Skip to main content

Posts

Showing posts from July 20, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mining Commission Sets Strategic Communication Plan to Boost Investment in Mineral Sector

_Iringa, July 21, 2025_ In a bold move to attract both local and international investors, the Mining Commission has unveiled a new Communication Strategy aimed at promoting Tanzania’s mineral sector and showcasing its immense potential. The strategy is part of a broader effort to position the country as a premier destination for sustainable and profitable mining ventures. Speaking during the official launch held at the Iringa Resident Mines Office, Greyson Mwase, Communication and Public Relations Manager of the Commission, emphasized that the strategy is designed to project Tanzania as an investor-friendly mining hub.  He stated that the initiative reflects the Commission’s commitment to delivering accurate, timely, and accessible information to stakeholders across the value chain. “This strategy is a deliberate step towards branding Tanzania’s mineral sector as open, well-regulated, and full of untapped opportunities. It aims to strengthen public trust and stakeholder engagement ...

Kikwete aunguruma China, asema Sasa ni wakati wa Vijana

* Asema wapewe nafasi waoneshe uwezo wao Na Mwandishi Maalum, China  MANENO hayo yamezungumzwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayesimamia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ndg. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akihutubia mkutano wa Vijana Wa Dunia katika Mji wa Suzhou, China. Mkutano huo ambao ukutanisha vijana toka nchi mbalimbali duniani wakiwemo toka asasi za kiraia, mashirika ya kitaifa na kimataifa na serikali mbalimbali, ulibeba ujumbe unaosema Vijana ni Chachu ya Maendeleo Endelevu wapewe nafasi kuonyesha Uwepo Wao.  Mkutano huo umekamilika kwa kutengeneza maazimio ambayo kila nchi iliyoshiriki itapaswa kuyaangalia ili kunyanyua ustawi wa vijana katika kushiriki ujenzi wa mataifa.  Mkutano huo ambao ulilenga pia kuangalia mafanikio katika utekelezaji wa Malengo ya Millenia kwa upande wa vijana ulihudhuria na kuhutubia kwa njia ya mtandao moja kwa moja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Gilbert Houngbo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Um...

Waziri Mkuu Aelekea Belarus Kwa Ziara ya Kikazi

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa, leo Julai 20, 2025 ameondoka nchini kuelekea nchini Belarus kwa ziara rasmi ya kikazi ya siku tatu. Ziara hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kukuza fursa za kiuchumi kati ya Tanzania na Belarus. Katika ziara hiyo, Mhe. Majaliwa anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Belarus, Alexander Turchin ambapo watajadili masuala ya ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu,Kilimo na viwanda. Waziri Mkuu pia atapata fursa ya kutembelea kiwanda kikubwa cha kutengeneza dawa nchini humo cha Republican Unitary Production Enterprise na kujionea mbinu za kisasa za uzalishaji wa bidhaa za afya.  Aidha, Mheshimiwa Majaliwa pia atatembelea kiwanda cha matrekta cha Minsk Tractor Works JSC pamoja na chuo kikuu cha Agrarian State University Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa anatarajiwa kufanya mikutano ya uwili itakayojumuisha viongozi wa kiserikali na Chama cha wafanyabiashara wa Belarus cha AFTRADE. Lengo la mikutano ...

Wafukua kaburi na kusepa na kichwa

Na MASHAKA MHANDO, Tanga JESHI la polisi mkoani Tanga, linafanya uchunguzi wa kuwasaka watu waliohusika  kufukua kaburi na kukata kichwa cha marehemu aliyezikwa na kundoka nacho. Akizungumza ofisini kwake Leo Julai 20, Kamanda wa polisi mkoani Tanga, ACP Alimachius Mchunguzi alisema jeshi hilo linafanyia uchunguzi taarifa za watu kufukua kaburi na kundoka na kichwa na kubakisha mwili kwenye kaburi. Akifafanua Kamanda Mchunguzi alisema kuwa tukio hilo lilitokea Julai 18 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi baada ya wananchi kutoa taarifa za kufukuliwa kaburi la mtu mmoja aliyezikwa katika makaburi ya familia Julai 12 mwaka huu katika Kijiji cha Mgela kilichopo wilayani Kilindi. Kamanda Mchunguzi alimtaja marehemu huyo kwa jina la Mohamed Athumani Mjaila (85) ambaye alifariki dunia Julai 11  na kuzikwa siku iliyofuata katika makaburi yao ya ukoo  katika Kijiji hicho. "Ni kweli tukio hilo limetokea Julai 18 majira ya asubuhi huko katika Kijiji cha Mgela kwenye makaburi ya fam...

DC Itunda amwakilisha RC mkutano wa Kimataifa

* Ni wa kujadili uhusiano wa maji, Nishati na Chakula Na Mwandishi Wetu, Mbeya MKUU wa Wilaya ya Mbeya, Solomon Itunda, amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Beno Malisa, katika Mkutano wa Kimataifa wa nchi tisa uliojadili namna bora ya kuunganisha rasilimali za maji, nishati na chakula ili ziweze kumnufaisha binadamu. Mkutano huo wa kihistoria umefanyika Jijini Mbeya ambapo uliandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI). Akifungua mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Itunda alisisitiza kuwa rasilimali za maji, nishati na chakula zinapaswa kutazamwa kwa jicho la pamoja kwani zinategemeana kwa kiasi kikubwa.  Alieleza kuwa mustakabali wa maendeleo endelevu ya jamii yoyote hauwezi kufikiwa endapo uhusiano kati ya sekta hizo hauzingatiwi kwa pamoja katika sera, mipango na utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Mkutano huo umehusisha wataalamu wa ndani na nje ya nchi kutoka mataifa tisa waliobadil...