Mbunge wa jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Ridhiwani Kikwete leo Amefanya mkutano Kiwangwa na kuwapongeza wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwa mfumo wa Kidijitali Hata hivyo Mhe. RIdhiwani Amezunguka katika matawi mbalimbali na kuzungumza na wanachama wapya wa CCM na kuwasisitiza wananchi kuhusu uandikishaji wa kadi za kupiga kura kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa vijiji na vitongoji pamoja na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 . Pamoja na kukumbushana na kuwapongeza Wananchi , Ndugu Kikwete amewakumbusha wananchi wa Kiwangwa kuendelea kuiunga Mkono Serikali inayoongozwa na Rais @SuluhuSamia kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika maendeleo ya Kata ya Kiwangwa .
Marato tv - Sauti ya Jamii