Skip to main content

Posts

Showing posts from April 2, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Dkt. Mwinyi Azindua Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026, Asisitiza Amani, Uzalendo na Uwajibikaji

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewataka Watanzania kulinda, kuimarisha na kudumisha Muungano wa Tanzania, amani, utulivu na umoja wa kitaifa kama msingi wa maendeleo endelevu. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 02 Aprili , 2026 wakati wa uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 uliofanyika Uwanja wa Gombani, Pemba. Aidha, Rais Mwinyi amesema taasisi zote nchini na wananchi kwa ujumla wana wajibu wa kuheshimu utu, haki, usawa na utawala wa sheria ili kuendeleza mshikamano wa Taifa. Ameeleza kuwa Mwenge wa Uhuru unaendelea kuwa chombo muhimu cha kuhamasisha uzalendo, uwajibikaji na mapambano dhidi ya maadui wa maendeleo wakiwemo umasikini, ujinga na maradhi.  Vilevile, amewahimiza Watanzania kupinga ubaguzi wa aina yoyote na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na rushwa, dawa za kulevya na magonjwa kama UKIMWI na malaria. Halikadhalika,  Rais Dkt. Mwinyi amebainisha kuwa Serikali inaendelea kuima...

Bajeti za Mashirika ya Umma kuchambuliwa kuakisi Dira 2050

Na Mwandishi wa OMH Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) imeanza zoezi la uchambuzi wa mipango na bajeti za taasisi na mashirika ya umma, likilenga kuimarisha mchango wa taasisi hizo katika utekelezaji wa Dira 2050. Akizungumza kuhusu zoezi hilo, Alhamis, Aprili 2, 2026, Bw. Joseph Mwaisemba, Mkurugenzi Msaidizi wa Tathmini ya Mashirika yasiyo ya kibiashara (kwa upande wa mamlaka za udhibiti), alisema jumla ya watumishi 50 wa OMH wamekutana katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere kwa ajili ya kuchambua bajeti za taasisi na mashirika ya umma 252. Alisema uchambuzi huo unalenga kuangalia namna taasisi hizo zilivyojipanga katika kutekeleza Dira 2050 sambamba na Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP IV). “Tunachofanya hapa ni kuangalia kwa kina mipango ya taasisi na mashirika ya umma ili kuona namna inavyochangia utekelezaji wa Dira 2050 na mipango ya maendeleo ya taifa kwa ujumla,” alisema. Aidha, alieleza kuwa zoezi hilo pia linahusisha uchambuzi wa mika...

Jitihada za Rais Samia Zazidi Kuinua Sekta y Utalii

Na Sixmund J. Begashe, Dodoma Jitihada kubwa zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo zimetambuliwa kitaifa, kikanda na kimataifa zimechechemua kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa watalii nchini. Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Bungeni Jijini Dodoma kwenye hotuba yake kuhusu Mapato na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa Mwaka 2026/2027. Dkt. Mwigulu amesema kutokana na uhuhimu wa Sekta ya Maliasili na Utalii katika ukuaji wa uchumi, ajira na pato la Taifa, Serikali imeendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ili kuinua sekta hiyo muhimu kwa uchumi wa nchi yetu. “Mikakati hiyo imeongeza idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi za Taifa kwa asilimia 10.73 kutoka watalii 5,360,247 mwaka 2024 hadi 5,935,561 mwaka 2025 na hivyo ku...