MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi ameongoza majadiliano yaliyohusisha wananchi na viongozi kuelekea maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2026-2050. Akizungumza kwenye kikao maalum cha kamati ya ushauri ya mkoa ( RCC ) kilichofanyika agosti 19 kwenye ukumbi wa uwekezaji amesema tayari majadiliano hayo yamefanyika ngazi ya wilaya na sasa ni mkoa kabla ya kupelekwa maoni ngazi ya taifa kwenye tume ya mipango. Amesema Dira ya Taifa ya Maendeleo ni suala la msingi katika masuala mbalimbali hivyo mkoa unayo nafasi kwa wananchi na viongozi kujadiliana Mtambi amesema lengo la kikao hicho ni kutoa fursa kwa wananchi na viongozi wa mkoa wa Mara kutoa maoni yao kuhusu Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 ambayo ipo katika hatua za maandalizi. “Dira inaonyesha matamanio na vipaumbele vya wananchi,serikali na taasisi binafsi zinapo tamani kufikia kwa muda flani na mipango mbalimbali inawekwa ili kufikia lengo hilo” Mchakato wa maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo...
Marato tv - Sauti ya Jamii