Skip to main content

Posts

Showing posts from May 8, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mbarawa Awaomba Watanzania Kushirikiana na Trc Kulinda Miundombinu ya Reli

 Waziri wa uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, amewasihi Watanzania kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC), kuilinda na kuitunza miundombinu ya treni ya kisasa ya Umeme (SGR). Prof. Mbarawa, ametoa wito huo katika stesheni ya Magufuli Dar es Salaaam, muda mchache baada ya kumsindikiza Rais wa Msumbiji Fransisco Chapo, aliyesafiri kwa SGR kutoka Stesheni ya Magufuli kwenda stesheni ya Pugu na kisha kurejea stesheni ya Magufuli, kwa lengo kushuhudia mradi huo ambao ni wa kilelezo barani Afrika. Waziri wa Uchukuzi amesema Rais Chapo, aliyeko nchini kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu aliyoaianza Mei 07, 2028 ameeleza kufurahishwa na mradi huo aliosema ni wa kiwango cha dunia na kuwataka Watanzania, kuulinda kwa wivu. Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkuu wa TRC Bw. Masanja Kadogosa, alisema kuwa ujio wa Mhe. Chapo ni ishara tosha ya kwamba Afrika inajua nini kinachoendelea Tanzania na pia kuzidi kudumisha mahusiano baina ya nchi za Afrika na kuimarisha katika ufanyaji biashara ...

Waziri Mavunde Azindua Taarifa ya Uchambuzi Uongezaji Thamani Madini Muhimu Tanzania

  ◾️ Asema Tanzania imeanza Safari ya Mageuzi ya Sekta ya Madini kuchochea ukuaji wa viwanda.  ◾️ Asisitiza dhamira ya Tanzania kuwa kitovu cha bidhaa zitokanazo na madini muhimu.  ◾️ Balozi wa Uingereza nchini asema hatua hiyo ni kielelezo cha ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza.  📍 *Dodoma* Waziri wa Madini Mhe.  Anthony Mavunde ameeleza kuwa, Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua hatua madhubuti kuelekea mageuzi ya kweli ya Sekta ya Madini hapa nchini kwa kuanza rasmi mkakati wa kuongeza thamani ya madini muhimu yanayopatikana nchini.  Alieleza hayo Mei 8, 2025  wakati akizindua rasmi  Taarifa ya Uchambuzi wa Kina wa Uongezaji Thamani Madini Muhimu na Mkakati ya Tanzania (Manufacturing Africa – Critical Minerals Value Addition Study), katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma.  Akizungumza katika Mkutano huo uliohudhuriwa na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Marianne Young akiongozana na maafisa wandamizi wa Ubalozi huo, wad...