Skip to main content

Posts

Showing posts from January 22, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Hussein Mwinyi:Tujiandikishe Tupige Kura,Ccm Ishinde Kwa Kishindo

Mgombea Mteule wa Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk .Hussein Ali Mwinyi amepokewa na Mamia ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, Viongozi na Wananchi alipowasili Zanzibar akitokea Dodoma alipoteuliwa Kupeperusha Bendera ya Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu Ujao katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Uliofanyika hivi Karibuni. Mgombea Mteule Dk. Mwinyi alipokelewa na Mamia ya Wana CCM, pamoja na Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi, Serikali , Vyombo vya ulinzi na usalama na Dini. Mamia ya Wananchi wa Zanzibar na Wana CCM walijitokeza kwa Wingi Pembezoni mwa Barabara kuu ya Uwanja wa Ndege- Kilimani kumpokea Dk ,Mwinyi aliyekuwa katika Gari la Wazi akiwapungia Mkono hadi Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui. Mgombea Mteule wa Urais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi alizuru Kaburi la alieyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume na Kuweka Shada la Maua pamo...

Mhe. Wanu H. Ameir amewasilisha Taarifa ya Oacp/Eu Kwenye Kamati ya Bunge

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. Vita Kawawa wamepokea na kujadili Taarifa ya Wawakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mabunge ya Afrika, Carribeani Pasifiki na Jumuiya ya Ulaya (OACP/EU). Aidha, Taarifa hiyo imewasilishwa na Mjumbe wa Umoja wa Mabunge ya Afrika, Carribeani Pasifiki na Jumuiya ya Ulaya (OACP/EU) kutoka Bunge la Tanzania, Mhe. Wanu Hafidh Ameir katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika tarehe 21 Januari, 2025 Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

Rais Samia atumia Treni Dodoma hadi Dar es salaam

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Stesheni ya Dar es Salaam wakati akitokea Mkoani Dodoma kwa usafiri wa Treni ya umeme ya (SGR) tarehe 22 Januari, 2025.

Bashungwa aapishwa Kuwa Mwenyekiti Wa Tume ya Jeshi La Polisi, Magereza, Zimamoto na Uhamiaji

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameapishwa na Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dodoma, Edwin Kakolaki kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Idara ya Uhamiaji, leo tarehe 21 Januari 2025 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kituo Jumuishi cha Utoaji wa Haki jijini Dodoma. Aidha, Jaji Kakolaki amewaapisha Kamishna wa Polisi Zanzibar, CP. Kombo Khamis Kombo na Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu katika Jeshi la Polisi, CP. Tatu Rashid Jumbe kuwa wajumbe wa Tume hiyo. Akizungumza mara baada ya uapisho, Jaji Kakolaki amemsisitiza Mwenyekiti wa Tume na Wajumbe kutekeleza majukumu yao kwa ufasini, weledi na kutenda haki kwa mujibu wa Sheria. “Niwaombe mtekeleze majukumu yenu bila upendeleo wala uonevu lakini mkiwa mnaongozwa na sheria, taratibu, miongozo na taratibu nyingine za kimazoea (busara)” amesisitiza Jaji Kakolaki Jaji Kakolaki amemhimiza Mwenyekiti wa Tume na Wajumbe kutimiza wajibu wao kw...

Rais Samia atumia Treni Dodoma hadi Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Stesheni ya Dar es Salaam wakati akitokea Mkoani Dodoma kwa usafiri wa Treni ya umeme ya (SGR) tarehe 22 Januari, 2025.