Skip to main content

Posts

Showing posts from May 28, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

SERIKALI YAHIMIZA WANANCHI KUMILIKI ARDHI KISHERIA KUEPUSHA MIGOGORO

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewataka wananchi nchini kuhakikisha wanamiliki ardhi zao kisheria, ikieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kupunguza migogoro ya ardhi na kuongeza fursa za maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Leonard Akwilapo amesema umiliki rasmi wa ardhi unasaidia kulinda haki za wananchi, kuongeza thamani ya maeneo yao pamoja na kuweka mazingira salama ya uwekezaji na uzalishaji. Akizungumza leo Mei 28,2026 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Dkt. Akwilapo amesema serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kurasimisha umiliki wa ardhi ili wananchi wengi zaidi waweze kupata hati na nyaraka halali za maeneo yao. Amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026 wizara ilijiwekea lengo la kuandaa na kusajili hatimiliki 500,000, kutoa hati za hakimiliki ya kimila 520,000, hati za sehemu ya jengo 1,000 pamoja na vyeti vya ardhi ya vijiji 100 na kushughulik...

SERIKALI YAJA NA SULUHISHO LA KUDUMU MIGOGORO YA ARDHI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Leonard Akwilapo amesema serikali imeanza rasmi utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Kudhibiti Migogoro ya Ardhi nchini, hatua inayolenga kumaliza changamoto ya migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikiathiri wananchi katika maeneo mbalimbali ya Tanzania. Akizungumza leo Mei 28 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti ya wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Dkt. Leonard  Akwilapo amesema mkakati huo umeandaliwa kwa lengo la kupata suluhisho la kudumu na kuhakikisha matumizi ya ardhi yanafanyika kwa utulivu, haki na maendeleo endelevu. Amesema hatua hiyo inatekelezwa kufuatia maelekezo ya Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba aliyeitaka Wizara ya Ardhi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuandaa mpango maalumu wa kushughulikia chanzo cha migogoro hiyo nchini. Kwa mujibu wa Dkt. Akwilapo, mkakati huo umehusisha makundi yote muhimu yanayotumia ardhi ikiwemo wakulima, wafugaji, wawek...

TANZANIA YAJIPANGA KUWA MZALISHAJI MKUBWA WA MADINI KINYWE(GRAPHITE)DUNIANI

■ Sera imara na usimamizi thabiti wa Mhe. Rais Samia kuchochea uzalishaji ■ Serikali yasaini mkataba wa ubia wa uchimbaji wa madini kinywe na Kampuni ya Lindi Jumbo ■ Tani 40,000 kuzalishwa kwa mwaka, kwa zaidi ya miaka 24. ▪️Waziri Mavunde awataka wamiliki wa Leseni 28 za uchimbaji wa madini kinywe kuanza uzalishaji kabla hawajafutiwa Leseni *Ruangwa, Lindi* Waziri wa Madini, *Mh. Anthony Mavunde (Mb)* amesema kwamba Tanzania inajiapanga kuwa mmoja ya wazalishaji wakubwa Duniani wa madini kinywe(𝙂𝙧𝙖𝙥𝙝𝙞𝙩𝙚) kupitia Kampuni 30 zinazomiliki Leseni za kati na kubwa za uchimbaji wa madini hayo na hivyo kutoa ushindani wa kiuzalishaji kwa nchi ya China ambayo ndio inaongoza kwa uzalishaji wa madini hayo duniani kwa kuzalisha tani milioni 1.2 kwa mwaka.  Mh. Mavunde ameyasema hayo leo tarehe 28 Mei, 2026 Wilayani Ruangwa, Lindi aliposhiriki katika hafla ya utiaji saini wa mikataba wa ubia baina ya Serikali na Kampuni ya Lindi Jumbo Limited kwa ajili ya mradi mkubwa wa uchimbaji ma...

RAIS SAMIA AFUNGA MAFUNZO YA MAAFISA WA POLISI NCHINI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhitimisha Mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Jeshi la Polisi, tarehe 28 Mei, 2026.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhitimisha Mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Jeshi la Polisi, tarehe 28 Mei, 2026.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhitimisha Mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Jeshi la Polisi, tarehe 28 Mei, 2026. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitoa vyeti kw...