzima kwa sasa linapam...

Waziri Mkuu Akutana Nlna Mabalozi wa Tanzania Nchi za Zimbabwe na Rwanda

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Machi 28, 2025 amefanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Habib Galus Kambanga (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Dkt. Suzan Kaganda (kulia), kwenye Ofisi ndogo  ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam.

Azania Bank yafuturu na wadau Zanzibar

Benki ya Azania kwa kutambua umuhimu wa mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni moja ya nguzo za Dini ya Kiislam,imeungana na wateja na wadau mbalimbali Zanzibar Kwa kuandaa Iftar kama sehemu ya matendo yanayopaswa kufanywa na wanajamii katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.  Hafla hii ya Iftar imefanyika Zanzibar na kuhudhuriwa na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mh.Mgeni Hassan Juma pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wadau mbalimbali.

Musoma Vijijini Yapania Kuongeza Ufaulu Kwa Kuzindua Kampeni Maalum

  Na Shomari Binda-Musoma  KAMPENI Maalum iliyopewa jina la"Mkomboe Nyangeta na Athumani Kielimu" Musoma Vijijini imezinduliwa rasmi jana machi 27,2025. Jimbo la Musoma Vijijini. Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amezindua kampeni hiyo baada ya kufanyika mjadala wa siku 3 wenye lengo la uboreshaji,ufundishaji na uelewa wa wanafunzi uliowashirikisha walimu,waratinu wa elimu,watendaji wa vijiji,madiwani na wadau mbalimbali. Akizungumza na washiriki wa mjadala huo uliokuja na mapendekezo 16 yenye lengo la kuinua kiwango cha elimu na ufaulu mkuu huyo Wilaya amesema moja ya pendekezo ni kampeni hiyo na kutaka ianze mara moja. Amesema kampeni hiyo itaendana na suala la chakula kwa wanafunzi kuwa cha lazima kwa wanafunzi wanapokuwa shuleni na kuwataka watendaji wa vijiji kuanza utekelezaji wake kwa kuwashirikisha wazazi na walezi wa wanafunzi. Chikoka amesema mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amekuja na maono makubwa ya kuleta mjadala huo kwa kuwaleta w...

Wanafunzi Hazina wa washangaza maofisa UN kwa umahiri wa kujilezea kwa kingereza

Na Mwandishi Wetu WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Hazina ya Magomeni jijini Dar es Salaam wameonyesha umahiri wa hali ya juu kiasi cha kuwashangaza maofisa wa Umoja wa Mataifa  (UN) na wa Ubalozi wa Rwanda walipokuwa wakijibu maswali na kuhusu mauaji ya Kimbari nchini Rwanda. Maofisa hao walitembelea shule hiyo hivi karibuni kwa lengo la kuzungumza nao na kuwaeleza kuhusu yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994 ambapo wanafunzi hao walipata muda wakuuliza maswali na kupatiwa majibu. Pia maofisa hao waliwauliza maswali wanafunzi hao ambao walionyesha umahiri mkubwa katika kuyajibu hali ambayo iliwashangaza maofisa  hao kutokana na udogo wa wanafunzi hao wa shule ya msingi na awali. Kila tarehe 7 Aprili Rwanda imekuwa ikiadhimisha mauaji ya Kimbari yaliyotokea mwaka 1994 ambapo idadi kubwa ya watu wa kabila la watusi waliuwawa na wa kabila la wahutu wenye msimamo wa wastani. Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Habari wa Umoja wa Mataiafa (UN),Nafisa Didi  alisema wameshangazwa na umah...

Uwanja wa Ndege wa Khartoum Wakombolewa kutoka kwa Waasi wa RSF

  Jeshi la Sudan limesema limeuteka tena uwanja wa ndege katika mji mkuu, Khartoum, kutoka kwa wanamgambo wa RSF. Kulingana na jeshi hilo, hatua hiyo inaashiria mafanikio yake ya hivi punde katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka miwili. Jenerali Mahomed Abdel Rahman al-Bilawi, amesema wanajeshi wameilinda kikamilifu na wanaweza kuwaondoa wapiganaji wengine wa RSF ifikapo mwisho wa siku. Jeshi limekuwa likienda kwa kasi tangu kutwaa tena ikulu ya rais wiki iliyopita na raia wamekuwa wakisherehekea barabarani linaposonga mbele. RSF ilikuwa imedhibiti sehemu kubwa ya miji mikuu tangu vita vilipoanza Aprili 2023. Nchini kote, mamia ya maelfu wameuawa, na mamilioni wamelazimika kuyakimbia makazi yao. Aidha msemaji wa jeshi alisemaa wanajeshi wameteka daraja la Manshiya, daraja la mwisho linaloshikiliwa na RSF, pamoja na kambi ya kijeshi katika ngome ya kusini mwa kundi hilo.Lakini vita bado havijaisha. RSF bado inashikilia karibu eneo lote la Darfur magharibi mwa Suda...

Wasira Ahutubia Mamia ya Wananchi Wilayani Kahama

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Stendi mjini Kahama akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025, uhai wa Chama na kusikiliza changamoto za wananchi mkoani Shinyanga. #kazinaututunasongambele

Ampaka Rangi Mbwa wake ili Aonekane kama Chui Kuwatisha Maafisa Wanaokusanya Marejesho ya Mkopo

Polisi katika Kaunti ya Nyamira nchini Kenya wanamsaka Kevin Onsombi mwanamume mwenye umri wa miaka 32 ambaye amempaka rangi mbwa wake ili aonekane kama Chui.  Hatua hiyo ya Onsombi ililenga kuwatisha maafisa wa kukusanya Marejesho ya mkopo baada ya kukosa kulipa mkopo wa Ksh 50,000.   Inasemekana Onsombi alikopa mkopo huo kutoka kwa Savings Sacco ili kulipia mahari ya mkewe ambapo alitoweka nyumbani kwake baada ya kubaini kugundulika kwa njama yake.

Ole wako unayebusu jamaa mwenye ndevu, bakteria zinakusubiri

DAKTARI na mtaalamu wa afya Dkt Myro Figura ametahadharisha dhidi ya kupiga busu wanaume wenye ndevu, akisema hatua hiyo inaweza kukusababishia maambukizi na muwasho kwa ngozi. Kutokana na hilo amewataka wanaume au wanawake wanaobusu wanaume wenye ndevu wajihadhari kwa sababu hiyo ni njia moja ya kujiletea maradhi. “Kupiga busu mwanamume mwenye ndevu kunaweza kukusababishia maradhi. Iwapo ndevu zenyewe si safi huwa ni hifadhi ya bakteria, na wakati wa kupiga busu vijidudu hivyo hatari vikitagusana na ngozi basi huleta upele wa malengelenge (impetigo kwa Kimombo),” asema Dkt Figura. Impetigo ni ugonjwa ambao unasambaa kwa urahisi. Huanza kwa ngozi kuwa na uvimbe kisha kutoa uchafu mwekundu. Mara nyingi uchafu huo ambao ni majimaji si rahisi kutambuliwa kwa watu wenye ngozi nyeusi au rangi kahawia. “Uvimbe ukipasuka huacha vidonda vidogo na husambaa sehemu mbalimbali za mwili. Kibaya zaidi ni kuwa aliyeathirika hujikuna sana na kuhisi uchungu kutokana na muwasho,” ameongeza mtaalamu huyo...

Biashara ya Kaboni yawapa Shavu Watanzania - Mhe. Chana

Na Happiness Shayo-Arusha Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema kuwa jamii zimeendelea kunufaika na biashara ya hewa ukaa kupitia miradi ya  Shirika la Uhifadhi wa mazingira la ‘The Nature Conservancy’ nchini Tanzania lililojikita katika kuhifadhi mifumo ya ikolojia , kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuongeza mapato kwa jamii. Ameyasema hayo katika hafla ya kuwashukuru wadau na kukuza mahusiano na washirika wa taasisi hiyo iliyofanyika leo Machi 27, 2025  jijini Arusha. “Tunashukuru sana kwa msaada wa The Nature Conservancy, hasa kwa kushirikiana na Carbon Tanzania, kuanzisha miradi ya kaboni katika maeneo muhimu kama vile Yaeda Chini, Makame Wildlife Management Area (WMA), Ntakata, na misitu ya Tongwe. Ushirikiano huu sio tu unasaidia kulinda mifumo muhimu ya ikolojia lakini pia hutoa fursa muhimu kwa jamii za wenyeji kufaidika kupitia mbinu bunifu za uhifadhi na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi” amesema Mhe.Chana....