📌 Dkt. Biteko asisitiza Watanzania wasijaribu kuchezea amani 📌 Dkt. Biteko awataka Watanzania kuenzi, kudumisha Muungano Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema wananchi wa wilayani Arumeru, mkoani Arusha na Watanzania kwa ujumla wana kila sababu ya kumshukuru na kumuombea Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini. Dkt. Biteko amesema hayo leo Aprili 25, 2025 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Tengeru Wilaya ya Arumeru, Mkoa wa Arusha ambapo amesema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia wilaya ya Arumeru imepokea zaidi ya shilingi bilioni 100 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. “Arusha DC imepata fedha kiasi cha shilingi bilioni 49.6 na Wilaya ya Arumeru imepokea zaidi ya shilingi bilioni 51 kwa ajili ya shughuli na miradi mbalimbali ya maendeleo,” amesema Dkt. Bitek...
Marato tv - Sauti ya Jamii