Skip to main content

Posts

Showing posts from March 5, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia Akutana na Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuatana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi Audrey Azoulay, wakati Mkurugenzi huyo alipofika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Machi, 2025.

Majaliwa Mgeni Rasmi Kongamano la Siku ya Wanawake, Kanda Ya Kusini

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Machi 06, 2025 ni mgeni rasmi katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kanda ya Kusini, yanayofanyika katika viwanja vya Maegesho, Nachingwea mkoani Lindi. Kaulimbiu ya kongamano hilo kwenye Kanda ya Kusini ni: Ushiriki na Mchango wa Wanawake katika Kukuza Maadili, Uzalishaji na Kuongeza Mnyororo wa Thamani ya Mazao.

Waziri Mkuu Ashiriki Iftari na Benki Ya Nmb Pamoja na Watoto Wanaoishi Kwenye Mazingira Magumu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana Machi 05, 2025 ameshiriki hafla ya Iftari na Benki ya NMB pamoja na watoto wanaoishi katika Mazingira Magumu, kwenye ukumbi wa The Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam.

Waziri Kikwete Abainisha Mafanikio Matano Miaka 10 ya Wcf

*•Asaini Kanuni za Fao la Utengamao ( Rehabilitation Benefits)* Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutekeleza Kwa vitendo dhamira yake ya kuwalinda wafanyakazi ambao ni nguzo muhimu katika maendeleo ya Nchi yetu. Mhe. Ridhiwani amebainisha hayo leo Machi 4, 2025 Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mfuko huo tangu kuanzishwa kwakwe, ikiwa ni hatua kubwa katika kuimarisha ustawi wa wafanyakazi na familia zao. Amesema WCF imeongeza wigo wa mafao ambapo hadi sasa unatoa jumla ya mafao saba ikiwemo Fao la Matibabu yasiyo na kikomo, Fao la Ulemavu wa Muda Mfupi, Fao la Ulemavu wa Kudumu, Fao la pensheni kwa wategemezi, Fao la Wasaidizi wa Mgonjwa, Fao la Utengamao, na Fao la Msaada wa Mazishi. Pia, imeboresha mifumo ya ushughulikiaji wa fidia kwa wafanyakazi kwa kutumia mifumo ya TEHAMA ambapo hadi ...

Mbunge Mathayo Akamilisha ziara ya Kata 16 Na Kutangaza Kugombea Tena 2025

Na Shomari Binda-Musoma  MBUNGE wa Jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amekamilisha ziara yake ya kutembelea Kata kwa Kata kwa kutangaza kugombea tena nafasi hiyo kwenye uchaguzi mkuu wa 2025 muda utakapofika. Nia yake ya kugombea tena nafasi hiyo ameitoa leo machi 5/2025 kwenye Mkutano Mkuu wa Kata ya Mshikamano uliohudhuriwa na wajumbe na viongozi wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) wa Kata hiyo. Amesema kutokana na Kata 16 alizofanya ziara kuombwa kugombea tena nafasi hiyo hivyo hana budi kugombea muda utakapofika. Akielezea  utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020 hadi 2025 amesema utekelezaji umefanyika kwa asilimia kubwa hivyo kila mwana CCM anapaswa kutembea kifua mbele. Amesema kuanzia sekta ya elimu,maji,afya na miundombinu kwenye Kata ya Mshikamano imetekelezwa na kuwataka wanachama na viongozi kuisemea vizuri serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kila wanapopita. Mbunge huyo amesema bado ana nguvu na ari ya kuwatumikia wananchi wa jimbo la Musoma mjini na kwe...

Rcc Mkoa wa Mara imeridhia Kuligawa Jimbo la Serengeti

 Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mara (RCC) leo tarehe 03/3/2025 imekubaliana kwa kauli moja kuligawa jimbo la uchaguzi la Serengeti ili kupata majimbo mawili ya Serengeti Mashariki na Serengeti Magharibi. Wakitoa hoja kuhusu mgawanyo wa jimbo hilo, wachangiaji wote wamezungumzia kuhusu ukubwa wa jimbo hilo lenye kata 30 na kubeba asilimia kubwa ya eneo la Mkoa wa Mara.  Hoja hiyo imejadiliwa baada ya kupitishwa kwenye vikao vya kisheria vya ngazi za Wilaya na Halmashauri na baada ya kupitishwa kwenye RCC suala hilo litawasilishwa Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC) kwa ajili ya maamuzi.  Agenda nyingine zilizojadiliwa katika kikao hicho ni mapendekezo ya mpango na bajeti ya Sekrerieti ya Mkoa wa Mara na Mamlaka za Serikali za Mitaa, bajeti ya maendeleo ya sekta ya maji na nishati.

Dkt.Mpango Ataka Afrika Kubuni Njia Bora Uendelezaji Rasilimali za Nishati ili Kukidhi Mahitaji

  📌 *Asema upatikanaji wa Nishati Afrika bado ni mdogo kulinganisha na Mabara mengine* 📌 *Asisitiza uendelezaji wa vyanzo vya Nishati uzingatie mustakabali wa vizazi vijavyo* 📌 *Afungua Kongamano na Maonesho ya Petroli kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAPCE’25)* Makamu wa Rais, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango amesema kuwa matumizi ya nishati katika Bara la  Afrika hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara  bado ni madogo ikilinganishwa na maeneo mengine kama Bara la Amerika, Asia na Ulaya hivyo kuna umuhimu wa kubuni njia bora za kuzitumia rasilimali zilizopo ikiwemo Mafuta na Gesi Asilia ili kuwawezesha wananchi kustawi kiuchumi na kijamii huku suala la utunzaji wa mazingira likizingatiwa. Amesema hayo tarehe 5 Machi, 2025 wakati akifungua rasmi Kongamano na Maonesho ya Petroli ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAPCE’25) ambalo litafanyika kwa muda wa Siku Tatu jijini Dar es Salaam. “Katika kipindi ambacho maendeleo ya nishati endelevu yana mchango mkubwa katika m...

Waziri Mkuu Amesema Rais Samia anatekeleza Maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere

 _▪️Asema ni utekelezaji wa maono ya Hayati Mwalimu Nyerere_ _▪️Atoa wito kwa wananchi kutunza vyanzo vya maji_ _▪️Asisitiza mradi huo ni mwendelezo wa azma ya Rais Dkt. Samia kumtua mama ndoo kichwani_   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Machi 05, 2025 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa Bwawa la Kidunda litakalokuwa na uwezo wa kuhifadhi maji lita bilioni 190 ambalo linatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 335.8 hadi kukamilika kwake. Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kidunda, Wilayani Morogoro, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa ujenzi wa bwawa hilo ambao umefikia asilimia 28. Ujenzi huo ni utekelezaji wa maono ya Hayati baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambaye alidhamiria kulijenga ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro. “Bwawa hili lilikuwa katika historia tangu Serikali ya awamu ya kwanza na zilizofuatia, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya kuhakikisha maji ya kutosha yanapatikana...