Skip to main content

Posts

Showing posts from October 8, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

AWESO: ELIMU NDIYO UWEKEZAJI WA UHAKIKA

NA: MWANDISHI WETU, PANGANI  Elimu imetajwa kuwa ndiyo uwekezaji wa uhakika kwa watoto na vijana kutokana na manufaa yake kuwa makubwa. Hayo yameelezwa na Mbunge wa Jimbo la Pangani na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, Oktoba 8, 2026, alipokuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Funguni, Jimboni humo. Aweso amesema, ni vizuri kwa wazazi na walezi, kuweka mkazo katika elimu, kwani uwekezaji huo unalipa katika ujenzi wa maisha ya vijana. "Leo ukilima unaweza kukosa mavuno, ukifanya biashara pia unaweza kukosa, lakini uwekezaji kwenye elimu una uhakika wa kufanikiwa katika maisha," amesema Aweso. Aidha, amesisitiza kuwa, ni vizuri wazazi na walezi wakawapa ushirikiano walimu katika kuwalea wanafunzi kimaadili na kitaaluma kwani ushirikiano wa pamoja ni nguzo ya mafanikio. "Wazazi tuwe kitu kimoja na walimu katika kuwalea watoto. Nidhamu ni muhimu katika  malezi ya watoto, hivyo tutoe ushirikiano kwa walimu ili vijana wetu wafanikiwe kitaaluma...

ZUNGU: TANZANIA READY TO SHARE EXPERIENCE ON MATERNAL AND NEWBORN HEALTH

 By TBN Reporter, Arusha Tanzania is ready to share its experience in improving access to maternal and newborn healthcare, reproductive health, nutrition and youth wellbeing, Speaker of the National Assembly Hon. Mussa Azzan Zungu has said. Hon. Zungu was speaking on 8 October 2026 at the opening of a forum on maternal and child health organised by the Tanzanian Government for delegates attending the 153rd Assembly of the Inter-Parliamentary Union (IPU). The meeting is taking place at the Arusha International Conference Centre (AICC). He said the health and wellbeing of women, children and young people were essential to national development. Tanzania, he added, looked forward to sharing its experience and working with partners to turn political commitments into lasting results. “Every preventable death, every unmet health need and every barrier to accessing care demands sustained attention and political action,” Hon. Zungu said. He noted that President Samia Suluhu Hassan had prior...

SPIKA ZUNGU: TANZANIA IPO TAYARI KUCHANGIA UZOEFU HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO

 Na Ripota wa TBN, Arusha. Sika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu amesema Tanzania ipo tayari kuchangia uzoefu wake katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za mama na mtoto mchanga, afya ya uzazi, lishe na ustawi wa vijana. Mheshimiwa Zungu ameeleza hayo Oktoba 8, 2026, wakati akitoa hotuba ya ufunguzi katika mdahalo kuhusu masuala ya afya ya mama na mtoto uliondaliwa na Serikali ya Tanzania wa wajumbe wa Mkutano wa 153 Umoja wa Mabunge Duniani.  Mkutano huo unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC). Mheshimiwa Spika amesema afya na ustawi wa wanawake, watoto na vijana ni msingi wa maendeleo ya Taifa na kwamba Tanzania inatarajia kuchangia uzoefu wake na kufanya kazi na washirika kugeuza dhamira ya kisiasa kuwa matokeo ya kudumu. “Kila kifo kinachozuilika, kila hitaji la kiafya lisilotimizwa na kila kikwazo cha kupata huduma,kinahitaji umakini na hatua endelevu za kisiasa. “Ndio maana Rais wangu Mhe. Rais Hassan amewe...

WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAISBL SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO.

 Arusha, Oktoba 8, 2026  Wabunge kutoka Kundi la Kijiografia-Kisiasa la Bara la Afrika kupitia Umoja wa Mabunge ya Duniani (IPU) wameunga mkono ajenda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuimarisha afya ya uzazi, mama, mtoto na vijana barani Afrika. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Arusha katika mkutano wa pembezoni wa Mkutano wa 153 wa IPU, ambapo viongozi hao pamoja na wadau wa maendeleo ya Sekya ya Afya Duniani wamejadili umuhimu wa kuimarisha sera, mifumo ya utoaji huduma, uwekezaji na uwajibikaji katika sekta ya afya. Kiongozi wa Kundi la Kijiografia-Kisiasa la Wabunge wa Bara la Afrika kupitia IPU, Mhe. Ali Kolotou Tchaïmi, amesema wakati umefika kwa nchi za Afrika kuunganisha nguvu, kujifunza kutoka kwa kila mmoja na kuwa na agenda ya pamoja ya kuboresha afya ya mama na mtoto. Kwa Upande wae Rais wa Umoja wa Mabunge ya Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amesema juhudi za Rais Samia katika kuimarisha afya ya uzazi zinapaswa ku...

ASKOFU BUNDALA ATOA NENO JAMII KUSHIRIKIANA NA POLISI

  Kutoka: Dawati la Habari Polisi Mwanza.  Askofu wa Kanisa la TGC, Robert Bundala amewataka wananchi kuiona Jeshi la Polisi kama sehemu ya jamii na si chombo kilicho mbali nao huku akisisitiza kuwa ushirikiano kati ya viongozi wa dini, Polisi na wananchi ni muhimu katika kuimarisha amani na usalama. Askofu Bundala ameyasema hayo Oktoba 08,2026 wakati wa ziara ya watumishi wa dini waliotembelea Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza na kukabidhi mipira kwa ajili ya shughuli za michezo, hatua iliyolenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Polisi na jamii. Amesema viongozi wa dini na Jeshi la Polisi wana majukumu yanayokaribiana katika kuelimisha jamii, kuzuia maovu na kuwasaidia watu kurejea katika mwenendo mwema. Amesema viongozi wa dini wanashirikiana na Polisi katika masuala mbalimbali, ikiwemo kutoa elimu kwa jamii na kushiriki katika kukemea uovu, shughuli za ulinzi na usalama, hususan katika maeneo ya nyumba za ibada. “Polisi si watu waliotoka Mbinguni. Polisi n...

ASKOFU BUNDALA ATOA NENO JAMII KUSHIRIKIANA NA POLISI

Kutoka: Dawati la Habari Polisi Mwanza.  Askofu wa Kanisa la TGC, Robert Bundala amewataka wananchi kuiona Jeshi la Polisi kama sehemu ya jamii na si chombo kilicho mbali nao huku akisisitiza kuwa ushirikiano kati ya viongozi wa dini, Polisi na wananchi ni muhimu katika kuimarisha amani na usalama. Askofu Bundala ameyasema hayo Oktoba 08,2026 wakati wa ziara ya watumishi wa dini waliotembelea Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza na kukabidhi mipira kwa ajili ya shughuli za michezo, hatua iliyolenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Polisi na jamii. Amesema viongozi wa dini na Jeshi la Polisi wana majukumu yanayokaribiana katika kuelimisha jamii, kuzuia maovu na kuwasaidia watu kurejea katika mwenendo mwema. Amesema viongozi wa dini wanashirikiana na Polisi katika masuala mbalimbali, ikiwemo kutoa elimu kwa jamii na kushiriki katika kukemea uovu, shughuli za ulinzi na usalama, hususan katika maeneo ya nyumba za ibada. “Polisi si watu waliotoka Mbinguni. Polisi ni ndugu...

IPU 153: ZUNGU AKUTANA NA 12 PLUS GROUP ARUSHA

 Rais wa Mkutano wa 153 wa IPU na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), amekutana na wajumbe wa umoja wa kundi la Kijografia na Kisiasa (12 Plus Group). Mazungumzo yao yamelenga  kuratibu sera, mitazamo, na msimamo mbalimbali inayojadiliwa kwenye mkutano wa 153  wa IPU. Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 8 Oktoba, 2026 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC).