Skip to main content

Posts

Showing posts from August 30, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

RAIS FEMATA JOHN BINA KUFANYA ZIARA MKOANI MWANZA

  🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥 *TANGAZO MAALUM* *MHE. JOHN WAMBURA BINA RAIS WA FEMATA NA MWENYEKITI WA KAMATI TENDAJI YA FEMATA*. *LEO TAREHE 31/8/2024 ATAKUWA NA ZIARA MKOANI MWANZA KUKUTANA NA VIONGOZI WA REMAs YA MWAREMA NA WACHIMBAJI WA MKOA WA MWANZA KIKAO HICHO CHA VIONGOZI WAANDAMIZI WA MWAREMA NA WACHIMBAJI KITAFANYIKA WILAYA YA MISUNGWI* *RAIS ATAAMBATANA NA NDUGU, JEREMIAH KITUYO MWENYEKITI WA CHAMMATA (CHAMA CHA MA-BROKERS)* *BAADAE LEO RAIS WA FEMATA ATAKUTANA NA WACHIMBAJI WA MKOA WA SHINYANGA NA BAADAE VIONGOZI WAANDAMIZI WA REMAs YA SHINYANGA - SHIREMA*. *KESHO TAREHE 1/9/2024 RAIS WA FEMATA ATAKUTANA NA WACHIMBAJI WA MKOA WA TABORA REMAs YA TABOREMA, TAREHE 2/9/2024 ATAFIKA MKOA WA SINGIDA REMAs YA SIREMA*   *RAIS WA FEMATA ANAWATANGAZIA WENYEVITI,  VIONGOZI WAANDAMIZI WA REMAs NA WACHIMBAJI WA MADINI MIKOA YA JIRANI KUAMBATANA NAE KWENYE ZIARA HIYO*. *RATIBA YA ZIARA MAALUM YA RAIS WA FEMATA AWAMU BAADA YA KUFIKA SINGIDA RATIBA ITAKAYO FUAT...

Gonjwa la Kutisha Latua Nchi Jirani

Kuripotiwa kwa Mgonjwa wa tatu mwenye maradhi ya Homa ya Nyani Kenya ni hatari kwa nchi Tanzania kama tahadhali haitachukuliwa. Wizara ya Afya imethibitisha kuwepo mgonjwa wa tatu wa Homa ya Nyani {Mpox} nchini, huku mgonjwa wa kike mwenye umri wa miaka 30 jijini Nairobi akipimwa na kukutwa na maradhi hayo . Mkurugenzi Mkuu wa Afya Dk.Patrick Amoth amesema kuwa mgonjwa, huyo ambaye ana historia ya kusafiri kuelekea Uganda hivi karibuni , kwa sasa yuko katika hali nzuri na anapatiwa matibabu katika sehemu aliyotengwa katika mji mkuu. Kisa hiki cha hivi punde kinafanya jumla ya watu waliothibitishwa kuwa na Mpox nchini Kenya kufikia watatu, baada ya wagonjwa wengine kugunduliwa katika kaunti za Taita Taveta na Busia. Hadi sasa, Wizara imepima jumla ya sampuli 89 za Mpox, huku 79 zikiwa hazina huku saba zikiwa zinaendelea kufanyiwa uchunguzi. Dkt. Amoth amesisitiza kuwa Wizara imekuwa ikifuatilia kwa karibu hali hiyo na imeongeza kwamba juhudi za kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo zinaendel...

Waziri Mkuu Atoa Wito Kwa Nchi Wanachama Afrika Mashariki Kuondoa Vikwazo Kwenye Huduma za Afya

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa watoa huduma za afya wa nchi wanachama wa kanda ya Afrika Mashariki kuondoa vikwazo vinavyozuia wagonjwa wanaotafuta matibabu ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki. "Hatua hii ni kwa manufaa ya wananchi wetu na kwa uchumi wa kikanda na ukuaji wa utalii tiba." Ametoa wito huo leo (Ijumaa Agosti 30, 2024 ) alipokuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa 12 wa Shirikisho la Watoa Huduma za Afya Afrika Mashariki uliofanyika katika Kituo  cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Njerere (JNICC). Dar es Salaam Amesema nchi wanachama ikiwemo Tanzania zimejitahidi kuwekeza katika sekta ya afya na kupunguza gharama za kupeleka wagonjwa nje ya Kanda kwa matibabu.  "Kwa sasa ni wagonjwa wachache sana wanaosafiri nje ya nchi zetu kwa ajili ya matibabu, kwani karibu magonjwa yote makubwa sasa yanaweza kutibiwa ndani ya Afrika Mashariki. Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa wawekezaji wa Sekta ya Afya kuwekeza nchini Tanzania kwa k...