JESHI la Polisi Mkoani, Tanga limefanikiwa kuzima mtandao wa utapeli wa kidijitali na kuwaokoa vijana 87 waliokuwa wamenaswa kwenye mtego wa biashara haramu ya upatu, huku likiwashikilia wasimamizi wawili wa kundi hilo kwa tuhuma za kujipatia mamilioni ya fedha kwa njia ya udanganyifu. Operesheni hiyo kabambe iliyofanywa na Kikosi cha Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CID), imefichua madudu ya kampuni inayojiita Champions E-Commerce Education, ambayo imekuwa ikitumia kivuli cha mafunzo ya biashara mtandaoni kuwarubuni vijana kutoa kiasi cha kuanzia Sh600,000 hadi Sh Milioni 4 kwa ahadi ya utajiri wa haraka. Akithibitisha tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Almachius Mchunguzi, amesema vijana hao walikutwa wakiishi katika mazingira duni wakisubiri "utajiri hewa" huku watuhumiwa Mohammed Hamlima Idrisa (24) na Fidolini Hamisi Rashidi (21) wakiendelea kuratibu mkusanyiko huo haramu. "Vijana hawa waliahidiwa faida kubwa ndani ya muda mfupi baada ya kutoa mamili...
Marato tv - Sauti ya Jamii