Skip to main content

Posts

Showing posts from October 2, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mgombea Ubunge wa Itilima Kwa Ccm Ndugu Njalu Ahimiza Amani na Utulivu

Mgombea Ubunge jimbo la Itilima kupitia chama Cha Mapinduzi Njalu Daudi Silanga Maarufu Profesa wa Maendeleo  ameendelea na kampeni kijiji kwa kijiji kuomba kura kwa wananchi yeye mwenyewe,Madiwani  na kumuomba kura Mgombea Urais wa CCM Dkt Samia Suluhu Hassan  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Njalu amefanya mikutano  ya Kampeni katika vijiji vya Nyantugutu,,Mwamalinze,Gaswa na Mwabuki ,huku mikutano yake ikihudhuriwa na mamia ya wananchi wanaokuja kusikiliza Sera za chama cha mapinduzi kwa ilani ya Ccm ya mwakan2025/2030  ambayo imelenga kuwaletea maendeleo wananchi. Akinadi Sera kwa  wananchi wa vijiji hivyo  Njalu amesisitiza upendo amani na utulivu siku ya tarehe 29 oktoba huku akiwaomba kujitokeza kwa wingi kupiga kura kumchagua Dkt Samia, kura za  ndiyo kwa Mbunge Njalu Silanga na  Madiwani wa CCM. "Leo Itilima tunajivunia hapa tulipo kwa sababu ya upendo na ushirikiano wetu ninawaomba ndugu zangu tuilinde amani na umoja hu...

Dkt Nchimbi | Wagombea Udiwani Tandahimba | Wataka Mitano Tena Kwa Dkt Samia

Pichani katikati ni Mgombea Mwenza wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja na Wagombea Udiwani katika wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtwara, baada ya kuwahutubia Wananchi katika jimbo hilo la Tandahimba, ambapo baadae alielekea Newala kwa ajili ya kuhitimisha mikutano yake ya Kusaka Kura za Ushindi wa Kishindo za CCM, mkoani Mtwara jana Oktoba 02, 2025. Dkt Nchimbi leo Oktoba 03, 2025, atafanya mikutano miwili ya hadhara akianzia Liwale  na kisha kuhitimisha siku kwa mkutano mkubwa wa hadhara katika Jimbo la Nachingwea mkoani Lindi. Dkt Emmanuel Nchimbi ambae ni mgombea mwenza wa Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Mikutano yake ya Kampeni za Urais amekuwa akinadi Sera na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025-2030, ambayo imelenga kwa dhati kuboresha maisha ya Wananchi kwa kuinua hali zao Kiuchumi.

Alex Msama Amwandikia Rais Samia Waraka Huu

  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amiri Jeshi Mkuu, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa,  na mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Watanzania wenzangu, Kazi na Utu?...... (Natumaini nyote mmeitikia, Tunasonga Mbele). Mhe. Rais na Watanzania wenzangu, kwa majina ninaitwa Alex Msama Mwita. Binafsi ni Mtanzania halisi, ninayetoka Kanda ya Ziwa, katika Mkoa wa Mara, makazi yangu ni Dar es Salaam, katika Manispaa ya Ilala, Jimbo la Uchaguzi la Ukonga, ambako nilitia nia ya kuomba nafasi ya Ubunge, ilivyo vyema ni kwamba Chama chetu kiliona wakati wangu bado, nami nilipokea kwa utiifu na unyenyekevu mkubwa maoni hayo. Mimi Alex Msama, ni mwanachama na kada mwaminifu mwenye kiapo cha utiifu kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kimaisha, mimi ni mfanyabiashara na muwekezaji wa kawaida, nikiwa Mkurugenzi wa Dira Media Group, Food Point, Msama Promotions na Msama Auction Mart. Ninaandika waraka au barua hii ya wazi, kutoa maoni ...

JKCI, HTAF waanzisha shindano la insha shuleni kuhusu magonjwa ya moyo

Na Mwandishi Wetu TAASISI ya Moyo ya Jakata Kikwete (JKCI), kwa kushirikiana na Heart Team Africa (HTAF) wameanzisha shindano la insha shuleni ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha watanzania wanatambua hatari ya magonjwa ya moyo tangu wakiwa wadogo. Shindano hilo lilizinduliwa Leo  na Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu, Dk Lyabwene Mtahabwa kwenye ofisi za HTAF jijini Dar es Salaam ambapo pia alikuwepo Mkurugenzi Mtendaji wa (JKCI), Dk Peter Kisenge na mratibu wa shindano hilo, Mwalimu Matuha Massati. Akizungumza kwenye mkutano huo, Dk Kisenge alisema kwenye shindano hilo, mshindi wa kwanza ataaondoka na 3,000,000 na kompyuta mpakato, mshindi wa pili kompyuta mpakato na 2,000,000, mshindi wa tatu atapata kishikwambi na 1,000,000. Dk Kisenge alisema mshindi wanne atapata Sh 500,000 na cheti wakati mshindi wa tano atapata shilingi 300,000 na cheti. Dk Kisenge alisema thamani ya shindano hilo ni kubwa sana hasa ikizingatiwa kuwa gharama za matibabu ya moyo ni kubwa na watu wengi hawana uwe...

Dkt Nchimbi Aahidi Neema Newala | Ccm Kuongeza Ruzuku Kwenye Mbolea na Mbegu Kwa Wakulima

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt .Emmanuel John Nchimbi amesema miaka mitano inayokuja Serikali ya Chama hicho imedhamiria kuendelea na mchakato ambao ulianzishwa na Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan, wa Kuboresha Kilimo ikiwemo pia kuongeza kiwango cha ruzuku ya mbolea kwa Wakulima katika wilaya ya Newala mkoani Mtwara. Dkt Nchimbi amebainisha hayo leo Oktoba 02, 2025 wakati akihutubia Wananchi kwenye uwanja wa mpira wa sabasaba,Newala  mjini,kwenye mkutano wake mkubwa wa hadhara wa Kampeni,akiendelea kuzisaka kura za ushindi wa kishindo za Chama Cha Mapinduzi (CCM). "Sambamba na hayo, Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Ilani yake ya Uchaguzi imejielekeza kuboresha Sekta ya Kilimo na Miongoni mwa Vipaumbele vyake ni kuongeza Ruzuku ya Mbegu kwa Wakulima wa hapa Newala na Kanda yote hii ya Kusini, bila kusahau kutanua wigo wa Watalaamu wa Masuala ya Kilimo 'Maofisa Ugani', tunataka kuwe na Wataalamu wengi zaidi ili...

Dkt Nchimbi "Dkt Samia Kuboresha Sekta ya Uchukuzi 'kusini' " Fursa za Kiuchumi Kuongezeka

Mgombea mwenza katika kiti cha Urais kupitia CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema kuwa Serikali ijayo Chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imepanga kuboresha sekta ya Uchukuzi mikoa ya kanda ya Kusini kwa kujenga meli mpya ya mizigo ikiwemo kupanua Kiwanja cha Ndege cha Mtwara, lengo ikiwa ni kuchochea kasi ya ukuaji wa Uchumi kwa Wananchi. Dkt.Nchimbi ametoa ahadi hiyo leo Oktoba 02, 2025 akihutubia maelfu ya Wananchi wa Tandahimba waliofurika kumsikiliza wakati akinadi Sera na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025-2030, katika muendelezo wa mikutano ya Kampeni za Urais kuelekea Uchaguzi  Mkuu wa Oktoba 29. "Nataka niwaambie ndugu zangu kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) moja ya ajenda zake muhimu ni kuhakikisha Sekta ya Uchukuzi inazidi kuimarika kwenye kanda hii ya kusini, ambapo baada ya Kuingia Madarakani tutajenga meli mpya ya Mizigo ambayo itasaidia kubeba Bidhaa kutoka hapa mtwara na kuzipeleka katika visiwa vya Comoro ili kuwa na Soko la Uhakika" amesema Dkt Nch...

Serikali Yaingiza Mabasi 60 Njia ya Kivukoni-kimara-Majaliwa*

_Asema sasa njia hiyo itakuwa na mabasi 90_ _Asema lengo ni kuhakikisha kero ya usafiri katika njia hiyo inakwisha_  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imeamua kuingiza mabasi 60 mapya kwenye Barabara ya mabasi yaendayo haraka njia ya Kimara hadi Kivukoni iliyokuwa na mabasi 30 yanayofanya kazi ili kukabiliana na upungufu wa magari uliokuwepo. Amesema kuwa idadi hiyo itafanya njia hiyo kuwa na mabasi 90 ambayo kwa kiasi kikubwa itasaidia kuondoa kero ya usafiri iliyokuwepo katika kipindi cha hivi karibuni. Amesema hayo leo Alhamisi ( Oktoba 02, 2025) alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma ya usafiri kwa mabasi yaendayo haraka kwa njia ya Kivukoni hadi Kimara jijini Dar es Salaam. "Serikali yenu baada ya kuruhusu makampuni binafsi tumeona tuchukue mabasi 60 kutoka kampuni ya Mofat yaingie katika barabara hii na yameanza kutoa huduma leo, malengo yetu ni kuondoa kadhia ya usafiri kwenye njia hii" Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameiagiza UDART na D...