Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi amewashukuru Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) pamoja na makundi mbalimbali ikiwemo watu wenye mahitaji maalum na wajane kwa kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono na kumchangia Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Zanzibar 2025, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Mama Mariam Mwinyi amesema hayo katika hafla maalum ya kumuunga mkono Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi iliyofanyika katika Ukumbi wa Madinat Al Bahr leo, tarehe 29 Agosti 2025. Aidha, Mama Mariam Mwinyi amewapongeza Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa kuandaa tukio hilo la kumuunga mkono Dkt. Mwinyi kwa kumchangia Shilingi Milioni 35 kwa ajili ya kuchukua fomu kesho katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC). Vilevile, Mama Mariam Mwinyi amewahimiza wananchi wote kuendelea kudumisha amani na utulivu kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba. Naye, Makamu Mwenyekiti wa UWT Zan...
Marato tv - Sauti ya Jamii