Skip to main content

Posts

Showing posts from February 27, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Dkt Samia awashukuru wana-Muheza kwa kumchagua MwanaFA

📍 Asema watu walimshangaa alipomteuwa kuwa Naibu Waziri  📍Walisema msanii wa Kurap atafanya nini serikalini  📍 Asema MwanaFA ni msaada mkubwa Serikalini 📍Awataka wana-Muheza wamsaidie kumlea katika kazi zake za ubunge 📍 Mwenyewe MwanaFA amshukuru Rais kwa kumrahisishia ubunge wake miaka hii minne 📍 Changamoto zote tatu alizomuomba Rais zapata majibu mazuri Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa watu walikuwa na wasiwasi alipowateua Hamis Mwinjuma kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, pamoja na Nickson Simon (Nikk wa Pili) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha. Hata hivyo sasa wamethibitisha kuwa hatua ya kuwateua hakukosea kwa kuwa wamekuwa na msaada mkubwa katika Taifa. Akizungumza  leo tarehe 27 Februari, 2025, wilayani Muheza, Mkoani Tanga, Rais Samia amesema: "Nawashukuru sana Muheza kwa kumlea kijana wetu Mwana FA, Mh. Hamisi Mwinjuma, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, na Mbunge wenu. Kijana huyu anatusaidia sana...

Serikali imetenga Bilioni 1.3 Uwanja wa Ndege Serengeti

  Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) imetiliana saini na Kampuni ya Saba Engineering kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Serengeti katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Mkoa wa Mara tarehe 27 Februari, 2025 Jijini Dar es salaam.  Akizungumza katika hafla ya kutia saini mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu wa TAA Bwana Abdul Mambokaleo amesema Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa uwanja huo katika mwaka wa fedha 2024/2025.  “Kampuni ya Saba Engneering imepewa mkataba wa miezi sita na baada ya kukamilisha upembuzi  yakinifu itatoa ushauri wa kitaalamu wa namna bora ya kujenga uwanja huo” amesema Bwana Mambokaleo.  Bwana Mambokaleo amesema kuwa Serikali inajenga uwanja huo ili kuongeza idadi ya watalii wanaoitembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) pamoja na kurahisisha usafiri wa wananchi na mizigo kuingia katika Mkoa wa Mara.  Kwa upande wake, Mkurug...

Mkuu Wa Majeshi Aongoza Maelfu Ya Wananchi Mkoa Ruvuma Kumbukizi Ya Miaka 120 Vita ya Majimaji

 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amewaongoza maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na maeneo jirani katika Maadhimisho ya Miaka 120 ya Kumbukumbu ya Vita vya Majimaji yaliyofanyika tarehe 27 Februari 25 katika eneo la Makumbusho ya Vita vya Majimaji mjini Songea. Katika hotuba yake Jenerali Mkunda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyotoa kipaumbele katika kuhifadhi Kumbukumbu muhimu za Mashujaa wa Tanzania waliopambana ili kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa salama. Amewaomba wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na maeneo yote ambayo Vita vya Majimaji vilipiganwa kuendelea kutunza historia hii nzuri kwaajili ya urithi kwa vizazi vijavyo.   Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abass Ahmed amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Chifu Hangaya kwa namna anavyohamasisha utamaduni ili kutunza historia na kuku...

Serikali Kutunga Sera Na Sheria Ili Kuharakisha Matumizi Ya Nishani Safi Nchini-Rais Samia

 Na MASHAKA MHANDO, Mkinga  Na Hadija Bagasha Tanga,  Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inakwenda kutunga sera na sheria ili kuharakisha mkakati wa matumizi ya nishati safi na kuweza kufikia lengo la watumiaji asilimia 80 ifikapo 2030. Rais Dkt Samia ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa nishati safi ya kupikia na ugawaji wa mitungi ya gesi kwa wananchi Wilayani Muheza Mkoani Tanga. Rais alisema kuwa sera hizo rafiki ambazo wanakwenda kuzitunza zitawezesha ushiriki wa sekta binfsi na makampuni yanayojihusisha na uzalishaji wa nishati safi ya kupikia kwa bei nafuu.  Alisema dhamira ya sasa kama tukiendelea kutumia kuni na mkaa kama nishati kuu ya kupikia tunakwenda kuwa na majanga ambayo yatasababisha kukauka kwa vyanzo vya maji kutokana na ukataji wa miti lakini pia upo uwezekano mkubwa wa kupata maradhi ya kifua kutokana na matumizi ya kuni.  "Kwasasa tulisema asilimia 80 ya watu wetu ikifika 2030 waw...

Mongela aongoza kuaga wanne wa ajali ya Mbeya

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndugu John Mongella, leo tarehe 27 Februari 2025 ameongoza shughuli ya kuaga miili ya marehemu wanne waliopoteza maisha katika ajali ya gari wakati wakitokea kwenye ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Fadhili Maganya, mkoani Mbeya. Akiwasilisha salamu za rambirambi kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Mongella amesema chama kimetoa ubani  wa shilingi milioni 20 kwa familia za marehemu na shilingi milioni 6 kwa majeruhi sita wanaoendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya. Mongella ametoa pole kwa familia za marehemu na kuwataka kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu.  Shughuli ya kuaga miili ya marehemu hao  imefanyika katika Viwanja vya Soko la Uhindini, jijini Mbeya.