Skip to main content

Posts

Showing posts from April 23, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Gavana wa Benki Kuu Afanya Mazungumzo na Rais Wa Kampuni ya Visa

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Kampuni ya VISA anayesimamia Ukanda wa Ulaya ya Kati, Mashariki ya Kati na Afrika, Bw. Andrew Torre. Katika kikao hicho, viongozi hao walijadili kwa kina namna mbalimbali za kupunguza gharama za miamala ya kifedha, kudhibiti uhalifu wa kimtandao, na kuimarisha utoaji wa elimu ya fedha kwa wananchi. Masuala hayo yanalenga kupunguza matumizi ya fedha taslimu pamoja na kuongeza upatikanaji na matumizi ya huduma rasmi za kifedha, hasa zile zinazotolewa kwa njia ya kidigitali. Aidha, kampuni ya VISA ilieleza dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania kwa kutoa mafunzo na kubadilishana ujuzi wa kitaalamu, ili kuimarisha mifumo ya malipo kuwa salama, rahisi na jumuishi kwa Watanzania wote. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Gavana, Dkt. Yamungu Kayandabila, Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Missango, Meneja wa Sera ya Fedha BoT, Bi. Asimwe Ba...

Dkt. Biteko Afurahishwa na Utatuzi Changamoto za Ardhi Monduli

📌 Azindua Shule ya Sekondari Migungani, awataka wanafunzi kutunza miundombinu 📌 Asema Serikali yajipanga kujenga mradi mkubwa wa umeme Monduli Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameupongeza uongozi wa Wilaya ya Monduli kwa jitihada zao za kutatua migogoro ya ardhi wilayani humo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la  Serikali la  kuwataka viongozi kutatua changamoto za wananchi katika maeneo yao. Dkt. Biteko ametoa pongezi hizo Aprili 23, 2025 wilayani Monduli, mkoani Arusha wakati akihutubia wananchi mara baada ya kuzindua Shule Mpya ya Sekondari ya Migungani iliyopo wilayani humo. “Naomba kuwapongeza tena uongozi wa Wilaya ya Monduli kwa kuendelea kufanya kazi nzuri sana hapa wilayani kwa maslahi mapana ya wananchi wa Monduli. Nimejulishwa kuwa, mmefanya mengi mno ikiwemo utatuzi wa changamoto na migogoro ya ardhi hapa wilayani. Nimejulishwa kuwa sehemu kubwa ya changamoto hizi mmefanikiwa kuzitatua ho...

Balozi Nchimbi Azungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu Ccm Mkoa wa Mara

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mara, kwenye kikao cha ndani kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Mara, leo Jumatano tarehe 23 Aprili 2025, akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku tano, mkoani humo. Ziara ya Balozi Nchimbi mkoani Mara inahusisha pia kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 - 2025, kupitia miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo, zinazotekelezwa na Serikali ya CCM, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano na Mwenyekiti wa CCM, katika kuwatumikia wananchi. Mapema kabla ya kikao hicho cha ndani, Balozi Nchimbi alitembelea na kukagua maendeleo ya miradi ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Musoma na Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambayo yote inajengwa mjini Musoma.  Akiwa katika ofisi hizo za CCM Mkoa wa Mara, Balozi Nchimbi pia alipata fursa ya...

Wanaokodi Watu Kuchafua Wabunge Walioko Madarakani Tutaonana Nao " Dkt.Nchimbi

Na Shomari Binda-Musoma  KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Dkt.Emanuel Nchimbi amesema wanaotaka nafasi ya ubunge na kuwachafua walioko madarakani hawatapita kwenye mikono yake. Kauli hiyo ameitoa leo aprili 23 kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM mkoa alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho kwenye kikao cha ndani. Amesema ni jambo la ajabu kuona wana CCM wanaandaa vijana kuwachafua na kuwazomea wabunge walioko madarakani na kudai kufanya hivyo ni kukichafua chama hicho. Dkt.Nchimbi amesema kamwe hawataweza kuwavumilia wanachama wanaofanya vitendo hivyo kwa kuwa ni utovu mkubwa wa nidhamu. Amesema yoyote atakayebainika kwenye vikao atakavyoshiriki yeye vya uteuzi halitapita jina la mwanachama huyo hata kama atashinda kwa kura nyingi. " Ipo tabia mbaya ambayo imeibuka ya kuwachafua wabunge waliopo madarakani hili halikubaliki na hatua zitachukuliwa kwa wanaofanya hivi. " Unapo mchafua mbunge kuwa hajafanya kitu ni kwamba unasema Chama hakijafanya kitu tusichafuan...

Sekta ya Madini yafikia Mchango wa Asilimia 10.1 Katika Pato la Taifa

▪️ *Rais Samia apongezwa kwa mageuzi makubwa ya sekta ya madini* ▪️**Wizara yafikia lengo kabla ya mwaka 2025** ▪️ *Sekta  Yatajwa Chanzo Kikuu kuingiza Fedha za Kigeni* ▪️ *Waziri Mavunde Awashukuru Watendaji, Watumishi na Wadau wa Sekta ya Madini* 📍 *Dodoma* Wizara ya Madini imetangaza kuwa Sekta ya Madini nchini Tanzania imepiga hatua kubwa ya kihistoria kwa kufikia mchango wa asilimia 10.1 katika Pato la Taifa mwaka 2024, ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya lengo lililowekwa kwenye Sera ya Madini ya mwaka 2009 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026). Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde leo Aprili 23, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, na kueleza kuwa mafanikio hayo makubwa yametokana na usimamizi na maelekezo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na  kwa uongozi wake mahiri uliopelekea sekta hiyo kufikia hatua hiyo muhimu mapema zaidi ya matarajio. “Ni jambo la...