Skip to main content

Posts

Showing posts from December 31, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Samia ameiheshimisha Tanzania Matumizi ya Nishati safi-Majaliwa

  _Asema Watanzania tunapaswa kumuunga mkono_   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiheshimisha Tanzania katika hamasa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kutokana na umuhimu wake kwenye afya ya binadamu na utunzaji wa mazingira. Amesema kuwa kutokana na jitihada hizo, mashirika ya kimataifa yameonesha nia ya kumuunga mkono ikiwemo kufanya mkutano mkubwa wa nishati safi Afrika hapa nchini. “Watanzania tumuunge mkono Rais Dkt. Samia katika kampeni hii na kuhakikisha tunaongoza kwenye matumizi ya nishati safi barani Afrika” Amesema hayo leo (Jumanne, Desemba 31, 2024) wakati wa Tamasha la Azimio la Kizimkazi ambalo lilienda sambamba na ugawaji wa majiko 1000 ya gesi kupitia kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia. Tukio hilo limefanyika katika eneo la Kilimahewa Majumbakumi, Ruangwa mkoani Lindi. “Tunapaswa kumuunga mkono kwasababu agenda imeanzishwa na Rais wetu, dunia lazima iitambue Tanzania kama ambavyo imetambua na kuleta mku...

Wananchi wa Ngombo Waendelea Kulipwa Fidia

Na Beatus Maganja, Malinyi. Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba amesema zoezi la kuwalipa fidia wananchi wa Kijiji cha Ngombo kilichopo ndani ya Pori la Akiba Kilombero Mkoani Morogoro linaendelea vizuri ambapo asilimia 93 ya wananchi wote tayari wamekwishalipwa fidia zao kwa ajili ya kupisha shughuli za uhifadhi katika Hifadhi hiyo na asilimia 7 ya wananchi waliosalia wanaendelea kushughulikiwa ili kukamilisha malipo yao. Akizungumzia zoezi hilo Desemba 31, 2024 wilayani humo Mhe. Sebastian amesema Serikali imetoa zaidi ya shilingi billioni 6.9 kulipa wananchi 1,056  ili waweze kuhama kwa hiari kutoka maeneo ya Hifadhi huku akitoa maelekezo kwa watendaji wa vijiji 32 wilayani Malinyi kuwapokea ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku. "Kwanza si kweli kwamba wananchi wa Ngombo hatujawaambia mahali pakwenda. Katika barua yangu ya tarehe 4 Disemba, 2024  niliyowaandikia watendaji wa vijiji 32 vilivyo ndani ya wilaya ya Malinyi, nilitoa maelekezo ya kuwapok...