Skip to main content

Posts

Showing posts from November 15, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali yawapa Uhakika Wajasiriamali Wanawake

SERIKALI imewahakikishia Wajasiriamali Wanawake na Vijana kuwa itaendelea kuwawezesha kwa kuwapatia maarifa, masoko, fursa za kijamii na kiuchumi ili waweze kupiga hatua katika kujenga uchumi wa familia na jamii kwa ujumla.  Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia kazi,ajira na watu wenye Ulemavu Mh Ridhwani Jakaya Mrisho Kikwete,ametoa msimamo huo wa Serikali jijini Dar es Salaam jana Novemba 15 mwaka 2024 wakati akizindua jukwaa la soko la bidhaa zinazozalishwa wajasiliamali wazawa. Kupitia jukwaa hilo la Wajasiliamali wazawa Wasichana na vijana wa Panda linaloratibiwa na taasisi ya Her Initiatives chini ya uongozi wa bi Lydia Thomas,waziri huyo wa nchi mwenye dhamana ya kazi na vijana amesema serikali inaamini ukisaidia makundi haya muhimu itakuwa umesaidia Jamii.  Taasisi hiyo inajulikana kutokana na juhudi kubwa inazofanya duniani kwa kuwanyanyua vijana na Wanawake na kuwezesha wameshinda zawadi za Utambuzi maeneo mengi ikiwemo ile ya Global Citizen inayotole...

Wakinamama Wajasiriamali wa Dodoma Wamshukuru Rais Samia Kwa Fursa za Kiuchumi

▪️Wajipanga kujiimarisha kiuchumi kwa fursa za kiuchumi kwa fursa zilizopo Dodoma. ▪️Wajipanga kujenga Maduka ya kibiashara na eneo maalum la uwekezaji ▪️Wampa tuzo Mbunge Mavunde kwa mchango wake kwa wakinamama Dodoma ▪️Mbunge Mavunde kukabidhi kiwanda cha kukamua mafuta kwa wakinamama 📍𝐃𝐎𝐃𝐎𝐌𝐀 Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoani Dodoma kwa kauli moja limempongeza *Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan* kwa kuweza mazingira mazuri ya ukuaji wa kiuchumi wa wanawake pamoja na kuongeza fursa za kiuchumi mkoani Dodoma ambapo wananwake ni kundi kubwa wanufaika. Pongezi hizo zimetolewa jana na Mwenyekiti wa Jukwaa Bi. Maryrhobi Mabhaya  wakati wa Kongamano la wakina Mama wa Dodoma kumpongeza Mh. Rais Samia kwa namna ambavyo serikali ya awamu ya sita ilivyochochea maendeleo katika Mkoa wa Dodoma na hivyo kutengeneza fursa kubwa ya kiuchumi. “Dodoma ya leo sio kama ya zamani,maendeleo ya Dodoma ya sasa huwezi kuyasema bila kumtaja Rais Samia. Hivi sasa kuna fursa lukuki za kiuchum...

Fahamu Taratibu za Kupata Mikopo wa Kununua Vifaa Vya Solar Kwa Ajili ya Miradi yako Toka NMB Bank Tawi la Musoma

Na Emmanuel Chibasa-Musoma Changamoto ya ukosefu wa fedha kwa wakulima wadogo katika wilaya ya Musoma Mkoani Mara, inatajwa kuwa sababu kubwa inayoplelekea kushindwa kumudu gharama ya kununua vifaa vya nishati ya umeme jua, kwa ajili ya shughuli za kilimo cha umwagiliaji na kusababisha chakula kinachozalishwa  kupotea baada ya mavuno kutokana na uhaba wa uhifadhi baridi na miundombinu duni ya usafirishaji, pamoja na ongezeko la joto linalochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa. Pia kukosekana Miradi inayotekelezwa na Kampuni za nishati ya jua katika wilaya ya Musoma kunachangia wakulima wadogo kuendelea kupoteza mazao ya Kilimo na Uvuvi baada ya mavuno kutoka na kukosa miradi inayoweza kuwasaidia  teknolojia  na vyumba vya uhifadhi wa baridi vinavyoendeshwa kwa nishati ya jua bila kuhitaji kuunganishwa kwenye gridi ya taifa, ili kulinda chakula baada ya mavuno hali inayochangia kuathiri mapato ya wakulima pamoja na uhaba wa chakula. Inaelezwa kuwa, endapo  pampu zina...

Mtendaji Mkuu Tarura Mhandisi Victor Seif amwagiza Mkandarasi Kukamilisha Ujenzi wa Nguzo Mbili za Daraja Zilizobakia Kabla ya Msimu wa Mvua Kuanza

*Rufiji, Pwani.* Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) amemtaka Mkandarasi MAC Contractor Ltd anayejenga Daraja la Mohoro lililopo Wilayani Rufiji  Mkoa wa Pwani kukamilisha ujenzi wa nguzo mbili zilizobakia  kwenye ujenzi wa daraja hilo kwa kuwa mvua za msimu zinakaribia.  Alisema, ujenzi wa nguzo hizo utapelekea utekelezaji wa Mradi kwa hatua inayofuata kutokukwama wakati wa Mvua. Agizo hilo amelitoa tarehe 15.11.2024 aliporudi tena kwa mara ya pili  ikiwa ni ahadi aliyoitoa wiki iliyopita alipoutembelea mradi huo. Mhandisi Seff, amemtaka Mhandisi  Mshauri  wa TREECO Mhandisi Emmanuel Mahimbo kumsimamia Mkandarasi  MAC ili amalize kazi kwa Wakati. Mhandisi Mahimbo alieleza kuwa tatizo kubwa la Mkandarasi ni kutokua na malighafi za Ujenzi kama Cement hivyo kupelekea baadhi ya kazi kusuasua. Vile vile Mhandisi Seff  alitembelea  kwa mara ya pili Mradi wa  Ujenzi wa Barabara ya Utete-Kingupira (32km) inayojeng...

Mbunge Ghati ataja Mafanikio Makubwa ya Rais Samia

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mara mh Ghati Chomete,amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu ambayo pia yamewezesha watoto wa masikini wakiwemo watoto wa kike kupata elimu hiyo bila vikwazo. Mh Chomete ameyasema hayo leo Novemba 15-2024  wilayani Tarime wakati akishiriki kampeni ya "Tunasimama na Mama Samia Binti Abaki Shuleni" kwa kuwagawia Taulo za kike kwa lengo la kulinda hedhi salama. Amesema  katika mageuzi hayo makubwa ambayo yamefanywa na Rais Samia ni pamoja na ujenzi wa shule mpya zikiwemo za watoto wa kike,miundombinu ya elimu,kutatua changamoto zikiwemo za upandishwaji wa madaraja kwa walimu hatua ambayo imewezesha kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu mkoa wa Mara na taifa kwa ujumla. Kwa sababu hiyo amewata wanafunzi hao wa shule ya Sekondari  ya Tarime Bomani na Iganana kusoma kwa bidii  katika kuunga mkono jitihada hizo kubwa za Rais Samia na kwamba Serikali itaend...

Rais Samia aumizwa na Mauaji ya Katibu wa Ccm Wilaya

_Simanzi yatanda mazishi yake_ _Nchimbi: matukio ya kutia hofu na shaka, hayakubaliki_ MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ‘ameumizwa na kusikitishwa sana’ na tukio la kuuwawa kwa Ndugu Christina Alex Kibiki, aliyekuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi alipokuwa akitoa salaam za rambirambi na pole za Mhe. Dkt. Samia wakati wa mazishi ya Ndugu Kibiki, yaliyofanyika katika eneo la Banavanu, Tosamaganga, Iringa vijijini, leo Ijumaa, tarehe 15 Novemba 2024. Ndugu Kibiki alipoteza uhai usiku wa tarehe 12 Novemba 2024, baada ya kuvamiwa na kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake usiku huo, na watu wambao hawajajulikana hadi sasa, huku vyombo vya dola, kupitia jeshi la polisi, vikitangaza kuanza kuwasaka kwa ajili ya hatua za kisheria. “Nianze kwa kutoa salaam za pole na rambirambi za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa ...

Mradi wa Umeme Rusumo Wafikia asilimia 99.9

*📌Mawaziri wa Nishati Tanzania, Rwanda na Burundi Wajadili Uzinduzi wa Mradi* *📌Dkt. Biteko Ahimiza Utunzaji wa Mradi, Mazingira* *📌Asema RUSUMO inakuza na kuchochea Uchumi* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Baraza la Mawaziri wa Nishati wanaosimamia Mradi wa Kufua Umeme wa Rusumo ambao wanatoka nchi za Tanzania, Burundi na Rwanda wamekutana na kujadiliana kuhusu mradi ambao utazinduliwa karibuni  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mwenyekiti, Dkt. Doto Biteko amesema pamoja na mambo mengine wamekubaliana mawaziri warejeshe makubaliano yaliyofikiwa na Kikao kwa marais ili waridhie uzinduzi rasmi. “ Mradi umefikia asilimia  99.9 na vimebaki vitu vichache ili kuukamikisha, katika kikao cha Baraza la Mawaziri kuhusu mradi  tumekubaliana kuwasilisha maombi yetu kwa wakuu wa nchi ili watakapota nafasi mwakani waweze kuzindua mradi huu,” amesema Dkt. Biteko. Amesema kuwa sasa mahitaji ya umeme Tanzania ni Megawati 1,800 na tuna uwezo wa k...