Skip to main content

Posts

Showing posts from February 16, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kamati ya Waziri Jafo wageni Kariakoo yaendelea kuhoji wafanyabiashara

Na Mwandishi Wetu KAMATI iliyoundwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Selemani Jafo kuchunguza wafanyabiashara wa kigeni maeneo ya Kariakoo imefikia asilimia 50 ya uchunguzi wake na imeahidi kukabidhi ripoti hiyo Machi 2 kama ilivyoagizwa. Februari 2 Waziri Jafo aliunda Kamati ya watu 15 kuchunguza wafanyabiashara wa kigeni eneo la Kariakoo inayoongozwa na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Edda Lwoga Aliunda Kamati hiyo baada ya agizo la Rais Samia alitoa agizo hilo Januari 30, 2025, Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa halfa ya chakula cha mchana alichokiandaa kwa ajili ya washiriki wa shughuli ya uokoaji wa kuporomoka kwa jengo Kariakoo. Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Edda Lwoga ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE). Alisema baada tu ya uteuzi walianza rasmi kazi ya kuwahoji wafanyabiashara wa makundi mbalimbali kama machinga, wauza vifaa vya umeme, vifaa vya magari,  vipodozi na biashara zi...

Majaliwa Amwakilisha Rais Dkt. Samia Kwenye Kilele Cha Maadhimisho Ya Miaka Ishirini Ya Heslb

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Februari 17, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, inayofanyika kwenye Kituo cha Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yaliambatana na kliniki za huduma katika mikoa 7 nchini yakilenga kutoa elimu kwa wadau muhimu wa masuala ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu. kaulimbiu ya maadhimisho ni _”Maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu- Athari chanya, Ubunifu na Huduma’’._

Dkt. Biteko Awahimiza Watanzania Kuliombea Taifa

📌 *Asema amani ya nchi ilindwe kwa wivu mkubwa* 📌*Asisitiza uchaguzi Mkuu wa Oktoba usiligawe Taifa* 📌*Asema Watanzania waendelee kumuombea Rais Samia kwa kazi nzuri anazofanya* 📌 *Serikali kuboresha mipango yake kulingana na mahitaji ya dunia* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuiombea nchi pamoja na Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. “ Tuendelee kuliombea kanisa, tuendelee kuiombea nchi yetu na Rais wetu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae kwa kweli anafanya kazi nzuri na sisi tunaofanya kazi karibu naye tunaona,” amesema Dkt. Biteko. Dkt. Biteko amesema hayo leo Februari 16, 2025 wakati akishiriki ibada katika Kanisa la Africa Inland Church Chang’ombe jijini Dar es salaam. Amewahimiza Watanzania kudumisha upendo na amani nyakati zote hususan kipindi hiki kuelekea Uchaguzi...

Waziri Mkuu akagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa ndege Shinyanga

  _▪️Amtaka mkandarasi kuharakisha uwekaji wa taa kwenye uwanja hio ili uanze kutumika nyakati za usiku._   _▪️Asema hana shaka na viwango vya ujenzi vya uwanja huo._   _▪️Amesema Kukamilika kwa uwanja huo kutaibua fursa kwa wakazi wa Shinyanga na maeneo ya jirani._ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga afanye kazi usiku na mchana ili kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa uwanja huo ikiwemo ufungaji wa taa na uanze kutumika wakati wote. Amesema kuwa uwanja huo niwa kimkakati uliokuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu na wakazi wa mkoa wa Shinyanga na maeneo ya jirani ikiwemo mkoa wa Simiyu. Amesema hayo leo Jumapili (Februari 16, 2025) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga ambao kwa ujumla ujenzi wake umefikia Asilimia 73.9.  “CHICO tunajua unafanya kazi nzuri, hapa kasoro yako unachelewesha kuingiza vifaa vilivyobaki, Meneja wa TANROAD ameniambia mmekamilisha kwa asilimia 100 kwenye ...

Kikwete Atoa Aina 25 Ya Vifaa Kwa Wenye Ulemavu, Aishukuru Serikali Na Kuahidi Kuwa Itaendelea Kuboresha Elimu Kwa Makundi Yote

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kupitia Serikali kuendelea kuhakikisha wanatoa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum. Kikwete ameyasema hayo Jana Februari 15, 2025 katika Ofisi za Halmashauri ya Chalinze alipokuwa akikabidhi aina 25 ya vifaa kwa watoto wenye mahitaji maalumu. Pia Mhe Ridhiwani ameishukuru Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze kwa usimamizi mzuri wa fedha na kutoa elimu kwa wazazi ili kuona umuhimu wa kuwapeleka shule watoto hao na ameahidi kuwa serikali italeta fedha ili kukamilisha ujenzi wa mabweni. Aidha Mhe Mbunge amesema kupitia mfuko wa Jimbo wameleta jumla ya madawati 500 pia wataendelea kuhakikisha wanasaidia ili kutatua changamoto zilizopo na kuweka mazingira mazuri kwa watoto ili waweze kusoma kama wengine. Pia ametoa pongezi kwa walimu wanaofundisha watoto hao . Akiwas...

Rais Samia Ameshiriki Mkutano Wa Mabadiliko Ya Tabia Nchi Nchini Ethiopia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki mkutano wa Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (CAHOSCC) kando ya Mkutano wa Kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU), Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari, 2025.

Viwanda Vinne Vya Uongezaji Thamani Madini Kujengwa Mkoani Dodoma-waziri Mavunde

▪️Akagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchenjua Madini ya Shaba* ▪️Dodoma inaongoza kwa uwepo wa aina nyingi za madini nchini* ▪️Atoa rai kwa Mikoa kutenga meneo maalum ya viwanda vya kuongeza thamani *📍 Dodoma* Waziri wa Madini *Mhe. Anthony Mavunde* amesema, ujenzi wa Viwanda vinne vya Uchenjuaji Madini ya Shaba ikiwemo kiwanda cha *Shengde Precious Metal Resources Co. Limited* kinachoendelea kujengwa katika eneo la Mahungu Kata ya Nala Jijini Dodoma vinatarajiwa kuwa mkombozi wa Wachimbaji Wadogo wa Madini ya Shaba nchini. Waziri Mavunde amebainisha hayo leo Februari 16, 2025 baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho na kutoa pongezi kwa Kampuni ya Shengde Precious Metal Resources Co. Limited kwa uwamuzi wa kujenga kiwanda hicho Jijini Dodoma . Aidha, Waziri Mavunde amesema Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wetu *Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan* imedhamiria kwa dhati kuyaongezea thamani madini hapa hapa nchini ili kukuza ajira kwa wa...