Skip to main content

Posts

Showing posts from July 12, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Dkt Samia Aipongeza Tanesco

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr Samia Suluhu Hassan, amepongeza kazi kubwa inayofanywa na shirika la usambazaji wa nishati ya umeme nchini TANESCO, huku akisema Serikali imetoa kiasi zaidi shilingi bilioni mia moja kwa ajili ya ujenzi wa njia ya kusafirishia umeme wa gridi kwenda mkoa wa Katavi, pamoja na shilingi bilioni 48 kwa ajili ya kujenga vituo vya kupozea nishati hiyo katika maeneo ya Sikonge,Inyonga na Mpanda. Mhe.Dr Samia ameyasema hayo leo julai 13-2024 wakati akihutubia maelfu ya wananchi wa Inyonga mkoani Katavi wakati wa ukaguzi wa kituo cha kupoozea umeme cha Inyonga ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 97 na kuitaka Tanesco kujipanga kusambaza nishati hiyo kwenda kwa wananchi baada kukamilika kwa ujenzi wa miundo mbinu hiyo. Amesema nishati ya umeme ni huduma lakini wananchi wana wajibu kulipia huduma hiyo muhimu kwa maendeleo yao na kwamba watumie nishati hiyo kuwekeza katika shughuli nbakimbali za kiuchumi na hivyo kuharakisha maendeleo ya mkoa huo. Ra...

Rais Dkt Samia Awasili Katavi Kwa Ziara Ya Kikazi

  "Nimewasili mkoani Katavi ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yangu ya kikazi ya siku nne mkoani hapa. Nikiwa hapa, nitazungumza na wananchi, nitakagua na kushuhudia hatua kubwa za maendeleo ambazo tumezipiga kwa pamoja, na kushirikishana mipango ijayo.  Takribani miezi mitatu ijayo tunatarajia kuiunga Katavi kwenye Gridi ya Taifa ili kupata umeme wa uhakika, ikiwa ni matokeo ya kukamilika kwa kazi nzuri ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme yenye uwezo wa kilovolti 132 ya urefu wa kilomita 383 kutoka Tabora hadi Mpanda, moja ya njia ndefu zaidi za kusafirisha umeme katika eneo la Afrika Mashariki. Pia, nikiwa Katavi nitajumuika na wananchi na kuzindua rasmi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambayo sasa ujenzi wake umekamilika, na kuondoa changamoto waliyokuwa nayo wananchi ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya za kibingwa" Amesema Dkt Samia. Asilimia kubwa ya wananchi wa mkoa huu ni wakulima. Ili kuendelea kuinua maisha yao zaidi kupitia kazi yao, tumetekeleza m...

Majaliwa Akagua Ujenzi wa Mnara wa Mashujaa Dodoma

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 12, 2024 amekagua  ujenzi wa Mnara wa Mashujaa  uliopo mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma ikiwa ni  maandalizi ya Siku ya Mashujaa itakayofanyika Dodoma, Julai 25, 2024. Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi wa mnara huo Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi na amemtaka mkandarasi wa mnara huo ambaye ni Suma JKT kukamilisha ujenzi kwa viwango na ubora ifikapo Julai 22 mwaka huu. Naye, mshauri elekezi kiongozi, Dkt. Ladislaus Mrema amesema kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa eneo hilo la mnara unajumuisha ujenzi wa uwanja wa gwaride, ngazi, njia za watu wenye mahitaji maalum pamoja na kitako cha mnara na bushati eneo la kuzunguka mnara “Mpaka  sasa mradi huu umefikia asilimia 84” Siku ya Mashujaa itafanyika Julai 25, mwaka huu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.