WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa Jukwaa la Nne la Biashara na Uwekezaji kati ya Afrika na Karibiani (ACTIF) linapaswa kuja na majibu ya changamoto za kibiashara na uwekezaji zinazoyakabili mataifa ya Afrika na yale ya eneo la Karibiani. Amesema kuwa changamoto hizo zinapaswa kujadiliwa kwa uwazi na kutaja bayana vikwazo vyote vinavyosababisha kutofanyika kwa biashara kati ya mataifa hayo Ameyasema hayo jana (Jumatatu, Julai 28, 2025) wakati akishiriki mjadala ya Wakuu wa Nchi na Serikali kwenye ufunguzi wa Jukwaa la Nne la Kibiashara na Uwekezaji kati ya Afrika na Karibiani (Afri-Caribbean Trade and Investment Forum-ACTIF 2025) linalofanyika katika kituo cha mikutano cha Radisson jijini St. George’s, nchini Grenada. Mheshimiwa Majaliwa anahudhuria jukwaa hilo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. “Mbali ya kujadili changamoto hizo, nchi zetu zinapaswa kutengeneza mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji na kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye mataifa...
Marato tv - Sauti ya Jamii