Skip to main content

Posts

Showing posts from March 9, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MwanaFA ashuhudia mafundi wa soka Yanga

📍Aisifu GSM na Rais Hersi kwa kukuza vipaji vya watoto Na Mashaka Mhando Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma (MwanaFA), amemwagia sifa Klabu ya Yanga na Taasisi ya GSM Foundation kwa jitihada zao za kuwekeza katika soka la vijana nchini, akisema hatua hiyo ni mustakabali wa mafanikio ya Taifa katika mchezo wa mpira wa miguu. Mhe. Mwinjuma aliyasema hayo jana alipokuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa programu ya "Safari ya Soka" iliyoandaliwa na Klabu ya Yanga kwa kushirikiana na GSM Foundation, tukio lililofanyika katika viwanja vya Gymkhana Club, Dar es Salaam. Akipokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said, Naibu Waziri huyo alipata fursa ya kushuhudia vijana wadogo wakionyesha umahiri wao uwanjani, jambo ambalo alikiri kuwa limempa matumaini makubwa. "Nimejionea mwenyewe, nchi hii ina 'mafundi' wa soka haswa. Vipaji vipo vingi sana, kinachohitajika ni uangalizi wa karibu na weledi kama huu unaofany...

Rais Dkt Samia amkumbuka nguli Zahir Zorro

📍Amtuma MwanaFA na shilingi milioni 10 Na Mashaka Mhando Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemtumia salamu za faraja na mkono wa heri nguli wa muziki wa dansi nchini, Mzee Zahir Ally Zorro, ambaye kwa sasa anakabiliwa na changamoto za kiafya. Salamu hizo za Rais zimefikishwa nyumbani kwa mwanamuziki huyo Kisota, Kigamboni Jijini Dar es salaam leo na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma (MwanaFA). Katika ziara hiyo, Mhe. Mwinjuma alipokelewa na Mzee Zahir Zorro pamoja na mwanawe, mwanamuziki nyota wa R&B, Banana Zorro. Akizungumza kwa niaba ya Rais, Mhe. Mwinjuma alisema kuwa Mkuu wa Nchi ameguswa na hali ya Mzee Zorro na ametambua mchango wake usiofutika katika utamaduni na sanaa ya Tanzania. "Nimetumwa na Mheshimiwa Rais kuja kukujulia hali na kukushika mkono. Rais anajua mchango wako na ameelekeza nikukabidhi kiasi hiki cha Shilingi Milioni 10 kusaidia taratibu zako za matibabu na mahitaji mengine,...

Waziri Mkuu Akagua Bandari ya Kasanga Mkoani Rukwa

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Jumanne (Machi 10, 2026) amekagua miundombinu na utendaji kazi wa Bandari ya Kasanga iliyopo Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani humo. TPA ilifanya upanuzi wa bandari ya Kasanga mwaka 2019 kwa kuongeza urefu wa gati kutoka mita 20 hadi 120 ya kina cha mita 14 pamoja na ujenzi wa nyumba za wafanyakazi na jengo la kuhudumia abiria 200 kwa wakati mmoja kwa gharama ya shilingi bilioni 4.7. Pia kumejengwa maghala mawili ya kuhifadhi mizigo yenye uwezo wa tani 2,500 kila moja. Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Desemba 2025, bandari hiyo imehudumia jumla ya tani 3,418 za mizigo, abiria 3,648, meli 11 pamoja na maboti 337. Miongoni mwa mizigo inayohudumiwa katika bandari hiyo ni saruji, makaa ya mawe pamoja na mazao ya chakula kama mahindi, mchele na unga wa sembe. Bandari hiyo ni miongoni mwa miundombinu ya kimkakati inayochochea shughuli za usafirishaji na biashara katika ukanda wa Ziwa Tanganyika na kuchangia ukuaji...

Rais Dkt Samia amfuta machozi Galacha Hassan Bitchuka

📍Amtumia shilingi milioni 10 Na Mashaka Mhando Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemjulia hali na kumpatia mkono wa pole nguli wa muziki wa dansi nchini, Mzee Hassan Rehani Bichuka, ambaye kwa sasa anauguza maradhi nyumbani kwake Sinza Mori, jijini Dar es Salaam. Salamu hizo za faraja zimefikishwa jana, Machi 9, 2026, na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma (MwanaFA), aliyefika nyumbani kwa mwanamuziki huyo kwa niaba ya Rais. Akikabidhi kiasi cha Shilingi Milioni 10 taslimu kutoka kwa Mheshimiwa Rais, Mhe. Mwinjuma alisema kuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anathamini mchango usiopimika ambao Mzee Bichuka ametoa katika kuijenga sanaa ya Tanzania kupitia sauti yake na tungo zilizolimika taifa kwa miongo mingi. "Mheshimiwa Rais Samia amenituma nifike hapa kukupelekea salamu zake za pole na upendo. Anakuombea upate nafuu ya haraka na ameelekeza nikukabidhi kiasi hiki cha Shilingi Milioni 10 kwa ajili ya kusaidia t...

Asilimia 89 ya Vitongoji Nkasi Vimefikiwa na Umeme- Mhe.Salome

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amesema asilimia 89 ya vitongoji 724 wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa  vimesambaziwa umeme, na vitongoji vilivyosalia  vitakuwa vimesambaziwa nishati hiyo ifikapo 2030. Mhe. Salome amesema hayo katika Mji wa Namanyere, Wilaya ya Nkasi, Mkoa wa Rukwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba. “Sisi Sekta ya Nishati jukumu letu ni kuhakikisha Watanzania wote wanapata umeme wa uhakika wakati wote. Hapa Nkasi kwa sasa wanatumia umeme kutoka nchini Zambia kupitia makubaliano ya kikanda ya kuuza na kununua umeme ili kuweka mfumo imara wa upatikanaji wa umeme. Hata hivyo, tunatarajia kama kila kitu kitakwenda sawa, Nkasi itapata umeme wa gridi ifikapo mwezi Mei mwaka huu,” amesema Mhe. Salome Ameongeza kuwa, mradi wa kupeleka umeme wa gridi mkoani Rukwa unaendelea vizuri na mara umeme huo utakapofika mkoani humo,  wananchi watanufaika na umeme wa uhakika  huku pia wakiwa na nafasi ya kupata umeme wa ziada kutoka nchi...

Mabadiliko Makubwa Yaja Wizara ya Mambo ya Ndani_Katambi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na Uboreshaji wa Ofisi, Makazi, Vifaa vya Kazi, Maslahi, Mikakati na Mafunzo ili vyombo hivyo viweze kujitegemea ambapo pia amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Ofisi za Mji wa Serikali,Mtumba. Ametoa kauli hiyo wakati wa ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa Gereza la Msalato jijini Dodoma ambapo mradi huo unajengwa wa wakandarasi wa ndani ya Jeshi la Magereza huku wafungwa wakipata fursa ya kushiriki ujenzi huo ikiwa ni mpango wa kuwawezesha kupata ujuzi sambamba na utekelezaji wa dhana ya urekebu kwa wafungwa hao ili wakimaliza vifungo wawe na ujuzi waliopata wakati wakitumikia vifungo. Akizungumza katika ziara hiyo,Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza,CGP Jeremiah Katungu amesema gereza hilo kukamilika kwake litaweza kuhifadhi wafungwa 1080 ambapo pia linajumuisha kituo cha afya,chumba cha mahakama mtandao amb...

Tanzania Yashika Nafasi ya Nne Kwa Uwekezaji Sekta ya Madini Afrika

▪️Ni ya 4 barani Afrika, nyuma ya Botswana, Morocco na Zambia ▪️Alama ya Tanzania yapanda hadi 68.04 mwaka 2025 kutoka 62.75 (2024) na 46.38 (2023) ▪️Tanzania yaorodheshwa nafasi ya 15 duniani kwenye Best Practices Mineral Potential Index kwa alama 75.00 ▪️Utafiti uliwahusisha wataalam na viongozi 2,304 wa kampuni za utafiti na uchimbaji. ▪️Rais Samia apongezwa kwa mazingira mazuri ya Uwekezaji Tanzania Tanzania imeendelea kuimarisha nafasi yake kama kivutio cha kimataifa cha uwekezaji kwenye sekta ya madini baada ya kuorodheshwa miongoni mwa maeneo yanayoongoza barani Afrika, kwa mujibu wa ripoti ya *Fraser Institute, Annual Survey of Mining Companies 2025.* Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Tanzania imepata nafasi ya 34 kati ya maeneo 68 duniani yaliyotathminiwa katika Investment Attractiveness Index (IAI), kielezo kinachotumiwa na wawekezaji na kampuni za utafiti wa madini kuamua wapi waelekeze mitaji ya utafiti na maendeleo ya miradi.  Katika muktadha wa Afrika, Tanzania imeendelea ku...

Dkt.Mwigulu: wanafunzi watakaofaulu vizuri kusomeshwa na nchi kupitia Samia Scholarship

_Awafikishia wanafunzi salamu za Rais Dkt. Samia; asema Serikali inaendelea kuwekeza katika elimu_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema wanafunzi watakaofaulu kwa viwango vya juu watanufaika na ufadhili wa masomo kupitia mpango wa Samia Scholarship unaotolewa na Serikali. Dkt. Mwigulu amesema hayo wakati akizungumza na wanafunzi katika ziara yake mkoani Rukwa, ambapo pia aliwasilisha salamu maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. “Daktari Samia Suluhu Hassan anasema kwa wale watakaofaulu kwa kiwango cha juu wanapata ufadhili asilimia 100. Na sio ufadhili tu wa asilimia 100 peke yake, asilimia 100 na unaenda kusoma nchi yoyote duniani… hiyo inaitwa Samia Scholarship,” alisema Waziri Mkuu. Aidha, alisema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya elimu ambapo zaidi ya shule za sekondari 1,300, shule za msingi zaidi ya 2,700 pamoja na maelfu ya madarasa yamejengwa katika maeneo mbalimbali nchini. Alion...