Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kulinda uhuru wa kuabudu na kuimarisha ushirikiano na taasisi za dini kwa kutambua mchango mkubwa unaotolewa na taasisi hizo katika kujenga maadili, amani, mshikamano na maendeleo ya Taifa. Dkt. Mwigulu amesema hayo leo, Jumapili Juni 14, 2026, aliposhiriki Ibada katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Kiomboi Christian Centre, mjini Kiomboi, Wilaya ya Iramba mkoani Singida. Ibada hiyo iliongozwa na Askofu wa Jimbo la Singida Kaskazini, Dkt. Danford Obadia pamoja na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Yona Suleman Essya. Akizungumza na waumini hao, Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua nafasi muhimu ya taasisi za dini katika malezi ya jamii na kwamba itaendelea kuweka mazingira rafiki yatakayowezesha taasisi hizo kutekeleza majukumu yake kwa uhuru na ufanisi. “Sisi wote tutaendelea kulinda mazingira bora ya kuendesha ibada. Serikali itaendelea kutambua na kuamini kazi inayofanywa na taasisi za dini katika kuje...
Marato tv - Sauti ya Jamii