Skip to main content

Posts

Showing posts from February 6, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu akichapa kazi ndani ya Treni akielekea Dar-es-Salaam

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesafiri kwa Treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) kutoka Dodoma kuelekea Dar es Salaa leo Februari 7, 2026.

Chuo Cha Polisi Wanamaji Mwanza Chakabidhiwa Boti ya Kisasa Kuimarisha Mafunzo na Usalama wa Majini

*Kutoka: Dawati la Habari Polisi Mwanza* Chuo cha Polisi Wanamaji Mkoa wa Mwanza kimepokea boti moja ya kisasa aina ya Fiber Speed Boat PB 23 PAPA, ikiwa ni hatua muhimu ya kuimarisha mafunzo kwa vitendo, doria za majini na usalama ndani ya Ziwa Victoria. Boti hiyo ilikabidhiwa rasmi tarehe 2 Februari, 2026, baada ya kubadilishiwa matumizi kutoka Makao Makuu ya Kikosi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam, kufuatia uamuzi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa kusogeza vitendea kazi karibu na maeneo ya utekelezaji wa majukumu. Akikabidhi boti hiyo kwa Mkuu wa Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza, SACP Ndagile Makubi, Mkuu wa Kikosi cha Polisi Wanamaji Tanzania, SACP Moshi Sokoro, alisema uhamisho wa boti hiyo unalenga kuongeza ufanisi wa mafunzo kwa wanafunzi wanaopata mafunzo chuoni hapo, hususan mafunzo ya uokoaji majini, doria, na operesheni maalum. SACP Sokoro alibainisha kuwa kwa muda mrefu chuo na kikosi cha Polisi Wanamaji vilikabiliwa na changamoto ya uhaba wa vitendea kazi vya kufundishia kwa v...

Tiseza Yawatia Moyo Wawekezaji wa Ndani

 Na Angela Sebastian; Missenyi  Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imefanya ziara katika kiwanda cha L and N Standerd Packaging Solution kilichopo Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera kinachomilikiwa na wawekezaji wazawa, kwa lengo la kuwatia moyo pamoja na kutoa elimu ya masuala ya uwekezaji na fursa zilizopo nchini.  Ziara hiyo iliyofanyika leo imelenga kuimarisha uelewa wa wamiliki wa viwanda kuhusu sera, taratibu na motisha zinazotolewa na serikali ili kukuza sekta ya viwanda na ajira kwa wananchi. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa TISEZA Balozi Aziz Mlima amesema kuwa, Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani ili waweze kupanua shughuli zao za uzalishaji na kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa nchini.  “Tupo hapa kuwatia moyo wawekezaji wazawa na kuwapatia elimu ya kina kuhusu fursa za uwekezaji, motisha zinazotolewa na Serikali pamoja na namna ya kunufaika na maeneo maalumu ya kiuchumi i...

Wasira:Vita Dhidi ya Rushwa Vinahitaji Mshikamano wa Jamii ‎

  ‎‎ ‎Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesema mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi nchini hayawezi kufanikiwa kwa juhudi za Serikali pekee, bali yanahitaji ushiriki wa wananchi na wadau wote wa maendeleo, wakiwamo vyama vya siasa. ‎Akizungumza Februari 5, 2026, mjini Bunda Mkoani mara  wakati wa maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa CCM, Wasira amesema rushwa bado ni changamoto kubwa inayokwamisha jitihada za maendeleo na kudhoofisha haki za wananchi. ‎ ‎Amesema kila Mtanzania ana wajibu wa kushiriki kikamilifu katika vita dhidi ya vitendo hivyo kwa kutoa taarifa pale anapobaini rushwa, badala ya kulalamika bila kuchukua hatua. ‎“Rushwa ni siri kati ya pande mbili, anayetoa na anayepokea. Mamlaka haziwezi kujua kinachoendelea bila ushirikiano wa wananchi,” amesema Wasira. ‎Aidha,amefafanua kuwa hata pale mtu anapolazimika kutoa rushwa ili kujiokoa, hapaswi kuishia hapo bali awasilishe taarifa kwenye mamlaka husika ili wahusika wachukuliwe...

Serikali Yaipongeza Khen Kwa Mtambo Mpya wa Laser wa Kusaidia Kupandikiza Mimba

Na Mwandishi Wetu KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Seif Shekalaghe, amezindua mtambo mpya wa kisasa wa teknolojia ya Laser ambao utasaidia kwenye uchambuzi wa viini tete wakati wa upandikizaji mimba ulioko katika Kituo cha kupandikiza mimba cha Kairuki Green IVF. Katibu Mkuu alipongeza Mtandao wa Afya na Elimu Kairuki (KHEN) kwa  kuanzisha kituo cha upandikizaji mimba na mchango wake wa muda mrefu kwenye sekta ya afya hapa nchini. Alitoa pongezi hizo leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua mtambo huo ulioko kwenye kituo ch Kairuki Green IVF  (KGIVF) kilichoko Bunju A  jijini Dar es Salaam. Uzinduzi wa teknolojia hiyo ya kisasa ulifanyika ikiwa ni kilele cha kumbukizi ya mwanzilishi wa Hospitali ya Kairuki, Chuo Kikuu Karuki na Mtandao wa KHEN, Hayati Profesa Kairuki aliyefariki mwaka 1999 na miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa kituo hichomwaka 2023. Dk Shelikaghe alisema anafurahi kuona urithi alioucha Profesa Kairuki unaendelezwa tena kwa ufanisi wa hali ya juu na kuahi...

Waziri Mkuu Achukizwa na Migogoro ya Ardhi

_Awasisitiza watendaji kuwafuata wananchi na kutatua kero zinazowakabili_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amewasisitiza Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya pamoja na watumishi wa umma wahakikishe wanatenga muda wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika maeneo yao hususani kwenye migogoro ya ardhi katika ngazi zao za kiutawala.  Ameyasema hayo leo Ijumaa, Februari 6, 2026 wakati wa kuahirisha Mkutano wa Pili wa Bunge la 13 jijini Dodoma, akisisitiza kuwa viongozi hao wanapaswa kuwafuata wananchi, kuwasikiliza na kuchukua hatua za haraka za kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wakiwa katika maeneo yao.   “Wafuateni, wasikilizeni na tatueni kero zao ili wasilazimike kwenda ngazi za juu au kusubiri ziara za viongozi wa kitaifa kwa masuala ambayo mngeweza kuyafanyia kazi.” Waziri Mkuu ameongeza kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka kuona wananchi wakihudumiwa ipasavyo. Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea k...

Agness Marwa ashinda ujumbe Kamati ya Bunge Sports Club

Dodoma   wa Viti Maalum Mkoa WA Mara Agnes Marwa amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Bunge Sports Club ukifuata mbunge leo katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma. Katika uchaguzi huo ulioshirikisha Waheshimiwa Wabunge zaidi ya Kumi na Tano, Agnes Marwa aliibuka mshindi baada ya kupata kura za kutosha zilizompa ushindi wa kuingia katika Kamati Tendaji ya klabu hiyo yenye wajumbe watano.  Kamati hii kazi yake ni pamoja na kuratibu shughuli za michezo kwa wabunge. Sauti mara baada ya kutangazwa kwa matokeo, Marwa aliwashukuru wabunge kwa imani waliyoonesha kwake na kuahidi kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu, uwajibikaji na uwajibikaji. Alisema michezo ni nyenzo muhimu ya kuimarisha afya, mshikamano na mahusiano mema miongoni mwa wabunge, hivyo atahakikisha Bunge Sports Club inazidi kuwa imara na yenye mafanikio. Kwa ushindi huo, Agnes Marwa anaungana na wengine wa Kamati Tendaji watakaosimamia mipango na maendeleo ya Bunge Sports Club kwa kipindi cha Miaka Mitano...

Tanzania Kuwa Kitovu Cha Usafirishaji – Waziri Mkuu

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema mipango inayoandaliwa na Serikali inalenga kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha usafiri na usafirishaji wa bidhaa, viwanda na biashara katika ukanda wa Afrika. Amesema Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2026/2027 – 2030/2031 una dhima ya mageuzi kwa ajili ya ukuaji wa uchumi jumuishi na uzalishaji wa ajira na kwamba unatarajiwa kuweka msukumo wa kipekee na kuleta mageuzi yatakayobadilisha mifumo, mitazamo na mwenendo katika utendaji. “Hatua hii itachochea tija katika uzalishaji, kuongeza uwezo wa nchi katika kushindana kikanda na kimataifa, na kuchochea muunganiko wa sekta mbalimbali. Lengo ni kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha usafiri na usafirishaji wa bidhaa, viwanda na biashara katika ukanda wa Afrika,” amesema. Ametoa kauli hiyo bungeni leo (Ijumaa, Februari 6, 2026) katika hotuba ya kuhitimisha mkutano wa pili wa Bunge wakati akielezea Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali katika muda wa Kati wa 2026/2027 – 2028/2029 na M...

Rc Kheri James Awataka Wahandisi wa Umwagiliaji Kutanguliza Uzalendo na Weledi Kulinda Fedha za Serikali

📍*NIRC Iringa.* Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, amewataka Wahandisi wa Mikoa na Wasimamizi wa miradi ya Umwagiliaji nchini kufanya kazi kwa uzalendo wa hali ya juu na weledi ili kuhakikisha uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali unaleta tija iliyokusudiwa kwa wananchi. Mhe. James ameyasema hayo mkoani Iringa wakati akifunga mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) yaliyohusu Usimamizi wa Mikataba, Sheria za Ununuzi, Uhandisi wa Geoteknolojia (Utafiti wa Miamba) na ubadilishanaji wa uzoefu. Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. James amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa miongozo na fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha sekta ya Umwagiliaji , akibainisha kuwa miradi hiyo ni tegemeo kubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kukuza uchumi wa taifa. “Serikali ya Awamu ya Sita imewekeza fedha nyingi; ni matarajio yetu kuwa miradi hii itatekelezwa kwa wakati, kwa viwa...