Skip to main content

Posts

Showing posts from June 17, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Fanyeni Tafiti Zenye Tija Kwa Wananchi-Majaliwa

_▪️Ataka matokeo ya tafiti hizo yatumike badala ya kuyafungia_ _▪️Awataka wadau wa Sekta ya Afya kuongeza uwekezaji katika vifaa tiba na teknolojia mpya_   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa watafiti na wapangaji wa Sera kuwekeza katika tafiti zenye tija kwa wananchi.

 Amesema kufanya hivyo, kutawezesha kuwa na matokeo ambayo yatatumika kutengeneza sera na mipango ya utekelezaji yenye kuleta mabadiliko halisi katika jamii.

 Ametoa wito huo leo Jumatano (Juni 18, 2025) kwenye Kongamano la 13 la Kisayansi la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) lililofanyika chuoni hapo kampasi ya Mloganzila, jijini Dar es Salaam.
  
“Tunataka kuona matokeo ya tafiti hizi yanatumika, msiweke tafiti hizi kwenye makabati tu, matokeo haya yanapaswa kuleta tija katika sekta ya afya, Ni matarajio yangu kuwa kongamano hili litatumika kutoa mapendekezo yatakayoimarisha mifumo, sera, na ushirikiano baina ya sekta ya umma na binafsi ili kuhakikisha Watanzania wananufaik...

Waziri Mkuu akutana na wajumbe wa Misheni Maalum ya kutathmini maandalizi ya uchaguzi mkuu

_▪️Wazungumzia kuhusu maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025_ _▪️Timu hiyo yaridhishwa na mabadiliko na maboresho ya mifumo na Sera kuelekea uchaguzi mkuu_ _▪️Yafurahishwa na na namna Serikali ilivyojipanga kuhakikisha idadi kubwa ya ushiriki wa wanawake katika masuala ya siasa na uchaguzi_ _▪️Mheshimiwa Waziri Mkuu awahakikishia uchaguzi kuwa wa huru na haki_ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa jana Juni 17, 2025 amekutana na Misheni Maalum ya Umoja wa Afrika ya Kutathmini Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, 2025 (Pre-election assessment mission - PAM), Misheni hiyo iliongozwa na Dkt. Phumzile Mlambo-Ngcuka; Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Afrika Kusini akiambatana na Wajumbe wengine takribani 16. Lengo la Misheni hiyo ni kutathmini maandalizi ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na hali ya kisiasa ilikuhakikisha misingi ya demokrasia inafuatwa kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Afrika kuhusu Demokrasia Chaguzi na Utawala (African Charter on Democracy, Elections and G...

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (Reb) Aihakikishia Ushirikiano Kampuni ya Kuzalisha ba Kusambaza Umeme ya Matembwe Village Company ya Mkoani Njombe

📌Inazalisha umeme wa kilowati 550 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Kiyepa 📌Inahudumia kaya 2,463 katika vijiji 8. Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu ameihakikishia ushirikiano kampuni ya kuzalisha na kusambaza umeme ya Matembwe Village Company Limited ya Mkoani Njombe ili kuiwezesha kuongeza upatikanaji wa umeme na kuwafikia wananchi wengi zaidi waishio maeneo hayo.  Amethibitisha hayo alipofanya ziara katika mradi wa kuzalisha na kusambaza umeme wa Matembwe uliopo katika Tarafa ya Lupembe Wilaya ya Njombe Mkoani Njombe Juni 17, 2025. "Nimekagua mradi mzima kuanzia eneo la uzalishaji na nimetembelea baadhi ya wanufaika wa mradi ili kujionea uendeshaji wake, uwezo wake na namna ambavyo mradi huu unanufaisha wananchi katika kujiletea maendeleo," alifafanua Mhe. Balozi Kingu. Alisema ameridhishwa na namna ambavyo mradi huo wa Matembwe unavyofanya kazi na alisisitiza kuwa ipo haja ya kuongeza uzalishaji hasa ikizinga...

Simbachawene aipa tano Tume ya Madini

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa George Simbachawene ameipongeza Tume ya Madini kwa kazi kubwa na yenye matokeo chanya katika ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali na kuchochea maendeleo ya Sekta ya Madini nchini. Akizungumza alipotembelea banda la Tume ya Madini katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma, Mhe. Simbachawene amesema mafanikio hayo ni matokeo ya uongozi thabiti wa Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde. “Nawapongeza Tume ya Madini, na nampongeza sana Waziri wenu Mheshimiwa Anthony Mavunde kwa kusimamia kwa weledi ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali, kufufua migodi iliyokuwa imesimama, pamoja na kutoa ajira kwa vijana. Haya ni mafanikio ya kujivunia,” amesema Mhe. Simbachawene. Ameeleza kuwa Sekta ya Madini kwa sasa inachangia zaidi ya asilimia 10 ya Pato la Taifa, jambo linaloonesha mchango mkubwa wa sekta hiyo katika uchumi wa taifa, huku akitoa wito ...

Azania Bank Yang'ara Kongamano la Kitaifa la Wafugaji-simiyu

Benki ya Azania imetunukiwa tuzo maalum ya kutambua mchango wake katika maendeleo ya sekta ya mifugo nchini. Imetunukiwa tuzo hiyo katika Kongamano la Kitaifa la Wafugaji-Simiyu ambapo benki hiyo pia ilishiriki kongamano hilo. Kongamano hilo limehitimishwa na  Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi likiambatana pia na ufunguzi wa kampeni ya kitaifa ya chanjo na utambuzi wa Mifugo.

Majaliwa: Tunataka Tet iwe Kitovu Cha Ubora Katika Uandaaji wa Mitaala

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ili ifikie maono ya kuwa kitovu maridhawa cha ubora katika uandaaji, ukuzaji na ubunifu wa mitaala. Amesema kuwa TET ni moyo wa ukuaji wa elimu nchini na hasa kwa kuwa ndiyo inayojenga msingi wa elimu kuanzia Darasa la Awali mpaka Kidato cha Sita. Amesema hayo leo Jumanne (Juni 17, 2025) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) yanayofanyika katika viwanja vya Taasisi hiyo, Bamaga Jijini Dar es Salaam. “Serikali inatambua wakuza mitaala wanafanya kazi kwa bidii, weledi, maarifa na moyo wa kizalendo sana. Hivyo, niwahakikishia Watanzania wote kuwa, wakati wote Serikali, itaendelea kuimarisha utendaji wa TET ili kwenda sambamba na kazi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia.” Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iimarishe ushirikiano na...

CBE kuendesha kongamano la kuimarisha fursa za ajira

 Na Mwandishi Wetu CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimeandaa kongamano la kuimarisha fursa za ajira na maendeleo endelevu linalolenga kuwawezesha vijana kujiajiri. Hayo yalisemwa jana jijini Dar es salaam na Mkuu wa chuo hicho, Prof Edda Lwoga, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano hilo litakalofanyika Alhamisi chuoni hapo. Alisema mgeni rasmi katika Kongamano hilo anatarajiwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Selemani Jafo  akiambatana na viongozi mbalimbali wa kitaifa kutoka Serikalini na Sekta Binafsi.  “Lengo kuu la kongamano hili ni kuandaa jukwaa rasmi kwa wanafunzi wetu kuonyesha kwa vitendo yale waliyojifunza, na kuwapa nafasi ya kujifunza moja kwa moja kutoka kwa waajiri na wadau mbalimbali wa maendeleo,” alisema. “Hii ni sehemu ya jitihada za CBE katika kushiriki kikamilifu kutafuta suluhisho la changamoto ya ajira nchini na kwa  mwaka huu, tunatarajia kuwa na zaidi ya kampuni na taasisi 30 kutoka sekta mbalimbali zitakazoshiriki...

Kinyozi Aenda Jela Miaka 30 Kwa Kubaka Mwanafunzi

Mahakama ya Wilaya ya Kwimba imemhukumu Lindwa Clement Balthazari (30), mkazi wa kijiji cha Malya na kinyozi wa saluni ya kiume, kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 14 kutoka Shule ya Msingi Mwakulilima (jina linahifadhiwa kwa sababu za kisheria). Hukumu hiyo imesomwa leo, Juni 17, 2025, na Hakimu Mkazi Mfawidhi Ndeko Dastan Ndeko katika kesi ya jinai namba 31961/2024, baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi wa upande wa Jamhuri. Mshtakiwa alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza Desemba 4, 2024, na kusomewa shtaka la kubaka na Wakili wa Serikali Juma Kiparo, ambapo alikana kutenda kosa hilo. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Lindwa alitenda kosa hilo nyumbani kwake kwa nyakati tofauti mwezi Oktoba 2024, akitumia nafasi ya kumhudumia mtoto huyo kwenye saluni yake kabla ya kumrubuni na kumbaka, kinyume na vifungu vya sheria 130(1), 130(2)(e), na 131(1) vya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 (marejeo ya 20...