Skip to main content

Posts

Showing posts from December 13, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kenya Yatangaza Matokeo ya Wanafunzi wanaotumia Mtaala Mpya wa Elimu

MATOKEO  ya wanafunzi wa Gredi ya 9, KJSEA ndiyo yaliyokuwa ya kwanza  kutolewa rasmi kupitia Mtaala wa Utendaji na Umilisi (CBE), tukio linaloonyesha jinsi mfumo wa elimu unavyoendelea kubadilika nchini. Zamani kupitia mfumo wa 8-4-4 wanafunzi walitilia mkazo tu alama walizozipata ila mfumo huu unajikita sana katika Vipaji na uelewa mpana wa masomo anayoyapenda mwanafunzi. Chini ya mfumo wa CBE, mwanafunzi anatathminiwa kuanzia Gredi ya Kwanza hadi afanye KJSEA. Chini ya uliokuwa mfumo wa 8-4-4, wanafunzi walikuwa wakifanya Mitihani ya Kumaliza Elimu ya Msingi(KCPE) ambayo alama za mtahiniwa ndizo zilikuwa zikitathminiwa katika kila somo, alama ya jumla ikiwa 500. Hata hivyo, KJSEA inachangia tu asilimia 60 ya alama ya mtahiniwa wa Gredi ya 9.   Asilimia 40 zilizosalia nazo hugawanywa ambapo asilimia 20 hutoka kwa mtihani wa Gredi ya 6 KPSEA, kisha asilimia 20 nyingine huchangiwa na alivyofanya mwanafunzi katika masomo ya vitendo shuleni. “Mfumo huu hautegemei alama kati...

Rais Samia Aongoza Viongozi,Wabunge na Wananchi Kuaga Mwili wa Jenista Mhagama Jijini Dodoma

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Joakim Mhagama, katika ibada iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kiwanja cha Ndege, Jimbo Kuu la Dodoma, tarehe 13 Desemba 2025.

Buriani Jenista Mhagama

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) John Mongella, wakitoa heshima za mwisho kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, marehemu Mhe. Jenista Joakim Mhagama, mara baada ya ibada, leo Jumamosi, tarehe 13 Desemba 2025.   Shughuli ya utoaji wa heshima za mwisho kuaga mwili wa Mhe. Jenista Mhagama iliyofanyika katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska, Kiwanja cha Ndege, jijini Dodoma, iliongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Balozi Dkt. Migiro Ibadani Kumuaga Jenista Mhagama

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM, amejumuika na waombolezaji wengine kushiriki ibada ya kumuaga aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, marehemu Jenista Joakimu Mhagama, inayofanyika katika Kanisa Katoliki Kiwanja cha Ndege, jijini Dodoma.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anawaongoza waombolezaji katika shughuli hiyo ya kumuaga marehemu Jenista Mhagama, kanisani hapo.