"Tuendelee Kuiunga Mkono Serikali Yetu Kwa sababu ni Serikali Sikivu na inatatua Kero za Wananchi", Mtendaji Mkuu Temesa
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Lazaro Kilahala amewaomba wananchi wa Kanda ya Ziwa na maeneo mengine ya Nchi kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita inayooongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwakuwa Serikali hiyo ni Serikali sikivu inayowajali wananchi wake kwa kutatua kero zinazowakabili hasa za usafiri wa maji ambao ndio umekuwa tegemeo kubwa kwa wakazi wanaoishi visiwani na pembezoni mwa Ziwa Victoria. Kilahala ameyasema hayo leo Tarehe 15 Desemba, 2024 wakati alipofanya ziara ya kikazi katika eneo la Buyagu Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza, kukagua maendeleo ya ujenzi wa maegesho mapya ya kivuko cha Buyagu- Mbalika yanayoendelea kujengwa katika eneo hilo. Kilahala amesema, katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inafanya kazi ya ujenzi wa vivuko vipya vitano huku vitatu kati ya hivyo vikiwa vinatarajiwa kupelekwa katika maeneo ambayo hayakuwahi kabisa kuwa na vivuko hapo awali na viwili ...