Skip to main content

Posts

Showing posts from September 3, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WAHITIMU VYUO VIKUU SASA WAKIMBILIA VETA

 Dhana kwamba elimu ya ufundi stadi ni kwa watu waliokosa fursa za elimu ya juu inaendelea kupotea, huku wahitimu wenye vyeti, stashahada, shahada na hata shahada za uzamili wakijitokeza kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi ili kuongeza ujuzi na kukidhi mahitaji ya soko la ajira. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), CPA Anthony Kasore, amesema katika kipindi cha mwaka 2022/2023 hadi 2025/2026, jumla ya waombaji 794 wa mafunzo ya ufundi stadi walikuwa tayari na elimu za juu katika taaluma mbalimbali. Amesema kati yao, 522 walikuwa na vyeti vya taaluma nyingine, 120 walikuwa na stashahada, 151 walikuwa na shahada na mmoja alikuwa na shahada ya uzamili. Kasore ameyasema hayo leo, Septemba 4, 2026, jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu nafasi ya VETA katika kujenga Taifa lenye wananchi wenye ujuzi. Amesema ongezeko hilo linaonesha mabadiliko makubwa katika mtazamo wa jamii kuhusu elimu ya ufundi stadi, ambayo kwa muda mrefu ime...

PBPA YADHAMILIA KULINDA AFYA ZA MAMA LISHE NA KUTUNZA MAZINGIRA NCHINI.

 Na Mwandishi wetu Jovina Massano Ili kulinda  afya za baba na mama lishe pamoja na kuhifadhi mazingira hapa nchini  Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) yahamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia Kurasini. Hamasa hiyo ya matumizi ya nishati safi ya kupikia pamoja na kampeni za uhifadhi wa mazingira imetolewa na Mkurugenzi  wa Uendeshaji wa PBPA,Mhandisi Bruno Tarimo. Mhandisi Tarimo amewahimiza mama na baba lishe kuachana na matumizi ya kuni na mkaa wa kawaida na kuhamia katika nishati safi ya kupikia ili kulinda afya zao sambamba na kuhifadhi mazingira lengo ikiwa  kuongeza ufanisi wa biashara zao. Septemba 3, 2026,PBPA imetoa mafunzo ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa mama na baba lishe wa Kikundi cha Jitihada, yaliyofanyika Kurasini jijini Dar es Salaam na kuwakabidhi mama na baba lishe 70 jumla ya tani 1.7 za mkaa mbadala. Mhandisi Tarimo ambae amemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa PBPA amesema mafunzo hayo ni sehemu ya ushiriki wa Wakala...

RWANDA YAANDAA MKUTANO WA MWAKA WA BARAZA LA MAWAZIRI NA MKUTANO WA MAAFISA WAANDAMIZI WA ESAAMLG

Na Benny Mwaipaja, Kigali-Rwanda Rwanda imekuwa nchi Mwenyeji wa Mikutano ya Mwaka ya Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Kupambana na Utakasishaji Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi (ESAAMLG), inayofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Kigali, kuanzia Agosti 31 hadi Septemba 5, 2026. Mikutano hiyo inajumuisha Mkutano wa 52 wa Maafisa Waandamizi na Mkutano wa 26 wa Baraza la Mawaziri, pamoja na Mkutano wa 9 wa Majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi. Mikutano hii huwakutanisha viongozi wa Serikali katika ngazi ya Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Fedha, Katiba na Sheria, Mambo ya Ndani na maafisa waandamizi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, ambapo kwa upande wa Tanzania utawashirikisha Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Juma Homera na Katibu Mkuu Wizara hiyo, Dkt. Seif Abdallah Shekalage. Wengine ni Mkurugenzi wa Mashtaka DPP Sylvester Mwakitalu, pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, Bw...

NSEKELA AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUENDELEZA FALSAFA YA MWENGE WA UHURU

 Na Angela Sebastian ;Kyerwa Mbunge wa Jimbo la Kyerwa, Khalid Nsekela, amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuenzi nyayo za waasisi wa Taifa letu kwa kuendeleza falsafa ya Mwenge wa Uhuru, unaoendelea kuwa chachu ya kuimarisha amani, uzalendo na upendo miongoni mwa Watanzania.  Amesema misingi hiyo imeendelea kuwa tunu muhimu inayolifanya Taifa kujivunia umoja na mshikamano wake. Nsekela alitoa pongezi hizo mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Wazo Michael Mwang’onda, baada ya kupata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa Jimbo la Kyerwa wakati wa uzinduzi wa jengo la Wodi ya Wazazi katika Zahanati ya Kata ya Rukulaijo mbapo, jengo hilo limejengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kwa kutumia mapato ya ndani, likiwa na thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 386.1. Kwa mujibu wa Nsekela, Serikali inayoongozwa na Rais Samia imeendelea kupeleka fedha nyingi katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi na kuc...

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA AZINDUA JENGO LA RAMANI LA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 03 Septemba, 2026, amezindua rasmi Jengo la Ramani la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lililopo katika Mji wa Serikali, Mtumba, Jijini Dodoma. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo hilo ambalo ni sehemu ya miundombinu ya kimkakati ya Jeshi, Dkt. Nyansaho amelipongeza JWTZ kwa kukamilisha mradi huo na kupata jengo la kisasa lililowekewa vifaa na teknolojia za kisasa zitakazowezesha utoaji wa huduma kwa ufanisi na weledi zaidi. Waziri Nyansaho amesema kukamilika kwa mradi huo ni kielelezo cha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuendelea kuliwezesha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kulinda uhuru, mamlaka na usalama wa nchi.  “Kukamilika kwa mradi huu wa kimkakati ni alama ya dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuendelea kuliwezesha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kutimiza majukumu yake ya ulinzi na usal...

DKT. MWIGULU AONGOZA MKUTANO WA KAZI WA MAWAZIRI

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Septemba 03, 2026 ameongoza Mkutano wa kazi wa Mawaziri, kwenye ukumbi wa mikutano wa Hazina jijini Dodoma.

MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA KIBAHA AWATAKA WAZAZI KUIMARISHA NA KUBORESHA ELIMU KWA KUSHIRIKIANA NA WALIMU

 Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dr Nicas Mawazo amewataka wazazi wa Shule zilizopo Manispaa ya Kibaha kuiga  jitihada zinazofanywa na Shule zingine katika kuimarisha na kuboresha elimu kwenye Shule zao kwa kushirikiana na walimu. Hayo ameyasema wakati wa kikao na Kamati ya Shule ya Sekondari ya Mwambisi, iliyofika katika Ofisi ya Mstahiki Meya kwa ajili ya kujadiliana na masuala mbalimbali. Akizungumza baada ya Kamati hiyo kuwasilisha mapendekezo yao, Mstahiki Meya Dr Nicas ameipongeza Kamati hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha wanafunzi wa Shule yaSekondari Mwambisi wanaendelea kufanya vizuri kwenye mitihani yao. "Nawapongeza sana Kamati ya Shule kwa jitihada kubwa mnazofanya , Shule zingine wangekuwa wanafuata utaratibu huu ina maana tungekuwa tunafanya vizuri zaidi  na zipo baadhi ya Shule zinafanya hivyo na matokeo yao yanakuwa ni mazuri," amesema Dr Nicas. Ameongeza kuwa,, Ofisi ya Mstahiki Meya itaongezea hela ya ununuzi wa mashine ya...