Skip to main content

Posts

Showing posts from December 14, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais na Amiri Jeshi Mkuu Akipokea Heshima Baada ya Kuwasili Skua Mkoani Tanga

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga (SKUA) mkoani Tanga kwa ajili ya kufungua mkutano wa 9 wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Makamanda, tarehe 15 Desemba, 2025.

Dkt. Mwigulu Awasili Songea Kushiriki Misa ya Kuaga Mwili wa Jenista Mhagama

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba Leo Desemba 15 amewasili Mjini Songea ambako atashiriki katika Ibada ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Jenista Mhagama aliyekuwa Mbunge wa Peramisho na Waziri Mstaafu, inayofanyika kwenye Kanisa Katoliki Peramiho. Jenista Mhagama alifariki Desemba 11, 2025 kwa maradhi ya moyo.

Katibu Mkuu wa Umoja Wa Mataifa Ataja Tanzania Kuwa Kinara wa Amani na Mshikamano Afrika na Duniani

 Ujumbe kutoka kwa Mheshimiwa António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo tarehe 14 Desemba 2025, wakati wa kupokea Ujumbe Maalum kutoka Tanzania. “Tanzania imekuwa rejea na mfano wa kuigwa katika masuala ya amani na mshikamano wa kijamii barani Afrika na duniani kote,” alisema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, alipokuwa akipokea Ujumbe Maalum. Sifa ya Tanzania kama kinara wa amani ilijaribiwa katika uchaguzi wa hivi karibuni uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025, lakini taifa lilifanikiwa kuvuka jaribio hilo la kwanza kwa mafanikio. “Umoja wa Mataifa ungependa kuona Tanzania ikiendelea kubaki kuwa taifa lenye umoja na mfano bora wa kuigwa,” alisema Katibu Mkuu Guterres alipokuwa akipokea Ujumbe Maalum uliobeba ujumbe kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, uliowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi ...

Waziri Mkuu: Watanzania Tunzeni Akiba ya Chakula

*_Ahimiza matumizi ya mbolea na mbegu za mazao ya muda mfupi_* WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania watunze akiba ya chakula walichonacho na waepuke matumizi yasiyofaa kutokana na hali ya kuchelewa kwa msimu wa mvua. Waziri Mkuu ametoa wito huo leo jioni (Jumapili, Desemba 14, 2025) wakati akizungumza na baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma. Amewaeleza viongozi hao kutoka mikoa ya Dodoma na Singida kwamba Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitoa utabiri wa mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli na mvua za msimu kwa kipindi cha Oktoba 2025 hadi Desemba 2025 na kipindi cha mwezi Novemba, 2025 hadi Aprili 2026 mtawalia.  “Kutokana na utabiri huo, baadhi ya mikoa nchini inatarajiwa kuwa na mvua za chini ya wastani hadi wastani na kutawaliwa na vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko wa mvua usioridhisha,” amesema.  Amesema tathmini hiyo ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inaonesha hali ya kuchelewa kwa mvua inatarajiwa k...

Makamu wa Rais Awasili Mkoani Kagera Kwa Ziara ya Kikazi

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba mkoani Kagera leo tarehe 14 Desemba 2025. Makamu wa Rais anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mkoa wa Kagera, itakayofanyika tarehe 15 Desemba 2025.

Mwili wa Jenista Mhagama Wapokelewa na Spika wa Bunge Mjini Songea

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu akiongoza waombolezaji kupokea mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Mhe. Jenista Mhagama wakati ulipowasili katika uwanja wa ndege wa Songea Mkoani Ruvuma leo tarehe 14 Desemba, 2025.