*●Yalenga kuchangia trilioni 1.4/- za maduhuli* *●Makusanyo yafikia Trilioni 1 na Milioni 156* *●Jumla ya tani 23.8 za dhahabu zakusaywa ndani ya miezi 18* *●Ni Juhudi za Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan* *Dodoma* Bunge la Jamhuru ya Muungano wa Tanzania, limeridhia na kupitisha bajeti ya Wizara ya Madini ya shilingi bilioni 174.9 kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 ili kuiwezesha Wizara ya Madini kufanikisha ukusanyaji wa maduhuli ya shilingi trilioni 1.4. Akiwasilisha Bungeni makadirio ya Mapato na Matumizi leo Aprili 27, 2026, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amesema fedha hizo zitawezesha kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara pamoja na taasisi zilizo chini yake, huku zikilenga kuendeleza kasi ya ukuaji wa sekta ya madini kwa kufanya tafiti za jiosayansi nchini. Akifafanua mgawanyo wa Bajeti hiyo, Waziri Mavunde amesema kiasi cha shilingi bilioni 71.5 sawa na asilimia 40.9 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo, wakati shilingi bilioni 103.5 sawa na asilimia 59.1 zikiwa...
Marato tv - Sauti ya Jamii