Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, akiwasilisha Bungeni jijini Dodoma Mei 22, 2026, amesema Serikali imeendelea kuimarisha udhibiti wa bidhaa bandia nchini kupitia Mamlaka ya Ushindani (FCC) pamoja na taasisi nyingine husika. Amesema hadi Aprili 2026, FCC ilitekeleza operesheni maalum katika maeneo mbalimbali, hususan mkoa wa Dar es Salaam, ambapo jumla ya chupa 4,251 za vinywaji bandia zilikamatwa, pamoja na chupa tupu 286 na katoni tupu 250. Katika operesheni hiyo, pia vifaa vya uzalishaji na ufungashaji wa bidhaa hizo vilikamatwa, vikiwemo mashine za kuchapisha maelezo ya bidhaa, kipima kilevi, mashine za kufunga vifuniko, mizani, ethanoli pamoja na vifaa vya kuchanganyia na kuchujia pombe. Aidha, FCC imebaini uwepo wa bidhaa nyingine bandia za vipuri na vilainishi, ambazo pia zilikamatwa, huku wahusika wakichukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria. Waziri Kapinga amesema Serikali imeweka mkakati madhubuti unaolenga kuimarisha uchunguzi wa kiintelijensi...
Marato tv - Sauti ya Jamii