Skip to main content

Posts

Showing posts from August 25, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Mwinyi Atunukiwa Phd ya Uchumi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu (PhD Honoris Causa) ya Uchumi iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU), ambayo ilitangazwa rasmi Desemba 2024 katika mahafali ya Chuo hicho. Mkuu wa Chuo hicho, Mhandisi Abdulqadir Othman Hafez, alikabidhi rasmi Shahada hiyo kwa Rais Dkt. Mwinyi Ikulu Zanzibar leo tarehe 25 Agosti, 2025. Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amekipongeza Chuo hicho kwa kuthamini na kutambua juhudi zake katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Zanzibar, hatua ambayo ameieleza kuwa itamwongezea ari ya kuendeleza maendeleo zaidi nchini.

Mutasingwa Achukua Fomu ya Ubunge Jimbo la Bukoba Mjini

 Na Angela Sebastian; Bukoba  Mgombea ubunge jimbo la Bukoba mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mhandisi Johnston Mutasingwa amewaomba wanachama wa chama hicho katika jimbo hilo kufuta makundi na kuungana kwa ajili ya kutafuta kura za kishindo za chama hicho. Mutasingwa ametoa wito leo wakati akizungumza na wananchi wa jimbo hilo waliomuunga mkono na kumsindikiza katika ofisi ya tume ya uchaguzi Manispaa ya Bukoba kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo. Amesema umoja na mshikamano ikiwemo kufuta makundi kwa wanachama wa CCM katika kata ya jimbo hilo vinahitajika ili kuhakikisha chama chama mapinduzi kinapata kura nyingi za wagombea wa ngazi ya udiwani,ubunge na Rais.  Aidha amewashukuru wananchi,viongozi wa chama cha mapinduzi kuanzia ngazi ya wilaya hadi Taifa kwa kumuamini na kuona anafaa kuipeperusha bendera kwa tiketi ya CCM ili aweze kugombea ubunge jimbo Bukoba mjini. Kwa upande wasimamizi wa uchaguzi jimbo la Bukoba mjini Melkion Komba wakati akimkabidhi fomu...

Ahadi ya Serikali Kufikisha Umeme wa Gridi Kagera Yatekelezwa

📌 Dkt.Biteko ashuhudia utiaji saini mikataba itakayowezesha Wilaya zote Kagera kupata umeme wa Gridi 📌 Awali umeme mwingi ulikuwa ukitoka nchini Uganda hivyo kufanya Mkoa kutokuwa na umeme wa uhakika na wa kutosha 📌 Asema Rais.Dkt. Samia alishatoa maagizo ya mradi huo kutekelezwa kwa wakati na kwa usahihi 📌 Aagiza wananchi 1,014 waliopisha mradi kulipwa fidia kuanzia mwezi Septemba 2025 📌 Apongeza Wizara ya Nishati na TANESCO kwa ufanisi katika.usimamizi wa miradi Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na  Waziri wa Nishati Ahadi ya Serikali ya kufikisha umeme wa gridi ya taifa katika Wilaya zote za Mkoa wa Kagera imetekelezwa baada ya Serikali kusaini mikataba ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Benako, Ngara  hadi Kyaka  wilayani Misenyi na kituo cha kupoza umeme cha Benako cha msongo wa kilovoti 220/33, hatua inayotoa uhakika kwa Mkoa huo sasa kupata umeme wa gridi badala ya kutegemea umeme kutoka Uganda kwa kiasi kikubwa. Akizungumza ba...

Tanga mjini tutatiki kwa Dkt Samia- Ummy Mwalimu

  Aliyekuwa mbunge wa Tanga Mjini, Ummy Mwalimu leo Agosti 25, 2025 amewataka wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Tanga kuacha makundi na kujikita katika kutafuta kura za ushindi wa kishindo kwa Dkt. Samia Suluhu Hassani ambaye ni Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mauungano wa Tanzania kupitia CCM pamoja na kumuunga mkono mgombea ubunge wa jimbo la Tanga mjini ndugu. Kassim Mbaraka Amali na kukiwezesha Chama hicho kushinda katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 29 Octoba 2025. “Watu wa Tanga tunakila sababu za kumpa kura zote za ndio Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi nzuri alizofanya Tanga mjini na Taifa letu, hivyo nawaomba sana wanatanga twendeni tukamlipe hisani Dkt. Samia na kazi yetu iwe ni kutafuta ushindi wa Chama Cha Mapinduzi”

Majaliwa - Elimu ya Watu Wazima ni zana ya maendeleo endelevu

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema elimu ya watu wazima sio tu elimu ya masomo ya kawaida, bali ni zana muhimu ya maendeleo endelevu, kwani inachangia kipato, ustawi wa kijamii, afya na ushiriki wa kiraia. ameongeza kuwa uzoefu duniani unaonesha kwamba elimu ya watu wazima ni chombo muhimu cha maendeleo ya kijamii, kiuchumi na binafsi. Amesema hayo leo Jumatatu (Agosti 25, 2025) alipofungua kongamano la kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima inayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. “Elimu si tukio la muda bali ni safari endelevu ya kujifunza katika maisha yote, elimu ya Watu wazima si kwa ajili ya watu wazima pekee, bali hata kundi la vijana wanaweza kujiunga na kunufaika na program mbalimbali za ujuzi zinazotolewa na taasisi hiyo”.   Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inatambua kwamba katika kipindi cha nusu karne iliyopita, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima imepiga ha...