Na Beda Msimbe,TBN, Moscow Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi- (RUDN University) huku akiitoa shahada hiyo kwa Watanzania. Shahada hiyo ilitolewa na Mkuu wa Chuo hicho Profesa Oleg Yastrebov kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo Moscow nchini Urusi, tarehe 04 Juni,2026. Rais Mhe. Dk Samia ametunukiwa Shahada hiyo ya Uzamivu kutokana na mchango wake katika Mageuzi ya sekta ya Elimu, juhudi zake za kuimarisha Diplomasia ya Tanzania, pamoja na mchango wake katika kuimarisha hadhi ya Tanzania Kimataifa ikiwemo kupitia sekta ya Utalii, Akizungumza baada ya kupewa shahada hiyo Rais Samia alisema kwamba heshima aliyopewa si ya mafanikio yake binafsi bali ni utambuzi wa juhudi na matarajio ya watanzania wote. Alisema shahada hiyo ni ishara ya utambuzi wa dhamira ya pamoja ya Watanzania wote katika kuleta maendeleo,ushirikiano na ustawi wa binadamu. “Nil...
Marato tv - Sauti ya Jamii