Skip to main content

Posts

Showing posts from October 21, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mavunde azindua magari 25 ya tume ya madini

_Ni sehemu ya magari 89 na pikipiki 140 zinazotarajiwa kununuliwa_ _Lengo kuboresha Sekta ya Madini_ _Aagiza Magari kufungwa GPS_ _Ampongeza  Rais Samia kwa kuiongezea bajeti Wizara ya Madini_  *DODOMA* Ikiwa ni mkakati wa kuimarisha usimamizi katika Sekta ya Madini hasa kwenye ukusanyaji wa maduhuli, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amezindua magari mapya 25 kwa ajili ya kusambazwa kwenye Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa sambamba na kukabidhi magari hayo kwa Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa waliohudhuria uzinduzi huo.  Uzinduzi huo umehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo na watendaji wengine kutoka Wizara ya Madini na Taasisi zake. Akizungumza kwenye  uzinduzi huo, Mhe. Waziri Mavunde amesema kuwa Wizara imepanga kununua magari 89 na pikipiki 140 kama sehemu ya uboreshaji wa  usimamizi wa Sekta ya Madin...

Waziri mkuu atoa agizo kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ruangwa

*Ni madarasa ya kidato cha tano na sita katika sekondari ya Mandawa WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Frank Chonya ahakikishe mkandarasi anayejenga mabweni, madarasa na vyoo katika shule ya sekondari Mandawa awe ameanza kazi ifikapo Oktoba 24, mwaka huu. Akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule hiyo pamoja na viongozi wa Wilaya hiyo, leo (Jumatatu, Oktoba 21, 2024) mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu hiyo, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali imeamua kuipandisha hadhi shule hiyo kwa kuamua kuifanya iwe na madarasa ya kidato cha tano na sita.  Waziri Mkuu Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, yupo wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi ya siku nne, amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa sh. milioni 545 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni matatu, madarasa sita na matundu ya vyoo 12 katika shule hiyo, iliyopo kata ya Mandawa, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi. Waziri Mkuu amekemea tabia ya watumishi kup...

Mbunge Tulia afanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo mbeya mjini

Rais wa umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt.Tulia Ackson, leo tarehe 21 Oktoba, 2024 amefanya ziara ya kukagua mradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo. Mh Tulia amekagua miradi hiyo inayotekelezwa na Serikali kuu kwa uboreshaji wa shule ya sekondari Iganzo iliyopo Jijini Mbeya ambapo ilitengewa kiasi cha shilingi Milioni 174 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa pamoja na matundu ya vyoo. Aidha mbunge huyo wa jimbo la Mbeya amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada za kuendelea kuboresha sekta ya elimu nchini ikiwemo katika jimbo hilo. Dkt Tulia amesisitiza kuwa Wananchi wanapaswa kuendelea kumuunga mkono Rais Samia kwa kulinda miundombinu hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule kwakuwa elimu sasa ni bure.  

CP.Wakulyamba awapiga msasa askari wa Ju, Simiyu na Mara

Na. Sixmund Begashe - Mara Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kutekeleza Maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan yaliyotoka na Maoni ya Tume ya Haki Jinai ya kuboresha Jeshi la Uhifadhi kwa kutoa Mafunzo ili liweze kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Misingi ya Sheria na Haki za Binadamu. Akitoa mafunzo hayo kwa Askari wa Jeshi hilo kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Shirika la  Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wa Mikoa ya Simiyu na Mara, Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii anayeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi (CP), Benedict Wakulyamba, amewaeleza Askari hao kwamba Taifa lina imani kubwa nao katika ulinzi na usimamizi wa Maliasili nchini, hivyo ni vyema wakaitunza tunu hiyo ambayo imetokana na imani ya wananchi kwao.  Aidha, CP Wakulyamba amewataka Askari hao kujiepusha na matendo maovu kazini, hususan rushwa na...