Na Zainab Ally-Mikumi. Ikiwa ni Siku moja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kuzindua Reli ya Mwendokasi (SGR) watalii ambao ni watumishi wa kada ya ualimu zaidi ya 1000 kutoka mkoa wa Dar es Salaam wametumia usafiri wa reli hiyo kutembelea Hifadhi ya Taifa Mikumi. Ziara hiyo iliyoratibiwa na Ofisi ya mkoa wa Dar es Salaam imelenga kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Rais Samia ikiwemo kutangaza vivutio vilivyopo Hifadhi za Taifa ambapo kwa umoja wao walichagua Hifadhi ya Taifa Mikumi lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia. Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es salaam Dkt. Toba Nguvila, amesema kuwa watalii hao ambao ni walimu wa mkoa wa Dar es Saam wameamua kuchangisha fedha zao wenyewe kwa ajili ya kuja kutembelea Hifadhi ya Taifa Mikumi kwa kutumia usafiri wa reli ya kisasa ya SGR lengo likiwa ni kumuunga mkono Rais Samia. “Baada ya Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kuizindua reli hii, walimu wa mkoa wa Dar es Salaam w...
Marato tv - Sauti ya Jamii